Na Mwandishi Wetu

WANAWAKE nchini Tanzania ambao wanaishi kwenye jamii zenye uhifadhi simamizi shirikishi wa misitu wameonesha mabadiliko makubwa katika ushiriki wa usimamizi na utumiaji wa rasilimali misitu.

Kauli hiyo imetolewa na Saimon Lugazo ambaye ni Ofisa Muhamasishaji kutoka shirika la kuhifadhi misitu ya asili nchini Tanzania (TFCG) wakati wa warsha ya asasi mbalimba zinazojishughulisha na rasilimali misitu ambazo ni mwanachama wa chama Cha wafanyakazi za misitu (TFWG).

Lugazo amesema kuwa ingawa bado hakujakuwa na idadi ya sawa kwa sawa na wanaume lakini wanawake wameamka ikiwemo kwenye suala la umiliki wa ardhi,kufanya biashara za misitu na kushiriki katika vikundi vya hisa.

Kwa upande wake Dokta Mroto ambaye amehusika na utafiti amesema kuwa wapo wanawake ambao kwa sasa wameanza kujishughulisha na ukataji mkaa na kuwaweza kufungua miradi mbalimbali huku akishauri pia vijana nao wanahamasishwa vya kutosha kushiriki katika mradi.

Nao baadhi ya washiriki wa warsha hiyo akiwemo Marygoreth Lwekiza kutoka MCDI ,Fadhila Kateta kutoka Jumuiko la maliasili Tanzania na Isaya Sekibo kutoka Suredo wamesema kuwa miongoni mwa shughuli kubwa wanazozifanya ni kuhakikisha wanawake wanashirikishwa na wanashiriki vya kutoka katika shughuli za misitu.

Warsha hiyo ambayo imehusisha wanachama TFWG imewezeshwa na mradi wa kuhifadhi misitu kupitia biashara endelevu ya mazao ya misitu(CoFoReST ) unaoendeshwa na TFCG wakishirikiana na MJUMITA kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo na ushirikiano la Uswizi (SDC).

Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa asasi mbalimbali zilipokutana kujadili masuala mbalimbali yanayohusu rasilimali za misitu



Washiriki wa warsha hiyo wakiwa makini kufuatilia mada mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...