JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO,
MHESHIMIWA DKT. MWIGULU LAMECK NCHEMBA
MADELU (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA
SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO
YA MAPATO NA MATUMIZI KWA
MWAKA 2022/23
14
Juni 2022 Dodoma
I.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako Tukufu lipokee, lijadili na kukubali
kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2022/23. Bajeti
hii inawasilishwa kwa mujibu wa Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 23 (3) cha Sheria ya
Bajeti, Sura 439 pamoja na Kifungu cha 124 (4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge,
Toleo la Juni 2020.
2.
Mheshimiwa Spika, pamoja na hotuba hii
ninawasilisha vitabu vinne vinavyoelezea kwa kina Bajeti ya Serikali. Kitabu
cha Kwanza ni Makadirio ya Mapato; Kitabu cha Pili ni Makadirio ya Matumizi ya
Kawaida kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea na Wakala wa Serikali; Kitabu cha Tatu ni Makadirio ya Matumizi ya Kawaida kwa Sekretarieti
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa; na Kitabu cha Nne ni Makadirio ya
Matumizi ya Maendeleo kwa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali,
Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Aidha, Muswada wa Sheria
ya Fedha wa mwaka 2022 pamoja na Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali wa
mwaka 2022 nayo ni sehemu ya bajeti hii.
3.
Mheshimiwa Spika, makadirio ya Bajeti ya Serikali
kwa mwaka 2022/23 yameandaliwa kwa kuzingatia nyaraka na miongozo mbalimbali
ikiwemo: Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26
ambao umeandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020; Dira ya Maendeleo ya Afrika Mashariki 2050;
Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030;
Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo; na makubaliano mengine ya kikanda na
kimataifa ambayo Tanzania imeyaridhia.
4.
Mheshimiwa Spika, napenda kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako
Tukufu kuwasilisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23. Kwa namna ya pekee
nitumie fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini katika dhamana
hii ya kuongoza Wizara ya Fedha na Mipango.
II.
MWENENDO WA MAPATO NA MATUMIZI
2021/22
Mwenendo wa Mapato
5.
Mheshimiwa Spika, katika bajeti
ya mwaka 2021/22, Serikali ilitarajia kukusanya jumla ya shilingi trilioni 37.99 kutoka katika
vyanzo vyote vya ndani na nje ambapo hadi Aprili 2022, kiasi cha shilingi
trilioni 29.84 kimekusanywa. Mchanganuo wa mapato yaliyopatikana hadi Aprili
2022 ni kama ifuatavyo:
(i)
Mapato yaliyokusanywa kupitia
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yalikuwa ni shilingi trilioni 17.20, ambapo lengo la mwaka ni shilingi trilioni
21.78;
(ii)
Mapato yasiyo ya kodi yalifikia
shilingi trilioni 2.03, ambapo lengo la mwaka ni
shilingi trilioni 3.05;
(iii)
Mapato ya Halmashauri yalifikia
shilingi bilioni 759.0, ambapo lengo la
mwaka ni shilingi bilioni 863.9;
(iv)
Misaada na mikopo yenye masharti
nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ilifikia shilingi trilioni 3.93, sawa
na asilimia 92.0 ya lengo la mwaka la shilingi trilioni 4.27;
(v)
Mikopo kutoka vyanzo vya ndani
ilifikia shilingi trilioni 4.12, ambapo lengo la mwaka ni shilingi trilioni
4.99; na
(vi)
Mikopo yenye masharti ya
kibiashara ilifikia shilingi trilioni 1.81, ambapo lengo la mwaka ni kukopa
shilingi trilioni 3.05.
Mwenendo wa Matumizi
6.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Aprili 2022, jumla
ya shilingi trilioni 29.40 zimetolewa
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 18.79, zilitolewa kwa ajili
ya matumizi ya kawaida ambazo zinajumuisha shilingi
trilioni 6.73 kwa ajili ya mishahara, shilingi trilioni 4.79
Matumizi Mengineyo na shilingi trilioni 7.27 kugharamia deni la Serikali.
Jumla ya shilingi
trilioni 10.61, sawa na asilimia 74.1 ya lengo
la mwaka zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kiasi hiki hakijumuishi baadhi ya fedha zilizopelekwa
moja kwa moja kwenye utakelezaji wa miradi (D-fund). Fedha hizi zitajumuishwa
kwenye hesabu za Serikali mwishoni mwa mwaka wa fedha pindi taratibu za
kihasibu zitakapokamilika.
Tathmini ya Uhimilivu wa Deni la Serikali
7.
Mheshimiwa Spika, hadi Aprili
2022, deni la Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44, sawa na ongezeko la
asilimia 14.4 ikilinganishwa na shilingi trilioni 60.72 Aprili 2021. Kati ya kiasi
hicho, deni la ndani ni shilingi trilioni 22.37, sawa na asilimia 32.2 na deni
la nje ni shilingi trilioni 47.07, sawa na asilimia 67.8. Kati ya deni la nje,
deni lenye masharti ya kibiashara ni shilingi trilioni 14.27, sawa na asilimia
30.3. Hivyo, sehemu kubwa ya deni la nje ni mikopo yenye masharti nafuu.
8.
Mheshimiwa Spika, tathmini ya uhimilivu
wa deni la Serikali iliyofanyika Novemba 2021 kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo,
Dhamana na Misaada Sura 134 ilionesha kuwa viashiria vya deni la Serikali viko
ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na
mrefu. Katika
Tathmini hiyo, viashiria vinaonesha kuwa: uwiano wa thamani ya sasa ya deni la
Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.0 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia
55; uwiano wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni asilimia 18.8
ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 40; na uwiano wa thamani ya sasa ya deni la
nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 142.4 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia
180.
Tathmini ya
Kukopesheka kwa Nchi (Credit Rating)
9.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka
2021/22, zoezi la tathmini na ukadiriaji wa kukopesheka kwa nchi (credit
rating) ambalo lilisimama hapo awali lilianza tena kupitia benki ya Citibank
ambayo ilikuwa mshauri wa Serikali. Hadi kufikia mwezi Mei 2022, Serikali
imefikia hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ununuzi ambapo imefanikiwa
kuchagua kampuni mbili ambazo zinatambulika kimataifa na kupitia mikataba yao.
Aidha, Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni hizo pamoja na kuandaa
takwimu mbalimbali ambazo zitatumika katika zoezi la tathmini na ukadiriaji wa
kukopesheka. Serikali inategemea kukamilisha zoezi hili ndani ya mwaka 2022/23.
Naomba nichukue fursa hii kuziomba taasisi za Serikali, za binafsi na benki
zitakazopata nafasi ya kuhojiwa na wataalamu wa Kampuni hizo kutoa ushirikiano
kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi. Kukamilika kwa zoezi hili kutatuwezesha
kuongeza wigo wa wakopeshaji kwa Serikali na makampuni binafsi hususan katika
masoko ya mitaji ya kimataifa (International Capital Markets).
III.
BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2022/23
10.
Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23 ni ya pili katika
utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 -
2025/26 wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo
ya Watu”. Aidha, dhima kuu ya bajeti ya mwaka
2022/23 kama ilivyokubaliwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni
“Kuongeza Kasi
ya Kufufua Uchumi na Kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya Kuboresha
Maisha”. Katika
utekelezaji wa dhima hiyo kwa mwaka 2022/23 kipaumbele kitakuwa katika sekta za
uzalishaji zikiwemo Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Nishati, Uwekezaji na Biashara.
Lengo la Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa
CCM ni kujenga uchumi, kukabiliana na umasikini pamoja na ukosefu
wa ajira hasa kwa vijana.
Shabaha za Uchumi Jumla
11.
Mheshimiwa Spika, kutokana na
mambo yaliyozingatiwa katika uandaaji wa bajeti hii, shabaha za uchumi jumla
katika kipindi cha mwaka 2022/23 ni kama ifuatavyo:
(i)
Ukuaji wa Pato Halisi la Taifa
kufikia asilimia 4.7 mwaka 2022 na asilimia 5.3 kwa mwaka 2023;
(ii)
Kuendelea kudhibiti kasi ya
mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya
wastani wa asilimia kati ya 3.0 hadi 7.0
katika muda wa kati;
(iii)
Mapato ya ndani kufikia asilimia
14.9 ya Pato la Taifa mwaka 2022/23;
(iv)
Mapato ya kodi kufikia asilimia
11.7 ya Pato la Taifa mwaka 2022/23; na
(v)
Kuwa na akiba ya fedha za kigeni
kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa
kipindi kisichopungua miezi minne (4);
IV.
