NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema Serikali imejipanga kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu hapa nchi kuanzia Shule ya Msingi ikiwemo kuwaandaa wanafunzi kujifunza kwa vitendo masomo ya michepua ya Sayansi kimu na kilimoili waweze kupata ujuzi wa kukidhi matakwa ya ajira ikiwemo kwenye sekta ya Utalii hapa nchini.

Waziri Profesa Mkenda ameyasema hayo mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo maalumu kwa walimu 322 wa masomo ya Mchepuo wa kilimo na Sayansi kimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wameshaweka mikakati ya kuwaandaa Walimu kwa kuwapa mafunzo ndani na nje ya nchi ili kuwafundisha wanafunzi.

Aidha alisema tayari Wizara hiyo imeanza kutoa kipaumbele kwa mafunzo ya walimu wa masomo hayo hapa nchini kwa kuwaongezea ujuzi na maarifa ya kwenda kuwafundisha wanafunzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Lengo la mafunzo hayo ni kuandaa vijana ambao wataweza kuongeza ajira katika sekta ya kilimo na utalii ambao tayari umeshatangazwa nje ya nchi na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya Utalii ya “ The RoyarTour.

Kwa Upande wake wa Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET),Dk Aneth Komba,alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kitalaamu walimu wa masomo ya Sayansi kimu na Kilimo kwa kuwapa mbinu za ufundishaji, ujifunzaji na upimaji unaozingatia ujenzi wa umahiri .

Dk Komba alisema kuwa matokeo ya mafunzo hayo yataweza kumuwezesha muhitimu wa masomo hayo kupata maarifa ,stadi za kutenda uelekeo wa kujitegemea kwa manufaa mapana ya jamii na Taifa kwa ujumla .

Alisema mafunzo ni ya kundi la tatu la walimu 322 ambao wanatoka katika shule za Serikali na Binafsi ili kuwajengea uwezo mkubwa wanafunzi ambao wataingia katika soko la ajira.

Naye Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi,Hadija Mcheka,alisema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati kutokana na kuwepo kwa upungufu mkubwa wa walimu wa masomo hayo na kwamba wataendelea kushirikiana na wizara ya elimu kusaidia kuongeza idadi ya walimu.

Mafunzo hayo ya siku tano yametolewa kwa waliu 332 kutoka shule za Serikali na binafsi upande wa Tanzania bara na visiwani wanaofundisha masomo ya kilimo na Sayansi kimu. 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akifungua mafunzo maalumu kwa walimu 322 wa masomo ya Mchepuo wa kilimo na Sayansi kimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar mkoani Morogoro
Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania(TET),Dk Aneth Komba akizungumza  wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa walimu 322 wa masomo ya Mchepuo wa kilimo na Sayansi kimu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar mkoani Morogoro .Dkt Komba alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni ya kuwajengea uwezo wa kitalaamu walimu wa masomo ya Sayansi kimu na Kilimo kwa kuwapa mbinu za ufundishaji, ujifunzaji na upimaji unaozingatia ujenzi wa umahiri . Mafunzo hayo yalifunguliwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...