Na.WAF-Geneva

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelipongeza shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kutoa usaidizi wa kitaalamu na misaada ya kibinadamu katika kukabiliana na magonjwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Dkt. Catherine Joachim  wakati wa mkutano wa 75 wa Shirika Afya duniani.

Dkt.Catherine amesema shirika hilo limepata mafanikio baada ya kuwa bega kwa bega na nchi wanachama katika kudhibiti athari za UVIKO-19.

"Shirika la Afya Duniani (WHO) haliwezi kufikia malengo iliyojiwekea bila ya kuwa na vyanzo vya fedha vilivyo endelevu katika kuendesha programu za Afya Duniani. "Amesema Dkt. Catherine

Aidha, amesema kikosi kazi cha wataalamu cha masuala ya ugharimishaji wa shirika hilo wamependekeza kuona umuhimu wa nchi wanachama kuongeza michango.

Hata hivyo wamesema mkakati wa kuongeza michango uende sambamba na kuimarisha uwajibikaji wenye tija na uwazi katika matumizi ya fedha za shirika hilo.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...