MAMBO MUHIMU KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
12.
Mheshimiwa Spika, nchi zote duniani zinapita kwenye athari kubwa za UVIKO 19
na vita kati ya Urusi na Ukraine iliyoanza Februari 2022 ambayo imeendelea
kuleta athari katika mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania kutokana na
mwingiliano wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Madhara ya UVIKO-19, yamekuwa
na makali zaidi baada ya uchumi kuanza kurejea, kwa kuwa nchi zilikuwa katika “lockdown”
na nyingine kupunguza uzalishaji wa bidhaa. Uchumi unaporejea katika hali ya
uzalishaji mataifa yote yanahitaji bidhaa ambazo ziliachwa kuzalishwa hivyo
kusababisha upungufu. Kungali hali iko hivyo, vita kati ya Urusi na Ukraine imeongeza
upungufu wa bidhaa kwa kuathiri uzalishaji na mnyororo wa usambazaji. Kwa
mujibu wa Shirika la Chakula Duniani, nchi za Urusi na Ukraine ni kati ya nchi
zenye uzalishaji na uuzaji mkubwa wa mazao mbalimbali ikiwemo ngano, mafuta ya
kula na shayiri.
13. Mheshimiwa Spika, nchi ya Urusi ni ya pili katika uzalishaji wa gesi asilia na
bidhaa za mafuta ya petroli duniani. Kadhalika, nchi ya Ukraine ni miongoni mwa
nchi zinazozalisha mafuta ya alizeti kwa wingi duniani. Kufuatia madhara haya ya vita, ni dhahiri
kuwa uchumi na gharama za maisha duniani hazitabaki zilivyokuwa awali. Ndio
maana Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameelekeza
bajeti hii ya Serikali ijikite kuchukua hatua za kutoa unafuu kwa wananchi na
kufufua uchumi. Bajeti hii itatilia mkazo Sera
za Mapato, Sera za matumizi, kujali ufanisi (Value for Money), mapambano ya
vitendo vya rushwa na kuwekeza
kwenye Sekta za uzalishaji ili
kutengeneza ajira kwa vijana.
Mikakati ya kuongeza
Mapato Mwaka 2022/23
14. Mheshimiwa Spika, nawapongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania na taasisi zingine
zinazokusanya mapato na maduhuli ya Serikali. Tumepiga hatua kubwa kwenye
makusanyo ya ndani. Hadi Aprili 2022, ukusanyaji wa mapato ya kodi na yasiyo ya
kodi ikijumuisha mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa umefikia shilingi
trilioni 19.99, sawa na asilimia 93.3 ya makadirio ya kukusanya shilingi
trilioni 21.42 katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi
yamefikia shilingi trilioni 17.20, sawa na asilimia 94.5 ya lengo la kukusanya
shilingi trilioni 18.2, mapato yasiyo ya kodi yamefikia shilingi trilioni 2.03,
sawa na asilimia 81.2 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 2.5 na mapato ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa yamefikia shilingi bilioni 759.0, ikiwa ni
asilimia 104.8 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 724.1 katika kipindi
hicho.
15.
Mheshimiwa Spika, pamoja
na mafanikio hayo, bado kuna vitendo vya rushwa kwenye ukusanyaji wa mapato, hasa kwenye
kodi kubwa, mapato ya Mamlaka za Serikali za mitaa na ardhi. Kuna mapato ya
Serikali yanaingia kwenye mifuko ya watu binafsi. Hii inafanyika kwa kukadiria
viwango vya juu ili katika majadiliano ya kwenda kwenye kodi stahiki
kinapunguzwa kiasi chini ya kile kinachostahili na kilichopunguzwa kinaingia
mifuko binafsi. Serikali imeshapokea taarifa kadhaa za matukio ya aina hii na
inaendelea kulifuatilia kwa umakini sana jambo hili. Wale wanaokataa kutoa
rushwa ndio wanaoonewa zaidi, ndio wanaobambikwa makadirio yasio halisi kwa
kuwakomoa, ndio wanaotishiwa kufilisiwa. Jambo hili halikubaliki. Nitoe rai
jambo hili liachwe mara moja. Tuache utaratibu wa kufanya majadiliano
(bargaining) kwenye kulipa kodi. Watumishi wa umma wanaokusanya kodi na
maduhuli ya Serikali wanaowaomba wafanyabiashara wawapunguzie wanachotakiwa
kulipa ili kisichoingia serikalini wapate wao wanafanya makosa ya uhujumu
uchumi. Kadhalika wapo wafanyabiashara na wauza maduka wanaowaambia wananchi “nikupe bei ya
risiti ya TRA au bila risiti”, na bei ile isiyo na risiti inakuwa ndogo kuliko bei ya
risiti ili kuwashawishi wakwepe kulipa mapato ya Seriakili na wao wenyewe
wabaki na kodi ya Serikali. Huu ni uhujumu uchumi. Naagiza vitendo hivyo vikome
mara moja na ambaye hataacha atakutana na mkono wa sheria.
16. Mheshimiwa Spika, nitoe rai kwa watanzania wote kulipa kodi wanayostahili
kulipa, wala wasiogope vitisho, na wala wasidhanie kuwa kuna wakati watakulipizia
kisasi, toa taarifa ofisi ya TAKUKURU
iliyo karibu nawe, ama toa taarifa Idara ya Usalama wa Taifa iliyo karibu nawe.
Watumishi wa aina hiyo watakaobainika
hutawakuta tena ofisi za umma, wala hatutawahamisha, Tutawafukuza kazi. Mheshemiwa
Rais anachukizwa sana na ukosefu wa maadili na uaminifu wa baadhi ya watumishi
wa umma. Asitokee anayedhani ana haki sana ya kuwa mtumishi wa umma, hii ni
dhamana tu. Wala asitokee anayedhani vijana wahitimu wa kitanzania walioko
mtaani na hawana kazi akadhani hawana haki ya kuwa watumishi wa umma. Tunao
uwezo wa kupangua safu nzima ya utumishi wa umma na tukapanga safu mpya ya
vijana hawa walioko mtaani. Kwenye uadilifu na uaminifu, hata tusibabaishane, Tutawakamata, Tutawashitaki na Tutawafunga.
Lazima
tukomeshe kabisa vitendo vya rushwa kwenye mapato na matumizi.
17.
Mheshimiwa Spika, mambo mengine tunayotarajia kuyafanya kwenye sera ya mapato
ni kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kufanya makadirio ya kodi kwa
wafanyabiashara wadogo ambao hawana uwezo wa kutunza kumbukumbu na kutengeneza
hesabu za biashara zao (Presumptive Regime), kuwekeza kwenye matumizi ya
teknolojia ili kurahisisha uwasilishaji wa ritani za kodi kielektroniki
(electronic filing) na ulipaji kodi kwa wakati; Kuimarisha Mfumo wa Serikali wa
Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato (GePG) na kuhimiza malipo ya Serikali
kutumia Namba ya Kumbukumbu ya Malipo; na kuimarisha mifumo ya usimamizi katika
Mashirika, Taasisi za Umma na Wakala za Serikali ili kuongeza ufanisi na
kuhakikisha gawio na michango stahiki inawasilishwa kwa wakati. Ili kukuza
mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi, kutoa ajira na kuongeza mapato,
Serikali inapanga kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuipa
nafasi zaidi sekta binafsi. Aidha, Serikali imepanga kuendeleza uanzishwaji wa
vituo vya pamoja vya utoaji huduma ili kuwezesha huduma muhimu zinazohitajika
katika kuanzisha na kufanya biashara kupatikana sehemu moja.
