Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wetu Mama Samia ameupiga mwingi!Ndivyo anavyoeleza muigizaji maarufu wa filamu nchini Lucas Lazaro Mhuvile maarufu kwa jina la Joti wakati anaelezea filamu ya Royal Tour ambapo amesema filamu hiyo inakwenda kuwaambia watu huko Duniani Tanzania kuna nini.
Jot ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na staili yake ya uigizaji alikuwa ni miongoni mwa wasanii walioshiriki katika uzinduzi wa filamu hiyo uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam ambapo amesema katika filamu hiyo ni wazi utalii wa Tanzania unakwenda kutambulika katika ramani ya dunia.
Kuhusu baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiibeza filamu ya Royal Tour, Joti amesema Rais Samia amefanya jambo kubwa na nzuri na wala asivunjike moyo kwani hata manabii pamoja na nia njema walizokuwa nazo bado walikataliwa.
“Nimwambie mama yetu hana sababu ya kuvunjika moyo, na Watanzania tunaendelea kumtia moyo .Ni jukumu letu kumsapoti na kumpa nguvu, yeye ni rais wa kike lakini ameamua kuja tofauti na marais wengine waliotangalia.
“Amekuja na ubunifu wa Royal Tour inamaana watu huko duniani wanajua Tanzania kuna nini.Kwa hiyo hao wanaobeza wanaweza wasiione faida sasa lakini ukweli utabaki kuwa mama ameupiga mwingi”.
Amesisitiza Royal Tour inakwenda kutangaza utalii lakini kutangaza sanaa ya Tanzania kwenye mataifa mengine.”Wasanii tumejipanga na ndio maana tuko kwenye uzinduzi huu , hapa hapa tunapata na Conection na niko tayari kwenye part ya Royal Tour na mimi niwepo nicheze na Simba.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...