*WaziriBashungwa:miundumbinu imeshaandaliwa kwa wanafunzi hao

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

 WANAFUNZI 153,219 wakiwemo wasichana 67,541 na wavulana 85,678 sawa na asilimia 91.8 ya wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na shule za Sekondari Kidato cha Tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2022.

Wanafunzi 90,825 wakiwemo wasichana 43,104 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shu shule za Serikali zilizoanza mwaka 2022 huku kukiwa na ongezeko la shule 22 za Sekondari mpya.

Ameyasema hayo leo Mei 12, 2022 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),  Innocent Bashungwa wakati akitangaza Matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ualimu na vyuo vya elimu za ufundi Jijini Dar es salaam.

Amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wapo wanafunzi wenye mahitaji maalum 481, ambao kati yao wasichana ni 204.

"Kati ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano, wanafunzi 41,401 wakiwemo wasichana 17,390 watajiunga kusoma tahasusi za Sayansi na Hisabati na wanafunzi 49,133 wakiwemo wasichana 25,508 watajiunga kusoma tahasusi za masomo ya Sanaa,Lugha na Biashara". Amesema Waziri Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa amesema kwa kuangalia takwimu za mwaka 2022, kumekuwa na ongezeko la wasichana 7,555 waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi, ukilinganisha na mwaka 2021 hata hivyo idadi hii bado ni ndogo kulinganisha na wavulana.

"Ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara inaendelea kuboresha miundombinu ya shule ili kuhakikisha wasichana wengi zaidi wanajiunga na Kidato cha Tano". Amesema Waziri Bashungwa.

Pamoja na hayo Waziri Bashungwa amesema jumla ya wanafunzi 14,254 wakiwemo wasichana 3,901 na wavulana 10,353 wamekosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha tano na Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi mwaka 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za  Serikali Mikoa na  Tawala za Serikali za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa akuzungumza na waandishi habari kuhusiana na wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha tano jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za  Serikali Mikoa na  Tawala za Serikali za Mitaa (Tamisemi) Innocent Bashungwa akuzungumza na waandishi habari kuhusiana na wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha tano jijini Dar es Salaam.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...