Mkakati wa Kubana Matumizi
18. Mheshimiwa Spika,
Sera za matumizi katika mwaka 2022/23 zitakuwa za kubana na kuondoa
matumizi yasiyo ya lazima. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali inatarajia kudhibiti ununuzi na matumizi ya
magari kwa kuzingatia Waraka wa Rais na.1 wa mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana
matumizi ya Serikali na Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Na. 2 wa mwaka 2021
kuhusu utaratibu wa kutumia magari, aina na stahili za magari kwa viongozi
katika utumishi wa umma ili kubana matumizi. Baadhi ya maeneo yenye gharama
kubwa sana kwa serikali ni Ununuzi wa magari, Ununuzi wa mafuta ya uendeshaji,
Ununuzi wa vipuli na matengenezo. Tunapanga kuchukua hatua za muda mfupi na za
muda mrefu. Lazima, matumizi ya
Serikali na matumizi ya watumishi wa umma yote yaakisi ugumu wa maisha
wanayopitia wananchi wetu kufuatia athari za majanga hususan ya UVIKO-19 ili
fedha zinazopatikana zifanye mambo muhimu hapa nchini. Hatua za muda mfupi zitakazochukuliwa ni
kupunguza safari za ndani na nje, kukata fedha za ununuzi usio wa lazima,
kupunguza ukubwa wa uwakilishi kwenye mikutano ya ndani na nje, na tutapimiana
mafuta ya magari ya Serikali kila mwezi kufuatana na shughuli za lazima.
Utaratibu huu unatumika kwa wabunge, na hawajaacha kufanya shughuli majimboni
mwao, BOT wanapimiwa, baadhi ya Taasisi za UN wanapimiwa. Namwelekeza Mlipaji Mkuu wa Serikali afanye uchambuzi wa wastani wa
mahitaji ya mafuta kufuatana na aina ya majukumu, ulazima wa majukumu na ngazi
katika utumishi.
19.
Mheshimiwa Spika,
kwa upande wa hatua za muda wa kati na
muda mrefu, napendekeza Serikali kubadili kabisa utaratibu uliopo kwa kuwakopesha magari watumishi wenye
hadhi ya kuwa na gari la Serikali wawe na magari yao wenyewe, wafanye
matengenezo wenyewe, wanunue vipuri wenyewe na masuala ya mafuta yaangaliwe kwa
utaratibu utakaoonekana unafaa. Kwa sasa Serikali ina magari zaidi ya 15,742, pikipiki 14,047 na mitambo
373 na inatumia zaidi ya shilingi 558,453,134,226.05
kwa mwaka kwa ajili ya ununuzi wa magari, ununuzi wa mafuta ya uendeshaji,
ununuzi wa vipuri na matengenezo ambapo kwa sasa ni zaidi ya shilingi bilioni 500. Ukiondoa vyombo vya ulinzi na
usalama pamoja na Mahakama, upande wa Serikali wabaki viongozi wakuu wa Wizara,
Mashirika, wakala, mikoa, wilaya na Miradi ambao wasimamizi watakuwa eneo la
mradi (site) muda mwingi ambapo kwenye makundi haya hawatazidi watano kwa taasisi,
wengine wote wenye stahili ya gari la Serikali wakopeshwe, watumie magari yao,
watasimamia vizuri matumizi, matengenezo, mafuta na vipuri. Tutaondoa utaratibu uliozoeleka, dereva na
gari anapitishwa chini, bosi anapanda ndege mpaka Mwanza au Mbeya kutoka Dar es
Salaam na kurudi hivyo hivyo. Kuna utafiti wa siri ulifanywa, kwa siku moja
yalibainika magari ya Serikali yaliyotoka Dodoma kwenda Dar es Salaam yalikuwa
132, na yaliyokuwa yanatoka Dar es Salaam yakipishana kuja Dodoma yalikuwa 76,
na mengine 8 yalikuwa yamepinduka. Je kwa mwezi ni gharama kiasi gani?
20.
Mheshimiwa Spika, kwa utaratibu
huo gharama za matumizi ya magari serikalini zitakuwa takribani shilingi 50,508,038,843.09. Zaidi ya
shilingi billion 500 zitaokolewa na kuelekezwa kwenye ununuzi wa dawa muhimu hospitalini, kutoa
mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati, na kutekeleza miradi ya
maendeleo. Tumezidi kupenda ubosi, magari makubwa kwa kila mtu serikalini,
matumizi ya starehe, wakati katika nchi yetu bado kuna watu wanapata shida kupata
mlo mmoja.
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania
ameielekeza Wizara ya Fedha na Mipango
ifanyie kazi jambo hili la kuelekeza fedha kwenye matumizi ya msingi tu. Jambo hili
halitaathiri mtumishi bali litafanyika gradually, yaani by phasing out, yaani
tunabadilisha kadri watu wanavyopanda kustahili kukopa na kutokuajiri madereva
kadri wanavyostaafu na kadri maafisa wanavyohamia skimu za kukopa. Madereva
wengine watabaki kwa viongozi, magari ya miradi ya site, na magari ya pool.
Mtoto wa Dereva sio lazima naye aje awe dereva.
21.
Mheshimiwa Spika,
sambamba na hayo, Serikali
itaachana na mfumo wa sasa wa Ununuzi wa Umma (Transactional Procurement) ambao
umeshindwa kuleta tija kwa kuwa msingi wake mkubwa ni ulinganishaji wa zabuni
zilizofunguliwa badala ya bei za bidhaa na huduma ambazo tunazijua. Mara nyingi
bei hizi za ununuzi zimekuwa kubwa kuliko zile zilizopo sokoni kwa jumla na
hata rejareja (wholesale and retail) na ingekuwa tunanunua kwa ajili ya
nyumbani kwetu au kwa ajili ya kampuni zetu tusingekubali bei hizo. Napendekeza
kuwa, ununuzi wa umma uwe wa kimkakati (Strategic Sourcing) kwa kuzingatia
ukubwa wa ununuzi wa Serikali na sekta ya umma kwa ujumla (Economies of Scale)
pamoja na uwiano na mfanano wa bidhaa na huduma zinazotumika serikalini na
sekta ya umma yaani synergies. Sasa Serikali ni moja, bidhaa zinafanana, hata ofisi zilizoko mkoa
mmoja, ila inatokea kila mmoja anakuwa na bei zake licha ya bidhaa
kufanana.
22.
Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti matumizi, Serikali imepanga
kufanya maboresho katika mfumo wa ununuzi wa umma ili kuhakikisha ununuzi wa
umma unakuwa wenye tija na unaoendana na ubora na thamani ya fedha. Tutaendelea
kuboresha Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (TANePS) ikiwemo kuweka
ukomo wa bei za bidhaa na huduma zinazotumika serikalini ili kudhibiti matumizi
ya fedha za Serikali; Wizara ya Fedha na Mipango itahakikisha kuwa, bei zote za
bidhaa na huduma zinazotumika sokoni kwa jumla na rejareja (Price Catalogue)
zinaingizwa kwenye mfumo wa TANePS na kuwa kikomo (limit) cha bei
zitakazotumika Serikalini. Hii itasaidia kuhakikisha kwamba mfumo wa TANePS
hauruhusu watoa huduma na wakandarasi au wauza bidhaa wanaotoa bei zilizo zaidi
ya soko kupata zabuni (tender) kwenye sekta ya umma.
23.
Mheshimiwa Spika,
katika kutekeleza hatua
hii, Wizara ya Fedha na Mipango itatoa Waraka wa Hazina kuelekeza idara na
taasisi nunuzi kununua bidhaa zinazofanana kwa bei ya kikomo. Endapo kutakuwa
na ulazima wa kununua magari kwa wingi, Serikali itafanya mazungumzo na Toyota
Tanzania na Japan (kwa njia za kidijitali) ili kufanya makubaliano ya jumla
(framework agreement) yatakayowezesha Serikali kupata bei nafuu kama ilivyo kwa
mashirika makubwa ya kimataifa kama vile UNDP. Hii itasaidia kuokoa fedha
katika ununuzi wa magari pamoja na vipuri. Zoezi hili litafanywa na Wizara ya
Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi. Fedha zitakazookolewa kutokana na
hatua hizi Serikali itazielekeza katika ujenzi wa vyuo vya ufundi kwenye Wilaya
zetu kwa ajili ya watoto wetu.
