TAASISI ya wanawake 100,000. Nchini Tanzania yampa kongole Rais wa Jamhuri Samia Suluhu Hassan kwa kuruka viunzi vitatu ikiwemo changamoto ya mishahara kwa watumishi, kupaa kwa bei ya mafuta dunian na ubunifu kwenye kutangaza utalii.


Taasisi hiyo yenye kujinasibu kwenye utetezi wa haki kwa wanawake yenye wanachama zaidi ya 100,000 nchi nzima kupitia vyombo vya habari leo tarehe 20 Mei 2022 jijini Dar es Salaam, wameamua kuvunja ukimya na kueleza kuwa utendaji wa rais  Samia unawafaharisha na kuchagiza dunia kuendelea kuwaamini wanawake kwenye kushika hatam. 

Vicky Kamata Mwenyekiti wa Taasisi hiyo amesema kuwa Rais Samia amechukua hataua za haraka kuwaongezea watumishi nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 jambo ambalo limewapa watendaji hao ari ya kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
"Kwa miaka mingi sasa, wafanyakazi nchini wamekuwa na kilio cha kutoongezwa mshahara na kutopandishwa vyeo kwa watumishi wa umma" amesema Kamata.
Amesema kuwa suala hilo limekwenda sambamba na  ustawi w mifuko ya pensheni kwa kuwa ilikuwa na ukata  wa fedha uliotokana na malimbikizo makubwa ya michango ya penchent ya watumishi wa umma. 
"Ndani ya mwaka mmoja tu, Rais Samia ameweza kuongeza mshahara kwa 23.3%, amepandisha watumishi wa umma maharaja na kulipa malimbikizo ya mchango wa pensheni za watumishi wa umma"

Kuhusu Rais Samia kuokoa uongezeko la bei ya mafuta taasisi hiyo inasema kuwa ni hatau ya kizalendo nay a haraka na kwamba serikali kufanya hivyo imenusuru sekta zote za uzalishaji mali nchini.
"Badala ya kusubiri hatua za kikodi kwenye bajeti ijayo ya serikali ambayo utekelezaji wake utaanza Julai 1, 2022, Rais Samia ameagiza kuwa ahueni itafutwe mapema zaidi kwa kutoa maelekezo kwamba katika kipindi hiki kabla hatujafikia mwaka mpya wa fedha, Serikali ijibane na ijinyime na itolewe ruzuku ya shilingi bilioni mia'' amesema Kamata.

Kamata amesema kuwa hatua nyingine zinazochukuliwa na serikali ni pamoja na kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghala moja kupitia maghala ya TIPER ili kupunguza au kuondoa gharama za meli kusubiri au kuchukua muda mrefu katika upakuaji wa mafuta katika maghala mengi,
"Pia Kuiongezea uwezo TPDC kuagiza mafuta nje ya nchi na Kuimarisha utendaji na weledi wa taasisi za Serikali zinazoshughulika na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo EWURA na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja" ameongeza Kamata. 
Amesema kuwa wakati mataifa mbalimbali duniani yamekumbwa na tafrani kutokana na sakata la bei la mafuta, ikiwemo changamoto za foleni na vurugu katika vituo vya mafuta kutokana na uhaba wa mafuta, kumekua na utulivu mkubwa nchini Tanzania, bila uhaba wa mafuta nchini kutokana na hatua za dharura za kijasiri za serikali chini ya uongozi i wa Rais Samia. 

Wakati huo huo Taasisi hiyo imeitazama Filamu ya 'The Tanzania Royal Tour' kuwa ni fikra bunifu ya kuutangaza utalii kwenye hatua ya kimataifa.
Amesisitiza kuwa Royal tour ni sehemu ya kitovu cha utalii "Ni vyema kusisitiza kuwa Royal Tour siyo movie kama zile zinazotengenezwa Hollywood au Bollywood au Nollywood au Bongo movie. Royal Tour ni makala malumu inayotoa fursa ya kipekee na mahsusi ya kuitangaza Tanzania ulimwenguni kama kitovu cha utalii"
Amesema kuwa mafanikio ya filamu hayo yapo wazi na kwamba Tayari filamu hii imefanikiwa kuitangaza Tanzania kimataifa na itaendelea kufanya hivyo kwa miaka mingi ijayo kwani imewekwa pia inapatikana katika mitandao mikubwa duniani kama Amazon na Apple TV na itaoneshwa katika channeli 350 nchini Marekani.

Mwenyekiti wa Wanawake 100,000 Vicky Kamata akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya jambo lao



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...