Na Mashaka Mhando,Tanga
MAMLAKA ya Bandari nchini (TPA) imesema kiwango cha shilingi Bilioni 500 zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa mara moja, kwa ajili ya kununulia vifaa vya kuhudumia mizigo ili kuongeza ufanisi katika bandari ya Dar es salaam.
Akizungumza jana katika mkutano wa wadau wa bandari unaofanyika mjini hapa, Mkurugenzi Mkuu wa TPA nchini Erick Hamissi alisema uwekezaji unaokwenda kufanyika katika bandari hiyo ni mkubwa ambao utafungua fursa kwa nchi za maziwa makuu kwa matumizi ya bandari hiyo.
Alisema kuwa kuna mradi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwara ambapo watapeleka mizigo ya nje katika nchi za Maziwa makuu (Transit) baada ya serikali kuwekeza fedha hizo ambapo pia zitatumika kununulia vifaa ili kuwezesha ufanisi huo.
“Tutakuwa na ujenzi wa bandari ya nchi kavu ya kwara, isitoshe serikali ya awamu ya sita imewekeza kiasi cha shilingi Bilioni 500 kwa mara moja uwekezaji ambao hauajwahi kufanyika kwa mara moja hii inaonesha mhe Rais amedhamiria kuifanya bandari yetu ifanye kazi kwa ufanisi,” alisema Hamissi.
Alisema uwekezaji unaofanyika kwasasa katika miundombinu ya reli, Bandari na kwenye maziwa inaoensha kwamba nchi zote zinazotuzunguka hazitakuwa na chaguo lingine bali kutumia bandari ya Dar es salaam karibu watu milioni 700 za nchi hizo.
Mkurugenzi huyo alisema mkutano unaofanyika mjini Tanga kuwakutanisha wadau wa bandari haujawahi kufanyika hivyo utatoa fursa kwa wadau kujadili vikwazo na fursa zilizopo katika kuongeza ufanisi zaidi ya bandari zilizopo hapa nchini.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Wakala wa meli nchini (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge, ambao ndiyo walioratibu mkutano huo alisema kwamba wadau wamekutanishwa pamoja ili kutazama changamoto wanazokutana nazo kasha waweze kuzipatia majawabu ya mapendekezo ya kuyafanyia kazi kwa pamoja.
“Warsha hii itatazama changamoto mbalimbali ambazo zinaipata bandari ya dare s salaam na furasa zilizopo na kutoa mapendekezo ya kuboresha ikiwemo bandari ya Tanga,” alisema .
Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa, alisema mkutano huo wa wadau utasaidia kuongeza fursa za usafirishaji mizigo utakaofanywa na shirika hilo ambalo limefanya ukarabati wa reli yake ili kuweza kuhudumai nchi za maziwa makuu.
Naye Mtendaji Mkuu wa Wasafirishaji nchini (TAT), Ashraf Khan alisema wao kama wasafirishaji wanaiomba bandari iwasaidie maroli yao yanayobeba mizigo bandarini yaweze kutoka kwa wepesi ili meli zinazoingia bandarini zichukue muda mfupi kukaa bandarini.
Awali akifungua warsa hiyo ya siku mbili Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima, aliwataka wajumbe wa mkutano huo ikiwemo uongozi wa Bandari kutazama changamoto hizo na kuzipatia majawabu ili bandari ya Dar es salaam iweze kushindana na bandari nyingine zilzopo katika ukanda huu.
Alisema wanapofikiria kuondoa changamoto katika bandari ya Dar es salaam wafuate maelekezo yanayotolewa na rais ili waweze kuongeza tija lakini pia kushindana na bandari za Beira nchini Msumbiji pamoja na ile ya Mombasa nchini Kenya.
“Kuweni mfano wa kile ambacho Rais wetu anachohubiri kuitaka bandari ifanye kazi kwa ufanisi, tusiwe watu wa kuiangusha bandari tufanye ifanye vizuri kushindana na bandari nyingine zinazotuzunguka," alisema Mkuu huyuo wa Mkoa
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) Erick Hamissi
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa
Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Wasafirishaji nchini (TAT) Ashraf Khan
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Meli nchini (TASAC) Kaimu Abdi Mkeyenge
Wadau wakisikiliza kwa makini kikao kilichopo malizika mjini hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...