24. Mheshimiwa Spika, napendekeza matumizi ya mifumo ya TEHAMA iwe chaguo namba
moja katika utekelezaji wa shughuli za Serikali ili kubana matumizi. Kuanzia
mwaka ujao wa fedha ofisi za serikali zianze paperless operations kwenye
shughuli zake. Kila shughuli zifanyike kwa mtandao, mbona Bunge mmeweza? Kumbi
za Mikoa na Wilaya zote ziwe na miundombinu ya mikutano ya njia ya
Mtandao (Virtual Meeting). Hata wabunge mtaweza kushiriki vikao vya Mabaraza ya
Madiwani mkiwa Dodoma au hata nje ya nchi. Utaratibu wa kuitana Wakuu wa Mikoa
nchi nzima, Wakuu wa Idara, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa
Halmashauri, na magari kwa nchi nzima na umbali wote kuja kukaa mahali na kusikiliza ni mzigo kwa
walipa kodi. Tumekopa fedha kwa ajili ya
mkongo wa taifa, tunalipa deni, ila tunatumia gharama kubwa kwa
kufanya kazi manually. Mheshimiwa
Rais anajenga chuo kikubwa cha TEHAMA, lakini tunaogopa TEHAMA. Tunataka kufuta usemi wa “Government works on papers” Sasa tunasema “Government
works on records”. Tumeongea na Wizara ya Kisekta kama alivyoelekeza
Mheshimiwa Rais kujadili utekelezaji wa jambo hili, Wizara tafuteni mtu wa
kusimika hiyo mitambo kila Wilaya. Eti mkurugenzi anakuja tokea Wialaya ya
pembezoni gharama yote ile eti ameleta barua, au anakuja kutoa ufafanuzi, au
wanakuja nchi nzima kwenye kikao ila anaongea mmoja kwa uwakilishi.
25. Mheshimiwa Spika, kuhusu ufanisi katika Miradi ya Maendeleo, Mheshimiwa Rais ameelekeza
kuangalia upya taratibu za ununuzi na thamani ya fedha kwenye Miradi ya
Maendeleo. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG
ilionesha bado kuna dosari katika matumizi ya Serikali hususani kwenye ununuzi
mkubwa na miradi ya maendeleo. Serikali imefuatilia eneo hili na kugundua mfumo
wa kufanya ukaguzi wa taratibu za ununuzi (Compliance Audit) na wa kifedha (Financial
Audit) ina upungufu. Yapo mazingira ya taratibu zote kufuatwa katika ununuzi,
sheria zote za ununuzi kufuatwa, na hatua zote za ukaguzi kufuatwa lakini fedha
ya umma kuibiwa. Hii inatokana na baadhi ya watumishi wa umma wasio waaminifu
kupanga njama na wafanyabiashara wasio wazalendo kupandisha bei za bidhaa
kwenye zabuni na kujipangia hata huyo aliyeshindania kwa kiwango cha chini
anakuwa mbali na bei ya soko au gharama halisia.
26.
Mheshimiwa Spika, kwenye mchezo wa aina hii, wanafuata sheria ya ununuzi,
wanafuata taratibu za kumchagua aliyeshinda bei ya chini, ila kwa kuwa hiyo
iliyoshindaniwa kwa bei ya chini ni ya chini tu ikilinganishwa na wazabuni
wengine ambapo zabuni imefanywa kwa njama basi bei hizo zinakuwa juu sana
ikilinganishwa na bei za bidhaa hizo hizo kwa bei ya soko. Hawa ni watu wanaoiba japo
wamezingatia sheria. Serikali itaendelea kumjengea uwezo CAG ili kumwezesha kukagua thamani ya fedha kwenye miradi yote mikubwa (Value for Money) na kufanya ukaguzi
kwa wakati ili kukabiliana na tatizo hili. Mheshimiwa
Spika, napendekeza kumwongezea fedha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili apate
watumishi wa kutosha kwa kuajiri na kuwahamisha watumishi kutoka idara yoyote
ya Serikali na kuwajengea uwezo kwa mafunzo na weledi wa ukaguzi wa thamani ya
fedha ili kuweza kukabiliana na tatizo hili. Mheshimiwa Spika, Serikali itafanyia marekebisho Sheria ya Ununuzi wa
Umma ili kuziba mianya inayotoa fursa ya miradi kutekelezwa bila kujali thamani
ya fedha (Value for Money) kama alivyoelekeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania.
27.
Mheshimiwa
Spika, Serikali itaendelea
kuimarisha vitengo vya ukaguzi wa ndani kwa kuvijengea uwezo wa kitaaluma na
kuongeza idadi ya watumishi katika fani mbalimbali kama vile TEHAMA, uhandisi,
ukadiriaji majenzi, wakemia, wanasheria na fani nyingine ili kuondokana na
dhana ya wakaguzi wa ndani kuwa na taaluma ya fedha pekee. Aidha, Serikali
itafanya marekebisho ya Kanuni za Fedha za Umma kwa kuziwezesha Kamati za
Ukaguzi kuwa na wajumbe wa nje watatu ikiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi
ili kuongeza uhuru na ufanisi wa kamati za ukaguzi kupitia Muswada wa Sheria ya
Fedha wa Mwaka 2022. Pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Kanuni hizo
yatazitaka Kamati za Ukaguzi kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa ndani kwa
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kila robo mwaka.
28. Mheshimiwa Spika,
Serikali itafanya tathmini ya muundo na majukumu ya Idara ya Mkaguzi wa Ndani
Mkuu wa Serikali ikiwemo kufanya stadi ya kujifunza kutoka nchi nyingine zenye
Idara ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu Serikali kama Tanzania ili kuangalia muundo
unaostahili na kukidhi mahitaji ya Idara hiyo kutekeleza majukumu yake kwa
uhuru na ufanisi. Vilevile napendekeza
Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kuwa na fungu lake (Independent Vote)
pamoja na kuongeza idadi ya wakaguzi wa ndani ili kuimarisha na kuboresha
ufanisi katika utendaji. Napendekeza
kuanzia mwaka wa fedha 2022/23 taarifa za wakaguzi wa ndani zipelekwe moja kwa
moja kwa Internal Auditor General
(IAG) kama alivyoelekeza Mheshimiwa Rais wakati anapokea taarifa ya CAG. IAG atakuwa
anawasilisha taarifa hizi kwenye Baraza la Kazi chini ya Mheshimiwa Waziri Mkuu
ili kila Waziri wa kisekta aweze kupokea hoja
zinazomhusu, kuzifanyia kazi na kuchukua hatua za kinidhamu. Wakaguzi wa
ndani wa ofisi mbalimbali watatoa msaada na ushauri kwa maafisa masuhuli husika
ila taarifa zote ziende kwa IAG na nakala zipelekwe kwa viongozi walio juu ya
maafisa masuhuli. Kwenye ngazi za Halmashauri, nakala ziende kwa wenyeviti,
mamea na wakuu wa Wilaya; kwa Sekretarieti za Mikoa, nakala ziende kwa Mkuu wa
mkoa; Kwa wizara, nakala ziende kwa mawaziri; na kwa taasisi, mashirika na
wakala, nakala ziende kwa wenyeviti wa Bodi.
29.
Mheshimiwa
Spika, kuna wakati inatokea tunaona
miradi ikikamilika, fedha zote zikiwa zimetumika lakini miradi ikiwa chini ya
viwango, jengo au mradi unakamilika ungali bado unanukia rangi lakini ukiwa
umetapakaa nyufa kila kona, sementi na tofali zikiwa ni mchanga. Katika
kukabiliana na hali hiyo, Serikali inamwelekeza IAG pamoja na vitengo vya
ukaguzi wa ndani kuanza kufanya Technical
Audit badala ya (Financial Audit) peke yake na kuanza kufanya ukaguzi kwa
wakati (Real Time Audit) na ukaguzi wa mifumo (Systems Audit) ili kupunguza
uwezekano wa upotevu fedha kupitia mifumo ya ukusanyaji au matumizi mabaya ya
fedha za umma.
