Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
Jumla
ya watoto 256,186 sawa na asilimia 127 walio chini ya miaka mitano
mkoani Pwani, wamefikiwa kwenye Kampeni ya chanjo ya matone (POLIO)
inayosaidia kujenga Kinga na kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa huo.
Lengo la mkoa ilikuwa ni kufikia watoto 200,967 hivyo kuwa na ongezeko kwenye malengo yao kwa kuwafikia watoto 55,222.
Mratibu
wa chanjo Mkoani Pwani,Abbas Hincha alieleza ,zoezi limekamilika lakini
vituo ambavyo vipo chini ya malengo yaliyotakiwa vinaendelea na kutoa
chanjo katika maeneo Yao.
";Kampeni hii imefanyika ,kufuatia
february17 mwaka huu nchi ya Malawi kutoa tamko la kuwepo kwa mlipuko wa
ugonjwa huo , baada ya mtoto mmoja kutoka Mji Mkuu wa Lilongwe
kuthibitika kuwa na ugonjwa huo."alifafanua Hincha.
Hata hivyo
,alisema kampeni hiyo,imefanyika nyumba kwa nyumba na katika vituo vya
afya, kuanzia Mei 18 hadi Mei 21 ndani ya mkoa huo.
Alibainisha,
watoto chini ya miaka mitano wamepata chanjo hii bila kujali kama
walishapata chanjo katika ratiba zao za kawaida ya chanjo.
Aliitaka ,jamii itambue usalama wa chanjo hiyo , kwani Ni Kama chanjo nyingine.
Vilevile Hincha alisema kuwa, ugonjwa huo hauna tiba ila hukingwa na chanjo ya Polio ambayo ipo katika mfumo wa matone .
Hincha
alisema, chanjo ni ileile inayotumika miaka yote lengo ni kuongeza
kinga , kuzuia mlipuko na kudhibiti watoto wasipatwe na virusi vya
ugonjwa huo.
Alieleza , kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata
mgonjwa wa Polio Julai 1996 hivyo kampeni hii inatarajiwa kufanyika
katika nchi zinazopakana na Malawi ikiwemo Zambia,Msumbuji, na Zimbabwe .
Ugonjwa
wa polio unasababishwa na kirusi cha polio ambacho huambukizwa kutoka
kwa mtu alieathirika kwenda kwa mwingine kwa kunywa au kula chakula ama
kinywaji kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa wa
polio.Virusi vya polio huzaliana katika utumbo na huweza kuathiri mfumo
wa fahamu ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa viungo ndani ya
masaa machache hata kupelekea kifo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...