Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MENEJA Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa zawadi aliyoipata ya fedha taslimu, Shilingi Milioni 2 (Tsh. 2,000,000/-) kutoka Kampuni ya Emirate Aluminium Profile atagawana wenzake alioshirikiana nao katika kampeni ya kuhamasisha ushindi kwa timu hiyo ya Simba SC wakati ikijiandaa kucheza na Orlando Pirates FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, mwezi Aprili, 2022.

Akizungumza baada ya kukabidhishwa fedha hizo na zawadi ya Kikombe, Ahmed Ally amesema atatoa fedha kidogo katika kiasi hicho alichopewa kama zawadi na kuwapa wenzake wote ambao ameshirikiana nao katika kampeni ya hamasa wakati Simba SC inajiandaa kucheza na Klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

“Zawadi hii nitatoa kipande kidogo na kuwapa angalau wale wote ambao tulihangaika nao kwenye Malori, Matope, Mvua, Vipaza sauti vya Sumu ya Panya, Mende”, amesema Ahmed Ally.

Ahmed ameishukuru Kampuni hiyo ya Emirate kuonyesha thamani ya walichokifanya huku akitoa wito kwa wegine kuiga mfano wa Kampuni hiyo katika kutambua mchango wa watu mbalimbali katika mambo mbalimbali kama kwenye Soka kutoa hamasa kwa watu hao.

Kwa upande wake, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Emirate Aluminium Profile, Issa Maeda amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Ahmed Ally kama ‘kifuta jasho’ ili kumpa hamasa na kumuongezea nguvu zaidi katik kufanya jambo hilo kwa timu yake.

“Tuzo hii ni ya mwezi Aprili na haina mchakato wa kupiga Kura, kama kwa Wachezaji ambao wao wanapigiwa Kura na mashabiki wa timu, hii tuzo binafsi ya Kampuni yetu, tumeitoa kwa Ahmed Ally kutambua mchango wake katika timu ya Simba SC”, amesema Maeda.

Hata hivyo, Beki kisiki wa Simba SC, Henock Inonga amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month) mwezi Aprili sanjari na kitita cha fedha Shilingi Milioni 2 (Tsh. 2,000,000/-) baada ya kupata Kura nyingi za Mashabiki hao akiwabwaga, Wachezaji wenzake, Shomari Kapombe na Joash Onyango.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amekabidhiwa Tuzo ya aliyeupiga mwingi mwezi wa April tuzo iliyotolewa na kampuni ya Emirate Aluminium Profile.
Beki wa Simba SC, Henock Baka Inonga akikabidhiwa Tuzo ya Mchezaji bora wa Mashabiki wa Emirate Aluminium Profile, anayekabidhi Tuzo hiyo ni Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni hiyo, Issa Maeda.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...