Na John Mapepele.
Serikali ya Tanzania na China zimetiliana Saini
mkataba wa makubaliano ya kusaidiana katika kuboresha maeneo ya Sekta
anazozisimamia.
Utiaji wa Saini wa mikataba hiyo ya kihitoria
umeongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Mhamed Omary
Mchengerwa kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Balozi wa China nchini Chen Mingjian kwa upande wa Serikali ya watu wa
China kwenye Ofisi ya Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
kuhusiana na manufaa ya mikataba hiyo, Mhe. Mchengerwa amesema Serikali
ya Tanzania imesaini mikataba hiyo ya ushirikiano inatarajia kuleta
mapinduzi makubwa kwenye sekta hizo.
Amesema kwa upande wa
utamaduni kutakuwa na kupeleka wadau wa utamaduni, sanaa na michezo
katika nchi ya china na watu wa china kuja nchini kwa ajili ya
kubadilishana uzoefu.
Kwa upande wa elimu Tanzania itapeleka
wanafunzi ambapo China itafadhili masomo haya kwa kutoa nafasi 120
kwenda kwenye maeneo ya lugha, utamaduni, sanaa na maeneo mengine ya
hinsia (humanities) kila mwaka ambapo Tanzania itatoa ufadhili wa
nafasi 15 kwa ajili ya wachina kuja Tanzania kusoma hasa kwenye maeneo
ya hinsia(humanities) pamoja na maeneo ya lugha.
Aidha, amesema
mkataba huu unatarajiwa kutoa nafasi kwa wataalam kwenye maeneo ya
sekta hizo zote. Pia imeelezwa kuwa Serikali ya China inatarajia kujenga
vituo vya kisasa vyenye miundombinu yenye viwango vya kimataifa vya
sanaa na utamaduni ambavyo vitatumika na wasanii wa hapa nchini katika
kuzalisha kazi zao zenye ubora ambazo zitauzwa duniani.
“Ni
jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kuwa wasanii wetu wanakwenda kupata
studio za kisasa kabisa kwa ajili ya kuzalisha kazi zao”amefafanua
Mhe. Mchengerwa.
Aidha, amesema Tanzania inaamini kuwa Tanzania
imebarikiwa kuwa na utamaduni uliosheheni vitu vingi kutokana na kuwa na
makabila ambayo ni zaidi ya 120.
Amesema kulingana na mikataba
hiyo Serikali za nchi zote zinakusudia kuchangamsha utamaduni na sanaa
ili ziwe kwenye kiwango halisi tofauti na sasa ambapo inaonekana kuwa
kutochangamka kwa kiwango hicho.
Katika ziara hiyo Waziri
Mchengerwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Dkt, Hassan Abbasi na Wakurugenzi wa Sekta za Utamaduni na Sanaa kwenye
Wizara hiyo, ambapo kwa Serikali ya China Mhe. Balozi Chen Mingjian
ameambatana na watendaji waandamizi kwenye sekta hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...