Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imeshiriki Maonesho ya Tano ya Mifuko ya Programu za Uwezeshaji wananchi kiuchumi, ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamhuri, Mjini Morogoro.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu *"Uchumi Imara Kwa Maendeleo endelevu"*, yalizinduliwa rasmi Mei 9, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela, ambapo taasisi za umma na binafsi zimeshiriki.

TAWA imetumia Maonesho hayo kujitangaza na  kubainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika shirika hilo zikiwezo fursa za malazi na ufugaji wa Wanyamapori hai.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho hayo, Afisa Mhifadhi kutoka TAWA, Imani Mkonda,  amewakaribisha Watanzania na raia wa kigeni kufika katika Maeneo ya TAWA kujionea fursa za uwekezaji ili wawekeze.

"Kama mtakumbuka Mhe. Rais (Samia Suluhu Hassan) amezindua Royal Tour ambayo tunaamini itaongeza idadi ya watalii wa ndani na wa nje ambao watafika kutembea katika maeneo yetu.

"..hivyo  tunawaalika Watanzania na wale ambao wasio Watanzania kufika katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA ili kuwekeza katika miundombinu ya malazi, kwa maana ya Logde, hoteli na kambi za kitalii (camps)," amesema.

Naye Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja, ametumia fursa hiyo kubainisha maeneo yaliyotengwa na TAWA kama fursa kwa kila Mtanzania na asiye Mtanzania kuwekeza 'loji', hoteli pamoja na kambi za Kitalii kuwa ni Pori la Akiba Mpanga/Kipengere (Mikoa ya Njombe na Mbeya), Pori la Akiba Swagaswaga (Dodoma), Pori la Akiba Pande (Dar es Salaam) na Pori la Akiba Kijereshi (Simiyu).

Maeneo mengine yaliyotajwa ni Pori la Akiba Wami Mbiki (Morogoro), Bustani za Wanyamapori Tabora na Ruhila iliyopo Manispaa ya Songea na Maeneo ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara (Lindi).

Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo Mei 14, 2022 na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...