Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania leo imekabidhi gari mpya aina IST kwa mshindi wa tatu wa kubwa ya Tesa Kimilionea. Kwenye promosheni ya Tesa Kimilionea, Airtel imekuwa ikitoa fedha taslimu Tzs 100,000 kwa washindi 100 pamoja na Tzs 1,000,000 kwa kila wiki huku kwenye droo kubwa ambayo inachezwa kila mwisho wa mwezi washindi wawili ushinda Tzs 10,000,000 na mwingine gari mpya aina ya Toyota IST.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo ya gari mpya aina ya Toyota IST kwa mshindi huyo ambaye ni Yahya Nahato mkazi wa Kondoa mkoani Dodoma, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alimpogeza kwa kuwa mshindi wa kwanza kujishindia zawadi ya gari kwenye promosheni ya Airtel Tesa Kimilionea.
‘Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza mshindi wetu wa kwanza kwa kujishindia zawadi ya gari aina ya IST kwenye promosheni hii ya Tesa Kimilionea. Hii ni promosheni maalum kwa wateja pamoja na Mawakala wa Airtel wanafanya miamala mbali mbali kwa kutumia Airtel Money kuweza kuwa mshindi.
Nawaomba wateja pamoja na wakala wa Airtel Money kutambua kwamba kila unapofanya muamala wowote kwa kutumia Airtel Money basi unaingia moja kwa moja kwenye droo ambayo kwa sasa imeboresha zaidi na hivyo kuwa kwenye ya kujishindia zawadi mbali mbali kama Tzs 1,000,000 kwa kila siku na zawadi kubwa ya Tzs 10,000,000 au gari mpya aina ya RAV 4.
Na kama tulivyomsikia mshindi wetu hapa kama alivyosema kuwa mteja au wakala wa Airtel Money haitaji kulipia chochote au kujisajili ili kuingia kwenye droo ya Tesa Kimilionea. Vile vile, unapokuwa mshindi hakuna kulipia chochote ili kupata zawadi yako. Alisema Mmbando huku akiongeza kuwa mshindi atapigiwa simu kwa kutumia namba ya huduma kwa wateja ya +255 100 na sio vinginevyo.
Kwa upande wake, mshindi huo Yahya Nahato mara baada ya kukabidhiwa gari lake mpya aina ya Toyota IST aliwashukuru sana Airtel Tanzania kwa kuweza kuleta huduma bunifu na nafuu kwa wateja ambazo leo zimemuwezesha kuweza kujishindia gari. ‘Naomba kutoa pongezi dhati kwa kampuni ya Airtel kwa promosheni hii ambayo leo mimi mwenyewe nimeweza kujishindia gari.
Ni kweli kwamba mteja au wakala haitaji kujisajili au kulipia chochote ili kuweza kuwa mshindi. Mimi nilikuwa nafanya tu miamala mbali mbali kwa kutumia Airtel Money na hatimaye nikapigiwa simu kuwa mimi ni mshindi wa gari. Nilikuwa siamini kama ni kweli mpaka nilipokuja hapa na kuonyesha gari langu, alisema Nahato.
Naomba nitoe rai kwa wateja na mawakala wa Airtel kuendelea kutumia huduma za Airtel Money kwani kila mtu anaweza kuwa mshindi. Kama mimi nimeweza kujishindia gari, basi na mwingine anayo fursa ya kujishindia fedha taslimu au pia gari kama mimi, alisema Nahato.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano (kulia) akimkabidhi mshindi wa promosheni ya Tesa Milionea Inaendelea Abdulaziz Christopher kiasi cha Tzs 1m/- baada ya kuibuka mshindi wa promosheni hiyo. Promosheni ya Tesa Kimilionea inawapa fursa wateja na mawakala wa Airtel kujishindia zawadi za pesa taslimu Tzs1, 000,000 kila siku au zawadi kubwa ya Tzs10, 000,000 au gari mpya aina ya RAV 4 kila mwisho wa mwezi pale wanapotumia huduma yeyote ya Airtel Money.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...