Na.Khadija Seif, Michuzi TV
WAFANYABIASHARA
hususani wanaofanya Huduma katika sherehe wametakiwa kujiunga na Benki
Ili waweze kukopesheka kusaidia kukuza Biashara zao pamoja na kutunza
akiba.
Akizungumza jijini
Dar es salaam wakati akifungua Maonyesho ya Biashara ya wahudumu
katika Sherehe (Adorable wedding trade fair) Msimu wa 5, Mkurugenzi wa
Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba amesema ni Muhimu Wafanyabiashara
kuweka akiba zao na kufunga akaunti za kibenki Ili kujiwekea umakini wa
biashara zao pale mteja anapotaka kutuma muamala kwa njia za kibenki
kuliko kutoa maelezo ya kutumiwa Fedha Kwa njia ya Mitandao ya simu.
Hata
hivyo Mwangalaba ametoa wito Kwa Wafanyabiashara hao kuendelea kukuza
Biashara zao na kutengeneza Mawasiliano wao Kwa wao kwani kufanya hivyo
ni kujenga Mahusiano mazuri kwenye fani hizo na kuboresha kazi zao .
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa My wedding solution ambae pia ni Mratibu wa
Maonyesho hayo Anna Rema amesema Maonyesho hayo yanaendelea kukuwa zaidi
Huku lengo lake likiwa ni kuandaa Maonyesho ya Afrika Mashariki .
Rema
amesema Maonyesho hayo yatachukua siku 3 na wanatarajia Mgeni rasmi wa
kufunga Maonyesho hayo Mei 15 ni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo
Mohamed Mchengerwa.
picha
ya pamoja kati ya washiriki wa Maonyesho ya Biashara ya wahudumu katika
Sherehe na Wafanyabiashara wengine pamoja na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa
Benki ya Maendeleo nchini Ibrahim Mwangalaba wakati akizundua rasmi
Msimu wa 5 wa Maonyesho hayo katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es
salaam.
Emmal
cakes ni Miongoni mwa Banda aliliotembelea Mgeni rasmi ambae ni
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba na kueleza jinsi
gani utengenezaji wao wa keki ni wakibunifu zaidi kutokana na
kutengeneza keki za Maumbo mfano wa Nyumba za kuishi za kifahari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...