Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa
Watanzania wa sekta mbalimbali ikiwemo ya utalii kujitayarisha kupokea
watalii watakaokuja kutalii nchini.
Ametoa rai hiyo leo Mei
8,2022 wakati akizindua filamu ya Royol Tour katika Jiji la Dar es
Salaam ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzinduliwa rasmi nchini
Marekani, kisha jijini Arusha na baadae Zanzibar.
“Mategemeo
yangu baada ya filamu hii kuzinduliwa Tanzania inatakiwa kujitayarisha
kupokea wageni wengi, wageni watakuwa wa tofauti tofauti hizo hata
watakapokuja watakaa katika hoteli za tofauti.
“Hivyo nitoe rai
kwa sekta za utalii kujitayarisha ili watalii wakija wakute hoteli
zipo, wakute watu wa kupokea wageni wapo, wapokea wageni viwanja vya
ndege nao wajiandea.
“Zile sifa ambazo zimeoneshwa kwenye filamu
lazima uonekane, tunapaswa kujitayarisha, watu wa sekta ya utalii na
sekta nyingine tujitayarishe, narudia tena lazima Watanzania wote
tujitayarishe,amesema Rais Samia.
Aidha amesema kuzinduliwa kwa
Filamu ya Royol Tour ni mwanzo tu wa kuzindua filamu nyingine za Royal
Tour awamu ya pili na ya tatu kwani kuna picha nyingi ambazo
zilichukuliwa ambazo zitatumika kutengeza filamu nyingine kwa lengo la
kendelea kutangaza utalii wa Tanzania.
“Filamu hii ya Royal Tour
ni mwanzo tu kwani nyingine zitakuja.Nimpongeze Rais wa Zanzibar
Dk.Hussein Mwinyi kwa ushiriki wake mzuri kwenye filamu hii na amekuwa
na msemo wake kuwa yajayo yanafurahisha, hivyo tuseme yajayo
yanafurahisha”amesema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati uzinduzi wa Filamu ya Tanzania'The Royal Tour' ambapo hafla ya Uzinduzi wa Filamu hiyo unafanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam leo Mei 8, 2022.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari wamewasili katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere tayari kwa ajili ya Uzinduzi wa Tanzania The Royal Tour ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...