Dar es Salaam
Taasisi
ya 'Dkt.Reginald Mengi Foundation' (DRMF) kwa kushirikiana na Marafiki
wa Dkt. Mengi wameandaa hafla maalumu itakayowakutanisha zaidi ya watu
wenye ulemavu 1000 itakayo hudhuriwa na viongozi wa serikali, mashirika
binafsi na mabalozi mbalimbali.
Akizungumzia
kuhusu hafla hiyo mbele ya waandishi wa habari Dar es
Salaam,Mkurugenzi wa Taasisi ya 'Dkt .Reginald Mengi Foundation
Shimimana Ntuyabaliwe alisema mgeni rasmi katika tukio hilo anatarajiwa
kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Ajira,Vijana na Watu
wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako.
Alisema
hafla hiyo itakayohusisha matukio mbalimbali ikiwemo michezo, burudani,
upimaji wa afya na kutoa shuhuda kuhusu Marehemu Dk Mengi inatarajiwa
kufanyika Mei 29 katika Viwanja vya 'Jakaya Kikwete Youth Park' katikati
ya Jiji la Dar es Salaam.
Alizitaja
baadhi ya huduma za upimaji afya zitakazotolewa siku ya hafla hiyo kuwa
ni pamoja na upimaji wa macho, kiwango cha sukari mwilini, tezi dume
pamoja na kutoa ushauri wa kitabibu kwa wale watakaokuwa na changamoto
mbalimbali.
"Pamoja na
matukio hayo vilevile washiriki na wageni wote watapata fursa ya kula
pamoja chakula cha mchana ikiwa ni ishara ya chakula alichokuwa
akikiandaa Dk Mengi na kula na watu wenye ulemavu wapatao 5000 kila
Mwaka kwa miongo mitatu" alisema Ntuyabaliwe
Alisema
shughuli hiyo ni mahususi Kwa ajili ya kumbukizi ya moyo wake wa
kujitolea na kujenga kizazi cha watanzania ambao watakumbuka na
kujifunza historia yake na kujenga tabasamu kwa watanzania wenzao kitu
ambacho marehemu Dk Mengi alikuwa akikifanya .
Alisema
katika kipindi cha uhai wake Dk Mengi alijitolea na kufanya mambo
mengi katika jamii ya watanzania Kwa kugusa maisha ya watu hususani watu
wenye ulemavu na kuwapa matumaini wenzake ambao wengi walinufahika na
uwepo wake.
"Kwa muktadha
huu tunawasii watanzania wote kuendeleza mshumaa wa matumaini kwa
kujenga moyo wa kujitolea kwa jamii kwani wahenga wana Usemi usemao
kutoa ni moyo na siyo utajiri hivyo tunawahamasisha watanzania wote kwa
umoja wao kujitolea kwa watu waliopo katika jamii zao" aliongeza
Ntuyabaliwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...