Na Pamela Mollel,Mererani

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Semamba  amesema kuwa usalama,utunzaji wa mazingira na usimamizi wa baruti kwa wachimbaji wa madini katika migodi ni jambo muhimu kwa serikali hivyo ni vyema wakazingatia sheria zilizopo ili kuepuka majanga mbalimbali

Amesema hayo wakati akifungua mafunzo maalumu kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite,Mameneja wa migodi na wasimamizi wa baruti yaliyofanyika Wilayani  Simanjiro  Mkoani Manyara

"Siku za hivi karibu kumekuwepo na matukio makubwa katika maeneo ya migodi na hii pia husababishwa na matumizi mabaya ya baruti,mafunzo haya ya leo mtajifunza sheria za madini,usimamizi wa baruti,uchimbaji salama pamoja na utunzaji wa mazingira "alisema Mhandisi Samamba

Aidha aliwataka wachimbaji hao kushiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi jambo ambalo litaiwezesha serikalk kupata idadi sahihi ya wachimbaji wa madini,aina ya madini wanayochimba na mahitaji ya msingi ya uchimbaji wa madini yakiwemo ya usimamizi wa usalama pamoja utunzaji wa mazingira  migodini

Kwa upande wao wadau wa madini katika migodi ya Mirerani  wameeleza umuhimu wa uchimbaji madini kuwekewa mipango bora ikiwemo ya udhibiti wa utoroshaji wa madini,ulipaji wa kodi na  usalama hasa suala la kuwa na walipuaji wa baruti katika migodi wenye sifa

Naye Mkuu wa wilaya ya Simanjiro  Dkt Suleiman Serera ameeleza kuwa serikalk tayari imeshatoa fedha za kuanza ujenzi wa Kituo jumuishi cha biashara ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani zaidi ya shilingi bilioni tano

"Nawapongeza sanaa Tume ya madini kwa kufanya mafunzo haya naamini yataleta manufaa makubwa kwao na jamii kwa ujumla"alisema Dkt Serera.

Katibu mtendaji wa tume ya madini mhandisi Yahya Samamba akiongea katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wachimbaji wa madini
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt Suleimani  Serera


Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Dkt Suleimani Serera akiteta jambo na katibu mtendaji Tume ya madini Mhandisi Yahya Samamba
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...