30. Mheshimiwa
Spika, kwenye eneo la usimamizi wa
fedha za umma, Serikali itahakikisha kuwa Sheria ya Fedha za Umma SURA 348
inasimamiwa na kutekelezwa ipasavyo na pale itakapotokea sheria na taratibu za
usimamizi wa fedha zimekiukwa ikiwa ni pamoja na kushindwa kujibu hoja
zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na hoja
za wakaguzi wa ndani, Afisa Masuuli wa
Fungu husika pamoja na Maafisa wake wa chini watachukuliwa hatua kulingana na
Kanuni za fedha zinazohusiana na adhabu (Surcharge and Penalties) za mwaka
2005. Baadhi ya hatua hizo ni pamoja na kuwakata mshahara kati ya asilimia 5
hadi 30 kwa mwezi kulingana na uzito wa kosa waliloshiriki kulitenda na
kupendekeza kwa Mamlaka zao za nidhamu, kuvuliwa wadhifa alionao au kuondolewa dhamana ya kuwa Afisa
Masuuli wa fedha za Fungu husika.
31.
Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Serikali imetoa mwongozo wa ufuatiliaji
na tathimini (Monitoring Evatuation)
yaani (M&E), na sasa inaandaa Sera ya M&E, na baadae Sheria ya M&E.
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani, Rais wa
Jamhuri ya Mungano wa Tanzania anakerwa sana na udhaifu uliopo katika eneo
la M&E serikalini. Eneo hili litaongezewa rasilimali watu na fedha na litapewa
malengo yanayopimika. Pamoja na hayo, napendekeza kuanzia mwaka ujao wa fedha
taarifa za M&E ziwasilishwe kwenye Baraza la Kazi chini ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu.
32.
Mheshimiwa Spika, Vitendo vya Rushwa vinasababisha utekelezaji wa miradi kuwa chini ya viwango
kwa kuwa fedha zilizopangwa kwenda kwenye mradi mingine zinachepushwa na kwenda
kwenye mikono ya watumishi wasio wazalendo. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania amelikemea vikali jambo hili. Watu wanapanga kuanzia wakati wa
maandalizi ya bajeti, wanafuatilia mchakato wote, siku ikipitishwa na Bunge
wanakesha wakishangilia bajeti yao imepita, mradi unaposainiwa wanaanza
kugawana fedha kabla ya utekelezaji wa mradi. Serikali itaendelea kuimarisha Technical
Audit, Value for Money Audit na Real
Time Audit katika mwaka ujao wa Fedha. Aidha, Serikali haitawanyima fedha
wananchi wa halmashauri yoyote kwa sababu ya hati chafu, wala haitarudisha fedha kwenye Mfuko Mkuu kwa
sababu hazijatumika kutokana na sababu za uzembe wa baadhi ya watumishi wa
umma. Wananchi hawahusiki na hati chafu. Tutawabaini wazembe,
Tutawakamata, Tutawashitaki na Tutawafunga.
33.
Mheshimiwa Spika, watumishi wa umma ni kiungo muhimu sana katika maendeleo
ya nchi. Mikataba yote inaingiwa na watumishi wa umma; ununuzi wowote wa
Serikali unafanywa na watumishi wa umma; miradi yote ya Serikali inatekelezwa
na watumishi wa umma; na mapato yote yanakusanywa na watumishi wa umma.
Wananchi waliwasomesha watumishi wa umma kwa kujinyima, wamewaamini
wakusanye na kutumia kodi zao kwa kuwapa huduma. Bado kuna vitendo vingi kwenye
utumishi wa umma vinavyopunguza ufanisi katika Taifa lao. “Wage bill” yetu ni kubwa kuliko viwango
vinavyotakiwa kiuchumi na wakati huo huo ikama hazijatimia na kila mtaa tuna
kijana anatafuta kazi. Hii ina maana kuna watu wanalipwa bila kufanya kazi au
wanalipwa bila kuwa na ufanisi kazini.
34. Mheshimiwa Spika, imezoeleka kwa mfano Makatibu Wakuu, Manaibu, Wakuu wa
Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Makatibu Tawala
wa Wilaya, wakurugenzi, wakuu wa taasisi mbalimbali, wakuu wa idara mbalimbali
tangu uhuru wakitenguliwa huendelea kulipwa mshahara ule ule sawa na aliyeko
kazini mpaka anastafu. Unaweza kukuta nchi ina Wizara 25 ila ina Makatibu Wakuu
50 au zaidi, au Halmashauri 184 lakini kuna wakurugenzi 300 au zaidi na hivyo
hivyo kwa nafasi nyingine. Wengine wamesabaisha upotevu na hasara kwa Taifa,
wote wanaendelea kuwabebesha mzigo watanzania na wanaziba nafasi ya ajira mpya
kwa vijana kwa kulipwa mshahara wa nafasi walizotolewa. Napendekeza yeyote aliyetokea kwenye nafasi
yake ya kuteuliwa akitolewa akabaki kwenye utumishi wa umma arejee pia kwenye mshahara wake wa zamani ili
kuwapunguzia watanzania mzigo wa kuwalipa watu waliokaa benchi huku wakiziba
nafasi za vijana wapya kuajiriwa. Mambo haya hayavutii lakini lazima tuambizane
ukweli. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
anakerwa kuona fedha nyingi zinakwenda kwenye matumizi ya kawaida
35. Mheshimiwa
Spika, napendekeza mashirika yote ya umma yenye kufanya kazi kwa
misingi ya kibiashara yafanye kazi kwa ufanisi na faida. Yale yasiyofanya kazi
kibiashara tutayapima kwa namna wanavyowezesha uchumi kuchangamka na jinsi
wanavyoimarisha huduma wanazozitoa kwa jamii. Mashirika mengi ni mzigo kwa
Serikali kwa kutegemea ruzuku kutoka serikalini ili yajiendeshe. Kwa nchi
zilizoendelea, mapato makubwa ya Serikali yanatoka kwenye mashirika yake ili
kuwapunguzia mzigo maskini wa kulipa kodi ili ziendeshe mashirika hayo lakini
pia kupunguzia Serikali kutegemea kukusanya fedha kutoka kwa watu maskini.
Napendekeza wakuu wote wa mashirika ya umma wafanyiwe usahili kwa ushindani.
Napendekeza nafasi zianze kutangazwa
punde nafasi ikiwa wazi ili wenye sifa wajitokeze na wafanyiwe usaili na
iwe hivyo hivyo kwa bodi. Wenye sifa ndio wafanyiwe upekuzi kufanyiwa uteuzi na
kupewa mkataba wenye malengo yanayopimika. Mashirika na taasisi zingine, bodi na Menejimenti zimezidisha urafiki sana na wanaendesha ofisi
kirafiki, hakuna uwajibikaji wa kutosha, hii inakiuka misingi ya mashirika kuwa
na bodi za wakurugenzi. Hii inasababisha watu wakikabidhiwa shirika la umma
wanageuza ni mali yao au duka.
36.
Mheshimiwa Spika, natambua kuna maeneo yatakayogusa sheria na kanuni mbalimbali,
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametuelekeza isiwepo sheria yoyote inayotumika
kama kikwazo cha kuwaletea watanzania ufanisi. Serikali, itafanyia marekebisho Sheria mbalimbali na kanuni
zitakazoguswa na maelekezo ya mheshimiwa Rais yanayolenga kuongeza ufanisi
Serikalini. Najua maswala ya udhibiti wa matumizi, udhibiti wa vitendo vya
rushwa, udhibiti wa uzembe, udhibiti wa ununuzi usiozingatia thamani ya fedha (value
for money) yanagusa maslahi ya watu na yatanifanya niwe unpopular Finance Minister, na hata siku nikitoka kwenye nafasi hii
marafiki watakaoona nilikwamisha dili zao potelea mbali watabaki wananchi wa Iramba
ambao huwa wanabaki nami hata nikiwa nje ya uwaziri. Mheshimiwa Rais
amenielekeza niyafanyie kazi maeneo haya ya mapato na matumizi ya nchi, nami
nitayasimamia, nawaomba waheshimiwa wabunge tumuunge mkono mheshimiwa Rais
wetu, hii ni nia njema ya kuwakwamua watanzania kwenye umasikini.
