Na Janeth Raphael - Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema Serikali ya Mkoa wa Dodoma ina nafasi kubwa katika kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa mkoa wa utalii nchini.

Mtaka amesema hayo usiku wa royal tour katika uzinduzi wa Filamu ya “Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre.

Mtaka amesema Mkoa wa Dodoma una sehemu mbalimbali za utalii ikiwemo utalii wa michoro ya mapango Kondoa , Dodoma ,utalii wa Zabibu.

Aidha,Mtaka amesema ,katika mkoa wa Dodoma una utalii wa miradi mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za mkoa.

“Dodoma tuna utalii wa miradi,tunatamani kila mtanzania apate fursa ya kuwekeza katika mkoa wa Dodoma ,tutahakikisha tunachepusha sekta binafsi mkoa wa Dodoma,na kuhakikisha unakuwa mkoa kila mfanyabiashara ananufaika na makao makuu ya nchi”amesema.

Kuhusu utalii wa mikutano Mkuu huyo wa mkoa amesema sasa mkoa wa Dodoma una una sehemu mbalimbali ya mikutano hivyo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta binafsi.

“Tunahamasisha utalii wa mikutano,watu waone ni fursa kubwa katika mkoa wa Dodoma ,Dodoma ni mji wa serikali itapendeza Zaidi katika kusaidia na kuchochea ukuaji wa sekta binafsi.

Uzinduzi wa Royal Tour Mkoa wa Dodoma umezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa kwa niaba ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere,Waziri wa Maliasili na Utalii,Pindi Chana,Spika wabunge Dkt.Tulia Ackson ,wananchi na wafanyabiashara mkoa wa Dodoma ambapo unarushwa mbashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari 

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana akimsikiliza Mkuu wa MKoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka

nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...