Watu 12 Mkoani Mtwara wakiwemo watumishi 4 wa Serikali wanashikiliwa kwa kukiuka na kuhujumu zoezi la ugawaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima wa zao la korosho.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Jen.Marco Gaguti leo Juni 24-2022 wakati wa zoezi la upokeaji wa salfa ya unga Tani 6523 Eneo la Bandarini Mkaoni Mtwara.

Brig.Jen.Gaguti ameongeza kuwa watumishi wa Serikali waliohusika kwenye uhujumu huo ni watendaji wawili (2) wa kijiji pamoja na Maafisa kilimo wawili (2) ambapo kwa Sasa tayari wamishasimamiahwa kazi na taratibu za kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria zinaendelea kuchukuliwa

Aidha Gaguti ameelezea uhujumu uliofanywa na watu hao ni uchepushwaji wa viwatilifu vya maji Lita Mia Nne (400) kutoka Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara.

Gaguti ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa kamati zinazohusika na ugawaji wa pembejeo kwa wakulima Mkoani Mtwara kuendelea kufanya kazi na kufuata miongozo Kama ilivyotolewa na Serikali na yeyote atakayekiuka zoezi hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig.Jen.Marco Gaguti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...