Sekta za Uzalishaji
37. Mheshimiwa Spika, kuhusu Sekta za Uzalishaji na Ajira kwa Vijana, Taifa letu ni Taifa la Vijana, (wastani wa miaka 18). Miaka ya
sitini, miaka ya sabini na miaka ya themanini vijana walikuwa wanahudumia wazee
na watoto. Njia ilikuwa rahisi kwa wahitimu wakitafutwa wangali masomoni
wachague wanataka kwenda kufanya kazi taasisi gani. Hali haiko hivyo sasa. Kwa
sasa, wazee ndio wanahudumia vijana na watoto wao. Ni kawaida sasa kukuta mzee
wa kijijini au mstaafu akiwahudumia vijana wahitimu. Uwiano huu sio mzuri kwa
Taifa letu kuwa na nguvu kazi kubwa ambayo haiko kazini licha ya uwekezaji
mkubwa uliowekwa katika sekta za uzalishaji.
Mipango yetu sasa na Sera zetu sasa lazima zijibu mahitaji ya vijana wa
Tanzania.
Sekta ya Kilimo
38. Mheshimiwa Spika, katika kuwekeza kwenye
sekta za uzalishaji na zinazotengeneza ajira kwa vijana, Serikali ya CCM inayoongozwa
na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imeongeza bajeti ya Kilimo kutoka shilingi billion 294 hadi shilingi bilioni
954 na itaendelea kuongezeka kila mwaka. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa
sekta ya kilimo inakua kwa zaidi ya asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. Bajeti ya
mwaka 2022/23 ni msingi muhimu kufikia lengo kuu hilo. Malengo mengine ni
kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula ndani ya nchi na kuuza nje ya nchi, kuongeza
thamani ya mauzo ya mazao nje ya nchi kutoka dola za Marekani bilioni 1.2 hadi
zaidi ya dola za Marekani bilioni 5 ifikapo mwaka 2030 ili kuongeza uhimilivu
wa deni la Taifa. Serikali inakusudia kuongeza mauzo ya Mazao ya Bustani (Horticulture) kutoka dola
za Marekani milioni 750 kwa mwaka hadi dola za Marekani bilioni 2 mwaka 2030.
39.
Mheshimiwa Spika, ili kupunguza umaskini kwa watanzania, Serikali ya CCM
inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inalenga kutengeneza ajira kwa
vijana na wanawake zaidi ya milioni 3 katika sekta ya kilimo ifikapo mwaka 2025. Hii itafanyika kwa
kuongeza eneo la umwagiliaji kufikia hekta 8,500,000, sawa na asilimia 50 ya
eneo lote linalolimwa nchini ifikapo 2030. Serikali kupitia Wizara ya Kilimo
itatekeleza Schemes ndogo za umwagiliaji kote nchini. Tunataka vijana
watoke mjini kuelekea kwenye mashamba ya umwagiliaji kwa kujenga miundombinu ya umwagiliaji ikiwemo ujenzi wa mabwawa ya
kuvunia maji ya mvua. Tuna Ziwa
Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na mito mikubwa, kama Malagarasi, Ruvuma,
Rufiji, Mara, Pangani, Ruvu nk, haya maji tutayatumia kwenye skimu za
Umwagiliaji. Kwa ardhi, maji na watu tulio nao, ni jambo la aibu kwa Tanzania
kulia shida ya ngano, shida ya mafuta ya kula kwa sababu ya vita vya Ukraine na
Urusi, sisi tunayo fursa ya kuilisha Afrika, Ulaya na Asia katika baadhi ya
mazao.
40.
Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia
kuongeza idadi ya mashamba makubwa (Block Farms/Commercial Farms) kutoka 110
mwaka 2020 hadi 10,000 mwaka 2030 na kufanya mwelekeo wa uzalishaji wa kilimo
kuwa cha kibiashara. Kwa kilimo cha michikichi,
tuache kung’ang’ania mchikichi mmoja mmoja
kila familia, Mkoa wa Kigoma ndio
kitovu cha Michikichi na upanuzi utafuata mikoa ya Tabora, Katavi, Pwani, Geita
na Kagera. Wakulima wawezeshwe kuunganisha mashamba ili yawe mashamba makubwa
(plantations). Kila mmoja anakuwa mmiliki ili itengenezwe miundombinu ya
pamoja. Hivyo ndivyo tunavyoweza kuitikisa dunia. Kwa alizeti hivyo hivyo. Serikali
inatarajia kufanya tathmini ya kupunguza au kuhamisha mifugo michache iliyopo katika ranchi ya Kongwa ili
hekta karibu elfu 38 zitumike kwa kilimo cha alizeti na kiwanda kikubwa kuliko
vyote Afrika Mashariki. Aidha, eneo la Mtanana ambapo huwa tunasumbuka kuweka
madaraja pale maji yanapokata barabara tuweke Bwawa kubwa ili bonde lote liwe
la “outgrowers” wa alizeti.
41. Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Tanzania
hatujajitosheleza kwa vitu vingi tu ambavyo tuna uwezo wa kuzalisha. Bidhaa nyingi
tunazoagiza kutoka nje tuna uwezo wa kuzizalisha hapa, hizo ni ajira za vijana
wa kitanzania ambazo tumewapa vijana wa mataifa tunakoagiza bidhaa. Serikali
imekusudia kuhakikisha upatikanaji wa malighafi kwenye viwanda vya kuongeza
thamani ya mazao na bidhaa za kilimo kufikia asilimia 100 ifikapo 2030, na
kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kupitia kilimo cha umwagiliaji kutoka
asilimia 10 hadi asilimia 50. Mafuta ya alizeti yale ni mengi tu yakipangwa pembezoni
mwa barabara, machungwa, mananasi, ni mengi tu yakipangwa pembezoni mwa
barabara, ukiweka viwanda vya masaa 24 kwa siku 7, vya kuwafanya vijana wafanye
kazi kwa zamu (shift), viwanda vitawashwa wiki tatu tu, upungufu wote wa
malighafi ni ajira za vijana tunazozikosa.
Sekta ya Mifugo
42. Mheshimiwa Spika, idadi ya mifugo hapa nchini ni
takriban ng’ombe milioni 35.3; mbuzi milioni 25.6; na kondoo milioni 8.8; kuku
milioni 92.8; na nguruwe milioni 3.2. Hata hivyo, mchango wa sekta hii kwenye
fedha za kigeni bado mdogo, na mchango wa kubadilisha maisha ya wafugaji bado
ni mdogo. Licha ya idadi hiyo ya mifugo, viwanda vyetu vilivyopo Rukwa,
Longido, Kibaha, na Mwanza havina malighafi, na wakati huo huo tuna vijana
hawana ajira. Sababu kubwa ni utofauti wa malengo kati ya mfugaji na mwenye
kiwanda. Malengo ya wafugaji wengi tulionao siyo ya kibiashara, anafuga ili
idadi iongezeke, hana mpango na kiwanda. Mheshimiwa Spika, ndugu zangu
wa usukumani hata ng’ombe akivunjika mguu anafungwa POP, hata akiwa na shughuli ya
kifamilia hachinji ng’ombe wa zizini, anakwenda kununua mnadani. Wale wa kwenye
zizi wote wana majina, chitamakuwi,
maagulya, nshoshawiye na majina ya shangazi, mjomba, bibi, hawachinjwi
halafu mwenye kiwanda anaweka kiwanda kutokana na takwimu tu za mifugo katika
mkoa huo.
43.
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mifugo na Uvuvi
imeongezewa ukomo wa bajeti kwa kiasi cha shilingi bilioni 100. Kati ya kiasi
hicho, shilingi bilioni 40 ni za sekta ya mifugo na shilingi bilioni 60 ni za
sekta ya uvuvi. Hivyo, bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeongezeka kutoka
shilingi 168,252,007,000 hadi kufikia shilingi 268,252,007,000. Kati ya fedha
hizo, Shilingi 92,050,824,000 ni kwa ajili ya Sekta ya Mifugo na shilingi
176,201,183,000 ni kwa ajili ya sekta ya uvuvi. Ongezeko hilo la bajeti linalenga kuimarisha sekta ya mifugo
ili ufugaji uwe wa kisasa zaidi na wenye tija (modernization). Katika mwaka
2022/2023, Serikali itaimarisha mashamba ya kuzalisha mitamba ya Sao Hill,
Kitulo na Mabuki kwa kuyapatia ng’ombe wazazi na vitendea kazi,
ikiwemo matrekta matatu (3) na vifaa vyake. Aidha, Serikali itanunua madume ya mbegu 366
kwa ajili ya kuboresha mbari za mifugo; na itazalisha mitamba 3,500 na
kuisambaza kwa wafugaji. Serikali inakusudia kuongeza uzalishaji wa vyakula
ambapo mpaka sasa uzalishaji wa vyakula vya mifugo umeongezeka kutoka tani
1,200,000 mwaka 2020/2021 hadi tani 1,380,000 mwaka 2021/2022.
