Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Karibu Tanzania Organization (KTO,) Maggid Mjengwa wakiwa katika picha ya pamoja na wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe mkoani Pwani mara baada ya kukabidhi msaada wa taulo za kike.


Na Mwandishi Maalum, Kisarawe.

WANAWAKE Vijana waliokatisha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujauzito na hali duni ya maisha, wameshauriwa kutumia vyema fursa iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia waliokatishwa masomo kurudi shuleni na kuendelea na masomo hayo. Ni kwa kupitia mfumo rasmi au mbadala.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa  Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) kupitia  Bi. Fatma Mwassa wakati wakikabidhi msaada wa taulo za kike kwa wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe, Pwani.

Bi. Mwassa amesema, katika kuhakikisha wanawake hao vijana waliokatisha masomo wanatumia fursa iliyotolewa na Rais Samia, Taasisi anayoiongoza wameshirikiana na taasisi ya Karibu Tanzania Organization  (KTO) kupitia programu ya 'Elimu Haina Mwisho' ili kuwasaidia wanawake hao vijana katika kutimiza ndoto zao zilizokatishwa awali.

 " Mabinti tumieni fursa hii iliyotolewa na Mh. Rais. Sisi tupo hapa kuwasaidia ili ndoto na malengo yenu yafikiwe. Zingatieni masomo ya maarifa, ujuzi na mafunzo ya ufundi mnayopewa kwa kuwa  ni fursa ya ajira mkononi baada ya kuhitimu masomo yenu." Amesema

Aidha amewataka  mabinti hao kutumia  changamoto zao kama fursa katika kutengeneza maisha yao kama Rais Samia alivyowapa kipaumbele na kuwataka kutunza mtaji wa mafunzo ya ufundi katika kutengeneza ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao.

Taasisi ya KTO inaratibu programu ya 'Elimu Haina Mwisho'  kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Ni kwa kupitia Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi 54 vinavyoendesha programu hiyo yenye kutoa maarifa na ujuzi kwenye masomo ya Sekondari, Ufundi, Stadi za Maisha na Ujasiriamali.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation ( MIF), Bi. Fatma Mwasa, akiwa Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Kilwa Masoko hapo jana ( Jumatano), alikabidhi msaada wa mahitaji muhimu ikiwamo sabuni, shuka na madaftari, kwa wanachuo wapya 18 kutoka Zanzibar wanaosoma chuoni hapo. Vyote hivyo ukichanganya na vilivyokabidhiwa Kisarawe, vina thamani ya Shilingi Milioni Kumi na Moja.


Baadhi ya wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa MIF mara baadaya ya kukabidhiwa msaada wa taulo za kike.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) Bi. Fatma Mwassa akiwakabidhi taulo za kike baadhi ya wanachuo wa Chuo  cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe, Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) Bi. Fatma Mwassa akiwakabidhi taulo za kike baadhi ya wanachuo wa Chuo  cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe, Pwani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF,) Bi. Fatma Mwassa akiwakabidhi taulo za kike baadhi ya wanachuo wa Chuo  cha Maendeleo ya Wananchi Kisarawe, Pwani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...