Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WADAU wanaohusika na masuala ya Ubunifu wamekutana Dar es Salaam kupitia Kongamano la Ubunifu ambalo limeratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH).

kongamano hilo limefanyika leo Mei 10,2022 jijini Dar es Salaam na wadau hao wamepata nafasi ya kujadili kwa kina masuala yanayohusu ubunifu na hatua wanazochukua kuendeleza sekta ya ubunifu ili kuwa na tija kwa Watanzania.

Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Mipango katika Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Alfred Mkombo akizungumza mbele ya wabunifu na wadau hao amesema kazi yao ni kusimamia masoko ya mitaji ili biashara zinazohitaji mitaji zinapata kupitia utaratibu uliopo.

“Leo tumekuwa ili kuangalia ubunifu katika maeneo ya biashara zinazoanza na zile biashara za kati kwamba namna gani hizi biashara zinapata mitaji kupitia masoko ya mitaji.

“Sisi kama Mamlaka ya Masoko na mitaji tunasaidia ubunifu katika masoko ya mitaji.Mojawapo ya jukumu letu ni kuendeleza masoko ya mitaji na ili kuendeleza lazima usimamie ubunifu, biashara ya ubunifu na ubunifu katika bidhaa na huduma zinazohitajika kwa wananchi.

“Kwa hiyo sisi tunawachagiza wananchi hasa vijana wawe wabunifu zaidi.Hivi tuna mpango tunaoufanya kwa ushirikiano na UNDP katika kutengeneza miongozo ya kusimamia mipango ya mitaji shirikishi.Tunaposema mitaji shirikishi ni utaratibu wa kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza mradi fulani unapata fedha,”amesema.

Amefafanua mtu anachanga fedha kidogo kidogo kama inavyofanyika msibani au kwenye makanisa lakini ile fedha sasa wanaichukua na wanaipeleka kwenye uzalishaji.

“Ukusanyaji huu unakuwa tofauti kidoogo kwasababu unakusanywa kupitia mitandao au majukwaa ya mitatandao ya kieletroniki na hii mitandao ni lazima iwe imesajiliwa , kwa hiyo tunafanya huo mpango , tunaandaa miongozo kwa ajili ya uendeshaji.”

Kwa upande wake Ofisa kutoka COSTECH Promise Mwakale amesema wamekuwa wakitoa ruzuku kwa ajili ya wabunifu na wanatoa ruzuku kuanzia kwenye mawazo na kuwakuza.“Kwa hiyo Kongamano hili ni muhimu kwetu kwani limejumuisha wadau wengine katika kufungua masoko na kuongeza mitaji kwa ajili ya wabunifu”amesema Mwakale.

Aidha Mtalaamu wa Fedha kutoka UNCDF Paul Damocha amesema wao mbali ya kuwa moja ya wadhamini wa Wiki ya Ubunifu kwa nyakati tofauti wamekuwa wakishiriki katika kukuza na kuendeleza ubunifu kwa njia tofauti kwa kushirikiana na Serikali, COSETCH na wadau wengine.

Ameongeza wamekuwa wakisaisia katika sekta ya fedha, sera na kutengeneza miongozo pamoja na kuelekeza idara za Serikali katika kutengeneza mazingira wezeshi kwa wabunifu na kuwapatia leseni.

“Kumekuwa na jitihada kubwa za kitalaam za kusaidia wajasiriamali kuanzisha biashara zao, mambo ya teknolojia na biashara.Kuhusu ubunifu tunaona haja ya kushirikisha washika dau wengi yakiwemo mashirikia makubwa.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Phema Agri Daniela Kwayu amesema wao wamejikita katika kutumia teknolojia mbalimbali kuwasaidia wakulima pamoja na kuwawezesha katika pembejeo.

Kuhusu ushiriki wao kwenye Kongamano la Ubunifu amesema wao ni miongoni mwa kampuni ambazo zimepata msaada mkubwa kutoka CMSA, hivyo wameshiriki ili kutoa shuhuda jinsi walivyofanikiwa na kusaidia wakulima wengi nchini.

Kwa kukumbusha tu Wiki ya Ubunifu Tanzania kilele chake kitafanyika jijini Dodoma Mei 16-20 mwaka huu na Wiki hiyo inaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikishirikiana na COSTECH na UNDP kupitia Programu yake ya Ubunifu –Funguo na mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu ya Vodacom- Tanzania.

Sehemu ya wadau wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa kipindi cha kwanza cha Kongamano maalum la majadiliano kuhusu sekta ya ubunifu na wabunifu.Kongamano hilo limefanyika leo Mei 10, 2022 jijini Dar es Salaam na limeandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, kwa kushirkiana na COSTECH pamoja na UNDP kupitia Programu yake ya Ubunifu –Funguo na mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu ya Voda-Tanzania.

Sosthenes Kewe kutoka FSDT (wa pili kushoto) akifafanua jambo wakati wa kongamano hilo ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya ubunifu na wabunifu.Wengine katika picha hiyo ni viongozi wa taasisi , kampuni na mashirika mbalimbali wakisikiliza majadiliano kabla ya kutoa maoni yao kuhusu sekta hiyo.
Sehemu ya washiriki wakiwa makini kufuatilia mijadala , maoni na michango kuhusu bunifu na wabunifu nchini hasa katika kuangalia mbinu mbalimbali ambazo zitasaidia kuendeleza wabunifu na kada nyingine za aina hiyo

Mkurugenzi Mkuu Kampuni ya Phema Agri Daniela Kwayu(katikati) akitoa mchango kuhusu ambavyo wamekuwa wakisaidia wakulima katika masuala mbalimbali yanayohusu kilimo na teknolojia.

Washiriki wa kongamano la Ubunifu wakiwa katika kongamano hilo.

Sosthenes Kewe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu kutoka Captain of Industry and Former( FSDT) aliyekaa katikati akisisitiza jambo kuhusu namna ambavyo wanashiriki katika kuendeleza masuala ya ubunifu nchini kwa kushirikiana na wadau wengine mbalimbali.

Meneja Mratibu wa Miradi kutoka Funguo Joseph E.M akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo ameeleza kwa kina kuhusu ushiriki wao katika kuendeleza sekta ya ubunifu.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakiwa wamenyoosha mikono kama ishara ya kufurahia jambo baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya majadiliano kuhusu ubunifu.


Mmoja ya washereheshaji katika kongamano la wabunifu akitoa akizungumza wakati akielezea umuhimu wa kongamano hilo ambalo linakwenda sambamba na wiki ya Ubinifu ambayo kilele chake kitafanyika jijini Dodoma kuanzia Mei 16-20 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...