44. Mheshimiwa Spika, Serikali ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa CCM inakusudia kuanzisha vituo nane (8) vya kukuza
ujuzi wa vijana (Youth Incubation Center) kwa kuanzia na wanufaika takriban 1000 kwa ajili ya vijana watakaofanya kazi ya
kunenepesha ng’ombe na kuuza kwenye viwanda hivi vinavyokosa malighafi. Serikali imepanga kutumia mitambo ya kuchimba
mabwawa kwa ajili ya wafugaji wadogo wadogo. Aidha, napendekeza Wizara
inayohusika na mifugo itunge kanuni za kukusanya na kulinda fedha kwa kila
Wilaya kwa makundi ya mifugo yanayozidi mia moja kwa ajili ya ujenzi wa
miundombinu. Mheshimiwa Spika, Serikali
inaendelea kuhamasisha uwekezaji zaidi katika viwanda vya kuchakata na
kusindika nyama kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi hususani nchi za
Mashariki ya Kati ambapo kwa sasa kuna machinjio na viwanda 24 vinavyokidhi
vigezo vya kuuza nyama nje ya nchi ambapo vitano kati ya hivyo vimeanza kufanya
mauzo nje ya nchi. Viwanda vya kutengeneza bidhaa za ngozi vina uwezo wa
kuzalisha jozi 2,855,600 za viatu kwa mwaka. Kwa upande wa maziwa, idadi ya
viwanda vya kusindika maziwa nchini imeongezeka kutoka 99 mwaka 2020/2021
vilivyosindika lita milioni 75.9 hadi viwanda 105 mwaka 2021/2022
vilivyosindika lita milioni 77.6 ikiwa ni ongezeko la asimilia 2.3
Sekta ya
Uvuvi
45.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021, sekta ya uvuvi
ilikua kwa asilimia 2.5 na ilichangia asilimia 1.8 kwenye Pato la Taifa. Aidha, sekta ya uvuvi inatoa ajira kwa
watanzania takriban milioni 4.5 katika mnyororo mzima wa thamani ambapo ajira
za moja kwa moja kwa wavuvi ni 194,804 na wakuzaji viumbe maji ni 31,998.
Serikali imepanga: Kuanza ujenzi wa bandari ya uvuvi katika eneo la Kilwa
Masoko - Lindi; ununuzi wa meli mbili (2)
za uvuvi katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari; ununuzi wa vifaa vya kuvutia samaki
(Fish Aggregate Device - FADs); ununuzi na usambazaji wa
boti 250 za kisasa za aina ya fibre kwa vyama vya ushirika wa wavuvi;
kuendelea na ufufuaji wa Shirika la Uvuvi Tanzania - TAFICO; kuwajengea uwezo wataalamu wa uvuvi; kuimarisha
Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi - FETA; kuimarisha Taasisi ya Utafiti wa
Uvuvi Tanzania - TAFIRI; kukamilisha ujenzi wa mialo ya kupokelea samaki ya
Igabiro, Mbamba Bay na Chifunfu na kujenga masoko sita (6) ya samaki kwenye
maeneo mbalimbali ya kimkakati; kukarabati kituo cha ulinzi na usimamizi wa
rasilimali za uvuvi cha Bukoba; kununua boti mbili (2) kwa ajili ya utalii wa
baharini; ujenzi na ukarabati wa vituo vya ukuzaji viumbe maji; na kuimarisha
shughuli za ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya sekta ya uvuvi ili kuhakikisha
mradi unatekelezwa kama ulivyopangwa.
Sekta ya Fedha
46.
Mheshimiwa Spika, sekta ya fedha imeendelea kutoa
mikopo kwa wafanyabiashara na uchumi. Pamoja na juhudi hizo, kumekuwepo na wafanyabiashara
wasiolipa mikopo yao kwa wakati na kupelekea kudhoofisha ustawi wa mabenki na
ustawi wa uchumi kwa ujumla. Hadi kufikia Machi 2022, mikopo chechefu ilikuwa asilimia
8.12. Hiki ni kiwango kikubwa sana ikilinganishwa na vigezo vilivyowekwa na Benki
Kuu ya Tanzania. Jambo hili linasababishwa na ukopaji usiozingatia kanuni na
unaohusisha ukosefu wa weledi na uaminifu wa baadhi ya watumishi wa benki.
Unakuta mtu amekopa mabenki zaidi ya matano na kote hajalipa. Akidaiwa anabakia
kuonesha ufundi wa kujificha, baadae akichoka kujificha anakimbilia mahakamani.
Tuache utapeli unatuchafulia nchi na unapozesha uchumi, "Ukikopa
Lipa". Nitoe rai kwa vyombo vya dola na vyombo vya sheria kuwa wakali
kwenye utapeli wa aina hii.
47.
Mheshimiwa Spika, niwapongeze
sana wanawake, taarifa za kitafiti nilizopewa zinaonesha wanawake wengi
wanajitahidi kurejesha mikopo kwa uaminifu. Hata mikopo ya familia kama
imekopwa na wanawake, mingi huwa inafanya kazi iliyokusudiwa na hivyo
inarejeshwa kwa uaminifu kuliko iliyokopwa na wanaume wengi ambao huwa hawarejeshi.
(Niweke sawa, Niliposema wanaume wengi ni ukimwondoa Makamu wa Rais na Waziri
Mkuu). Tujenge utaratibu wa kukopa kwa kuzingatia kanuni, uwezo wa kulipa na
tujenge utaratibu wa kurejesha mikopo kwa uaminifu ili kuimarisha sekta ya
fedha na kukuza uchumi. Kwa upande
mwingine, wako baadhi ya watumishi wa mabenki wasio waaminifu kwa
kushirikikiana na madalali wao wanapenda kutamani dhamana za wateja wao na
kutafuta wateja wa kununua dhamana za wateja wangali wameshalipa zaidi ya
asilimia tisini ya deni. Tena wanauza dhamana kwa kiwango cha chini
ukilinganisha na thamani ya dhamana iliyowekwa. Jambo hili linawatia umaskini
watanzania. Nitoe rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kwa karibu
kila inapofanyika minada kwa madalali wa dhamana na bandarini.
Sekta ya Nishati
48.
Mheshimiwa Spika, mafanikio
tuliyoyapata katika sekta ya nishati ni pamoja na kuendelea kutekeleza: Mradi wa
Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere - MW 2,115 ambapo hadi Aprili 2022 utekelezaji umefikia
asilimia 60.22; miradi ya Kupeleka Umeme Vijijini - REA; mradi wa ujenzi wa
Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (East African Crude Oil Pipeline -
EACOP) kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania; na mradi wa kusindika na
kuongeza kasi ya usambazaji gesi asilia. Aidha, Serikali imeendelea
kuwashirikisha wazawa ambapo shughuli za uendeshaji wa mitambo ya uchakataji,
usafirishaji na usambazaji wa gesi asilia unafanywa na watanzania.
49.
