Adeladius Makwega TANGA

Mbozi ni Wilaya iIiyotokana na Kijiji kimoja kilichopo jirani na Mji Mdogo wa Vwawa kinachoitwa Mbozi. Kwa mazungumzo ya watu wa asili ya Mbozi, Kjiji cha hiki ndicho kilianza kabla ya jina hilo kutumika kuitambulisha wilaya hiyo ambayo awali ilikuwa katika Mkoa wa Mbeya na sasa ipo mkoa Mpya wa Songwe.

Mtu akiwa Vwawa anapokwenda kijiji cha Mbozi huwa anapita katika kata ya Ichenjezya na pia kata ya Isanga na hapo kuna vijiji vya Isangu, Shanko alafu anatelemka bonde anakutana na Mto Khana akiuvuka mto huo ndiyo anafika kijiji chenye jina la Wilaya ya Mbozi. Mto Khana wenyewe unayamwaga maji yake katika Mto Momba na wengine wakidai kuwa maji haya yanafika hadi Mto Songwe.

Kwa miaka kadhaa ya nyuma Mkoloni alijenga daraja lililokuwa linauganisha Vwawa na kijiji cha Mbozi. Mvua kubwa ilionyesha ikalibomoa daraja hilo kwa hiyo mawasiliano baina ya Kijiji cha Mbozi na Vwawa yakawa ya tabu kwa kuzunguka kupitia eneo linalofahamika kama Karasha, Matura alafu unaingia Kijiji cha Mbozi chenye Kituo cha Afya Cha Mbozi Misheni.

Baada ya daraja kubomoka kwa muda mrefu ziliombwa pesa za kujenga daraja hilo na baadaye Mungu Bahati Serikali ikatoa pesa kwa bajeti ya ujenzi kupitia TARURA na ujenzi kuanza. Wakati huo TARURA ndiyo imeanza kazi chini ya TAMISEMI ya Katibu Mkuu TAMISEMI Injinia Iyombe na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano alikuwa Balozi Injinia Kijazi.

TARURA Wilaya walikuwa sasa wanajisimamia wenyewe chini ya Mkuu wa Wilaya na TARURA MKOA na siyo tena chini Halmashauri ya Wilaya (Mkurugenzi na Baraza na Madiwani). TARURA walikuwa wanafanya kazi kwa moyo wote kuonesha kuwa sasa wanajisimamia wao wenyewe japokuwa walikuwa bado chini ya TAMISEMI.
Ujenzi ukafanyika, ukakamilika na daraja hilo likawa miongoni mwa miradi mitano iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 katika Wilaya ya Mbozi. Injinia aliyekuwa anasimamia mradi huo namkumbuka kwa jina moja tu la Chaula.
Mwenge ulifika katika mradi huo baada ya kuvuka daraja hilo na kuwekwa kando ya eneo jirani na daraja na shuguli za kuzindua zikaanza.

Ikasoma taarifa ya mradi, Huku Saluti kwa Mwenge zikitolewa kweli kweli, zikitajwa takwimu za wanufaika wa mradi huo na kadhalika.Mkimbiza mwenge alishaugakua mradi huo,. yakaulizwa maswali mengi naye injia wa wilaya akiyajibu .

Msumari wa mwisho wa jeneza hilo kutoka kwa mkimbiza mwenge ulikuwa ni kwanini takwimu alizopewa na mkoa hazifanani na takwimu zilizosomwa na za Injini wa Wilaya? Hapo mwanakwetu yakaanza mazungumzo mengi baada ya habari. Tamati mradi haukufunguliwa kwa hoja hiyo hiyo ya tofauti ya takwimu.

Watu wakabaki wanashanga, jamani mradi huo wa pili, jamaa wamegoma kuufungua tena. Watu tukaingia katika magari kwenda kwenye mradi mwingine. Wakati hilo linafanyika mama mmoja akasema maneno haya ya Kinyia.

“Shoni mwalihanile idalaji, mukuti libhibhi litali nubhubora alfu amagari na bhantu bhakwendelela kutuha!”

Mwanakwetu nilimuuliza dereva niliyekuwa naye jirani mama huyu anasema nini?

Akanijibu kuwa,

“Kwa nini mmelikataa daraja, nakusema ni baya na halina ubora wakati huo huo magari na watu wanaendelea kupita!”

Kwa ukweli wa Mungu hata gari ya mwenge lilipita hapo hapo na hata wakimbiza Mwenge viatu vyao vya mabuti vilikanyaga juu ya daraja hilo.

Binafsi nilijiuliza hiyo tofauti ya takwimu kwa wananchi wanaolitumia daraja hilo ni ngumu kukuelewa, huku Daraja la Mto Khana likiwahudumia wananchi wa Majimbo Mawili ya Vwawa na Mbozi ukiwa ndiyo mpaka wa majimbo haya mawili.


Mwanakwetu jioni ya siku wananchi wa wilaya Mbozi walijitokeza katika viwanja vya Mlowo katika mkesha wa Mwenge wa Uhuru kutumbuizwa na mwanamuziki Vitalis Maembe na nyimbo zake kama vile SUMU YA TEJA, AFRIKA SHILINGI TANO, KUDU, SALAMA na nyingine nyingi.

makwadeladius@gmail.com

0717649257 



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...