KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo ametoa wito kwa Wasimamizi wa miradi mbalimbali kusimamia kwa umakini miradi hiyo ili Wananchi waone matokeo ya haraka kwa kunufaika na utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na Serikali kwenye maeneo mbalimbali kote nchini.
Ndugu Chongolo ameyasema hayo alipopita kukagua mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka, eneo la Malampaka, Maswa mkoani Simiyu, Ujenzi wa Reli yenye urefu wa Kilometa 341 (KM 249 njia kuu na KM 92 njia za kupishana), amesema kuna haja ya kwenda na Spidi kubwa ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
“Haipendezi, tunafika miezi 36 ya mkataba huku bado tupo nyuma miezi Tisa au Kumi, katika mradi huu malizeni ‘Gap’ iliyobaki sasa ili twende na Spidi ya matokeo kwa muda tuliojiwekea”, amesema Chongolo.
“Nipongeze hatua zinazoendelea kwenye ‘route’ ya kwanza ambayo inaunganisha hadi njia ya umeme na ya pili kufikia asilimia 80%, hizi ni hatua kubwa niwapongeze kwa sababu Wananchi wetu wa Tanzania wanataka kuona matokeo, wanataka kuona wanatoka asubuhi Dodoma wanaenda kunywa Chai Dar es Salaam, na unakuja kula Chakula cha Mchana Dodoma”, ameeleza
Kwa upande wake Meneja Mradi wa SGR - TRC, Mhandisi Machibya Masanja amesema tayari hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni 400 katika kutekeleza mradi huo wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Mwanza hadi Isaka, amesema kuna mpango wa kuwajengea uwezo Watanzania kunufaika na ujenzi wa Mradi huo kwa kuwa na Watanzania zaidi ya asilimia 70% wakati hapo baadae unatarajia kuwaajiri Watanzania Elfu Kumi na Moja (11,000) wakati wa utekelezaji.
Naye, Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe.Mashimba Ndaki amesema idadi kubwa ya Wananchi wa eneo hilo wamelipwa kupisha mradi huo unapendelea kutekelezwa kwenye Jimbo lake, amesema wanaendelea kutoa ushirikiano sanjari na Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya kuendelea kushughulikia kero mbalimbali za Wananchi hao katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.
“Tunashukuru katika utekelezaji wa mradi huu, Vijana wengi wa maeneo ya Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Maswa na maeneo ya jirani, idadi kubwa ya vijana wamepata ajira kupitia mardi huu, pia malipo ya fidia kwa kiasi kikubwa yamefanyika na hakuna tena malalamiko kutoka kwa Wananchi”, ameeleza Mhe. Ndaki.Meneja Mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR -TRC Mhandisi Machibya Masanja akiwatambulisha wakandarasi wa mradi huo Kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakati alipowasili katika eneo la ujenzi kijiji Cha Malampaka Maswa mkoani Simiyu kipande Cha Isaka Mwanza wakati alipokagua mradi huo akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2020-2025 na uhai wa chama.
Meneja Mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR -TRC Mhandisi Machibya Masanja akiwatambulisha wakandarasi wa mradi huo Kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakati alipowasili katika eneo la ujenzi kijiji Cha Malampaka Maswa mkoani Simiyu kipande Cha Isaka Mwanza
Meneja Mradi wa Reli ya Kisasa ya Umeme SGR -TRC Mhandisi Machibya Masanja akitoa maelelzo ya mradi huo Kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo wakati alipowasili katika eneo la ujenzi kijiji Cha Malampaka Maswa mkoani Simiyu kipande Cha Isaka Mwanza.
Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mbunge wa Maswa Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Mashimba Ndaki wakati alipowasili katika eneo la mradi kwenye eneo la ujenzi Kijiji Cha Malampaka kushoto ni Mh. Stanslaus Nyongo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa madaraja madogo ya reli hiyo.
Muonekano wa tuta la kutandika reli ya kisasa ya SGR kipande Cha Isaka -Mwanza.
Muonekano wa tuta la kutandika reli ya kisasa ya SGR kipande Cha Isaka -Mwanza.
……………………………………
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...