Mkuu wa Wilaya ya Morogoro amewaagiza wawekezaji wote wanao fanya shughuli zao wilayani Morogoro kufuwata sheria za mazingira ili kuepuka athari zinazo weza kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanyika katika Wilaya ya Morogoro ukihusishwa na shughuli za kibinadamu Mkuu wa Wilaya hiyo amewaagiza wawekezaji wote kufuata sheria za mazigira pamoja na kuwa na mikakati ya upandaji miti katika wilaya hiyo ili kuepuka athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Wakili Albert Msando ametoa kauli hiyo alipofika kukagua na kufanya uzinduzi wa kiwanda cha RAHA BEVERAGES katika Manispaa ya Morogoro ambapo amesisitiza wawekezaji wanapaswa kuwa mstari wa mbele kufuata sheria za mazingira pamoja na kupanda miti haswa kwenye maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Beatha Anthony alisema tayari kiwanda hicho kimechukua hatua mbalimbali za utunzaji wa mazingira pamoja na kueleza walivyoweza kutoa fursa za ajira kwa muda mfupi kwa wakazi wa Manispaa hiyo.

Aidha alisema mbali na kutoa ajira kwa wafanyabiashara na wakulima kupitia soko la ndizi tayari wameweza kuajiri vijana zaidi ya 40 huku mikakakti yao ikiwa ni kupita idadi hiyo ambapo Mwenyekiti na mwanzilishi wa kiwanda hicho Adolf Olomi akawasisitiza wakazi wa Morogoro kuchangamkia fursa mbalimbali zinazo patikana katika kiwanda hicho.

Kufunguliwa kwa Kiwanda cha RAHA BEVERAGES itakuwa mwarobaini wa changamoto ya soko la ndizi wilayani Morogoro ambapo wakulima watapata soko la uhakika la kuuza ndizi katika kiwanda hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...