Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi nchini limejipanga kuhakikisha kuwa hakuna mhalifu anayetamba hapa nchini na wanaofanya uhalifu wataendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria kwakushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL).

DCI Wambura ameyasema hayo Mei 13,2022 jijini Dodoma wakati wa ufungaji wa mafunzo ya mradi wa INTERPOL EAST AFRICA COMMUNITY (I-EAC) kwa Watendaji wa Taasisi mbalimbali  watakaohusika na mradi huo ambao lengo lake ni kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka.

Kwa upande wake Mshiriki wa Mafunzo hayo kutoka Wakala wa Usajili ufilisi na udhamini (RITA) ROBBY OTAIGO amesema mafunzo hayo yatawajenga kushirikiana na INTERPOL katika kupambana na uhalifu huku Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka Kenya Bi. ALLEN BAMBAZI akisema wanatarajia kuongeza muda wa mafunzo hayo ili kuwafikia watu wengi zaidi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...