Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka
amewasili mkoani Lindi ambapo pamoja na mambi mengine amepokea taarifa
ya utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetumia
mabilioni ya fedha yaliyotolewa na Seriakli ya Awamu ya Sita
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Shaka
amewasili katika Mkoa wa Lindi leo Mei 29 mwaka 2022 kwa ajili ya ziara
kikazi inayoambana na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama pamoja na
uhai wa Chama hicho.
Akizungumza
na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Mkoa wa Lindi Shaka amesema
amefurahishwa na mapokeozi ya kihistoria aliyoyapata kwenye mkoa huo na
atahakikisha analipa deni hilo kwa kuendeelea kuwapigania.
“Niwahakikishie
ndugu wananchi Serikali hii inayoongozwa na Rais wetu Samia Suluhu
Hassan haitawaacha kinyonge na itaendelea kutoa mabilioni ya fedha kwa
ajli ya miradi ya maendeleo,”amesema Shaka na kusisitiza Serikali ya
Awamu ya Sita imetoa Sh.bilioni 52 za maendeleo kwenye mkoa huu.
Akizungumzia
taarifa ambazo amepokea kutoka kwa viongozi wa Mkoa wa Lindi Shaka
amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.“Nawapongeza
kwa kazi nzuri ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo imefanyika
katika mkoa huu.”
Kuhusu
kero ambazo zimetolewa na wananchi wa Mkoa wa Lindi, Shaka amesema
amefarijika kuona wnanchi wakitoa kero na kisha kupatiwa ufumbuzi ambazo
zimekuwa zikiwatatiza na kupata majibu na yale yanayohitaji muda
yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.
Ametumia
nafasi hiyo kuwahakikihsia wananchi kwamba Seriakli ya Rais Samia
itaendelea kuwatumikia katika kuleta maendeleo. “Bilioni 52zimeletwa
katika Mkoa wa Lindi kwa ajili ya maendeleo na kuja kwa fedha nyingi
kiasi hiki haijawahi kutokea huko nyuma, ni Serikali ya Rais Samia
imeleta fedha hii.
“Lindi
ya leo hii ni tofauti na ile ya zamani, maendeleo yapo na mageuzi
yamefanyika, wananchi wamekiri ndani ya mwaka mmoja Rais Samia Suluhu
Hassan amefanya mambo makubwa.Niwaombe msiwe wanyonge, Serikali ipo na
Rais wetu yupo.Yale ambayo yanaonekana kama changamoto yafanyiwe
kazi,”amesema Shaka.
Kwa
upande wake Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Hamida Sharifu ametumia
nafasi hiyo kutoa shukrani za wananchi wa Mkoa huo kwa Raisa Samia
Suluhu Hassana kwani katika kipindi cha mwaka mmoja ametoa fedha nyingi
za maendeleo.
“Tumepokea
fedha nyingi za maendeleo kwa ajili ya Lindi, kila eneo leo hii ujenzi
unaendelea.Katika elimu kwa mapenzi makubwa ya Rais wetu Samia tumepokea
Sh.bilioni 3.5 ambazo zimetumika kwenye miradi mbalimbali ya elimu
kwenye sekta hiyo.Tumepokea Sh.bilioni 4.5 kwa ajili ya sekta ya afya,
tumepokea Sh.milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya
Lindi.
“Rais
anaupendo mkubwa kwetu na katika kila sekta kuna fedha tumepokea.
Tumepokea milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa zanati.Tunajenga hospitali
ya Mkoa wa Lindi na Sh.bilioni nne zimetua tayari.
“Kwenye
sekta ya maji nako tumepokea fedha , tumepokea Sh.bilioni nane na mwaka
huu tumepokea Sh.bilioni 3.5 kwenye sekta hiyo hiyo ya maji,”amesema na
kufafanua kwa ujumla wamepokea Sh.bilioni 52 kwa ajili ya maendeleo na
fedha hizo zote ni katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa Rais Samia.
Awali
akipokea taarifa ya CCM Mkoa wa Lindi, Shaka ameelezwa ambavyo uhai wa
Chama umeimarika kwa kiasi kikubwa na kuhusu mchakato wa uchaguzi wa
ndani ya Chama hicho umekwenda vizuri na hadi sasa hakuna dosari ya aina
yoyote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...