WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameahidi kuunga mkono juhudi za kukuza timu ya wanawake katika mchezo wa gofu ili kuleta Ushindani Kimataifa.

Akizungumza hayo wakati wa kufunga shindano la wanawake la Lugalo Ladies Open 2022 lililomalizika Jana katika klabu ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania Lugalo Dar es salaam amesema yeye ni mmoja ya waliokua wachezaji wa mchezo wa gofu hivyo hatosita kuunga Mkono na kuhakikisha Mchezo huo unakua na muamko zaidi na hamasa kwa wachezaji chipukizi kutoka vilabu mbalimbali vya gofu.

Sherehe hizo za kufunga Shindano zilifanyika sambamba na Harambee Maalumu ya kukuza Mfuko wa gofu wanawake ambapo Dkt. Stergomena Tax alichangia shilingi Milioni 25.

Kwa upende wake Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo mstaafu amewapongeza wana kamati, wachezaji na wawakilishi kutoka Klabu mbalimbali kwa kufanikisha mashindano hayo.

Angel Eaton wa Lugalo ndiye mshindi katika shindano hilo kwa kupiga mikwaju 148 akifuatiwa na nahodha wa wanawake Hawa wanyeche wa Lugalo Mikwaju 161 na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Neema Ulomi wa Arusha Gymkhana mikwaju 163.

Upande wa Divisheni A mshindi ni Ayne Magombe aliyefungana na Chiku Elias kwa mikwaju ya jumla 166, Divisheni B mshindi wa kwanza ni Christina charles aliyechapa mikwaju jumla 148 na kumpindua Rehema Athumani aliyechukua nafasi ya pili kwa mikwaju ya jumla 153 huku Divisheni C mshindi ni Yvonne Ondari mikwaju ya Jumla 145 na kumtangulia Rachel Mushi aliyepata mikwaju ya jumla 148 huku mshindi wa Jumla kwa Net akiwa ni Loveness Franko wa Arusha Gymkhana aliyepiga mikwaju ya Jumla 140.

Aidha upande wa wachezaji wanaume waliosindikiza shindano hilo Mshindi ni Seif Mcharo akipiga mikwaju 148,

Divisheni A mshindi ni John Hiza kwa Mikwaju ya Jumla 151 akifuatiwa na Peter Fiwa mikwaju ya Jumla153, Divisheni B ikichukuliwa na Livingstone Christopher kwa Mikwaju ya Jumla 141 akimpiku Joseph Tairo aliyechapa mikwaju ya Jumla 145.

Hata hivyo, kumaliza kwa Shindano la wanawake (Lugalo Ladies Open) ni Maandalizi ya Shindano kubwa la wazi linalotaraji kufanyika Mei 28 na 29, 2022 Lugalo Dar es salaam.


 Mchezaji wa gofu Angel Eaton(katikati) akikabidhiwa kikombe na waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa JKT Dkt.Stergomena Lawrence Tax(kushoto) baada ya kutangazwa Mshindi kwenye Shindano la wanawake (Lugalo ladies open 2022) lililomalizika Jana mei 22 katika viwanja vya Lugalo gofu jijini Dar es salaam (kulia) Meneja wa Kampeni ya ndege ya Qatar nchini Tanzania Anil sreenivasan


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa JKT Dkt. Stergomena Lawrence Tax (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo gofu brigedia Michael Luwongo pamoja na washindi wa vipengele tofauti tofauti waliofanya vizuri kwenye Shindano la wanawake (Lugalo ladies open 2022) lililomalizika Jana mei 22 katika viwanja vya Lugalo gofu jijini Dar es salaam wakiwemo na wadhamini walioshiriki kutoka Makampuni mbalimbali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...