Mheshimiwa Spika, katika sekta ya nishati, Serikali itaendelea
kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji
umeme. Kwa mwaka 2022/23, Serikali
ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM itaendelea
na utekelezaji wa mradi mkubwa wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (National
Grid Stabilization Project) kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa
umeme wa uhakika nchini pamoja
na kutekeleza miradi ya nishati vijijini kupitia Wakala wa
Nishati Vijijini (REA). Miradi
mingine itakayotekelezwa inahusisha Ruhudji (MW 358), Kinyerezi I -
Extension (MW 185), Rusumo (MW 80) na Kikonge (MW 300). Aidha, Serikali
itaendelea kujenga njia za mzunguko pete (ring circuit) ili kuzuia upotevu wa
umeme kwa kuwezesha umeme kupita njia mbadala pale miundombinu inapopata
hitilafu. Miradi ya njia ya umeme wa msongo itakayoendelea kutekelezwa ni
pamoja na kV 400 Rufiji - Chalinze - Dodoma na Chalinze - Kinyerezi; kV 400 Singida - Arusha -
Namanga; kV 400 North - West Grid Extension (Iringa - Mbeya - Sumbawanga - Mpanda
- Kigoma - Nyakanazi); pamoja na kujenga miundombinu ya umeme kwa ajili ya SGR.
50. Mheshimiwa Spika, Serikali
itakamilisha uunganishaji wa mikoa miwili yaani Kigoma na Katavi kwenye Gridi
ya Taifa. Mradi wa Nyakanazi – Kakonko –
Kasulu - Kigoma KV33 unaojengwa na Mkandarasi Sinotech, Mradi wa Nyakanazi -
Kigoma KV 400 Mkandarasi yuko site kwa gharama ya dola za Marekani milioni
168, fedha zipo! Kadhalika mradi wa kufua umeme wa Malagarasi mw 49.5 fedha
tayari zipo kwa ajili ya mradi huo. Serikali itaendelea na miradi mikubwa
miwili pia ya kuunganisha umeme kutokea Sumbawanga – Katavi - Kigoma na ule wa
Tabora – Katavi - Kigoma. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mkoa wa Katavi,
tayari mkandarasi yuko site ukianza na ujenzi wa sub station Ipole
Sikonge, Inyonga wenye thamani ya bilion 124. Napenda niwahakikishie wananchi
wa mikoa hiyo kuwa umeme wa Grid ya Taifa utafika kama alivyoeleza Waziri wa
Nishati. Wabunge wa Kigoma na wabunge wa Katavi mliokuja kuweka kambi Wizara ya
Fedha na Mipango mkifuatilia ahadi ya Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania, mtarudi mikoani kwenu mkiwa mashujaa na mtatembea
kifuambele.
Ujenzi na Uchukuzi
51.
Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango
cha Kimataifa - SGR kwa
kipande cha Dar es Salaam - Morogoro (km 300) umefikia asilimia 96.54; na kipande cha
Morogoro - Makutupora (km 422) asilimia 85.02. Aidha, Serikali imesaini mkataba
wa ujenzi wa SGR kwa kipande cha tatu cha kutoka Makutopora mpaka Tabora (km
368) wenye thamani ya shilingi trilioni 4.4. Serikali iko katika hatua za
mwisho ya kusaini mktaba wa kipande cha Tabora - Isaka (km 163) (dola za
Marekani milioni 695.7). Serikali
imeanza mchakato wa kutafuta mkandarasi kwa kipande cha Tabora - Kigoma km 514
(dola za Marekani bilioni 2.1) na kipande cha Uvinza – Malagarasi – Msongati – Gitega
- Kindu (DRC)
52. Mheshimiwa Spika, Serikali
imekamilisha ujenzi wa
jumla ya kilometa 216.26 za barabara kuu na kilometa 34.8 za barabara za mikoa kwa kiwango cha lami. Aidha, kilometa 307.41 za barabara za mikoa zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Vilevile, Serikali imeanza
ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje - Outer Ring Road (km 112.3)
katika Jiji la Dodoma pamoja na kuendelea na upanuzi wa njia nane wa barabara
ya Kimara - Kibaha (km 19.2). Kadhalika, Serikali imekamilisha ujenzi wa madaraja ya Tanzanite (Dar es Salaam), Kiyegeya (Morogoro),
na Ruhuhu (Ruvuma) na
kuendelea na ujenzi wa madaraja ikijumuisha daraja la J.P Magufuli (Kigongo - Busisi,
Mwanza) ambalo ujenzi umefikia asilimia 40.2, Kitengule, Kagera (asilimia 90)
na Wami, Pwani (asilimia 72.9). Serikali pia imeendelea na
ukarabati wa viwanja vya ndege vya Songea, Mtwara, Iringa, Musoma na Songwe.
53. Mheshimiwa Spika, Serikali ya
CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM itaweka
msisitizo katika ujenzi wa barabara za kufungua fursa za kiuchumi na zile za
kuunganisha Tanzania na nchi jirani kwa utaratibu wa EPC + F ikiwemo (1) barabara
za Kidatu - Ifakara - Lupilo - Malinyi - Londo - Lumecha (Songea), (km 499);
(2) Handeni - Kibirashi - Kibaya - Kwa Mtoro - Singida (km 460); (3) Karatu -
Mbulu - Haydom - Sibiti River - Lalago - Maswa (Simiyu) (km 389); (4) Daraja la Juu la Magomeni-Jangwani-Fire-Bibi
Titi (5) Kibaha - Mlandizi - Chalinze - Morogoro Expressway
(km 158); (6) Igawa - Songwe - Tunduma (Expressway)
(km 218.0), ambazo zitawekewa road toll pamoja na daraja la Tanzanite
kwa kuwa lina sifa zote za kufanya hivyo. Serikali
itamalizia barabara zinazounganisha Mikoa ambayo wakandarasi wako kazini
ikiwepo Tabora - Kigoma na Nyakanazi - Kigoma na kuweka kipaumbele kwenye kujenga barabara
muhimu za kiuchumi kama Barabara ya Makongorosi-Itigi - Mokiwa,
Mafinga-Mtwango-Nyololo - Mgololo, Kahama -Nyang – wale - Geita na nyinginezo.
54.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya
awamu ya sita imeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha bandari ili kurahisisha
shughuli za kiuchumi za usafirishaji kwa njia ya maji na uvuvi katika kina
kirefu cha bahari. Katika kufanikisha hilo, Serikali imendelea na miradi ya
ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya bandari zilizopo katika ukanda
wa Bahari ya Hindi. Miradi hiyo ni pamoja na: kukamilika kwa
ujenzi wa gati maalumu la kuhudumia meli za magari (RoRo), yadi ya kuhudumia makasha
pamoja na kuboresha gati namba 1 - 7
katika Bandari ya Dar es Salaam; kusainiwa kwa mkataba na mkandarasi China Harbour Engineering
Co. Ltd kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya
Uvuvi, Kilwa Masoko - Lindi;
kukamilika kwa ujenzi wa gati moja lenye urefu wa mita 300; kuendelea na ujenzi
wa uzio na sakafu ngumu katika eneo la mita za mraba 75,807 katika Bandari ya Mtwara; na kukamilika kwa
uongezaji wa kina kwenye lango la kuingia meli kutoka mita nne (4) hadi mita 13
pamoja na kuweka vifaa vya kuongoza meli katika Bandari ya Tanga.
Aidha, Serikali inaendelea na majadiliano na wawekezaji watakaowekeza kwenye
Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo hususani katika miradi ya msingi mitatu (3)
ambayo ni: Bandari ya kisasa (Modern Seaport Component); Sehemu ya Kanda Maalum
kwa ajili ya mizigo na usafirishaji (Logistics Park); na Sehemu ya Mji wa
Viwanda (Port side Industrial City).
55. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Serikali ilikamilisha ujenzi wa
chelezo cha kujengea na kukarabati meli katika Bandari ya Mwanza pamoja na
ukarabati wa meli za New Butiama Hapa Kazi Tu na New Victoria Hapa Kazi Tu.
Aidha, serikali imeendelea na ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa kazi Tu
yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo, ambapo ujenzi
umefikia asilimia 66. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Serikali
inatarajia kujenga meli mpya: moja (1) katika Ziwa Victoria; mbili (2) katika
Ziwa Tanganyika; na moja katika Bahari ya Hindi. Aidha, Serikali itaendelea na
ujenzi wa meli ya MV. Mwanza katika ziwa Victoria pamoja na ukarabati wa Meli
za MV Umoja, MT Sangara, MV Liemba - Ukerewe, MT. Nyangumi na boti moja (1) ya mwendokasi (Sea
Warrios) - Ziwa Tanganyika. Aidha, Serikali itafanya ukaguzi wa kina wa
Meli ya MV Mwongozo katika Ziwa Tanganyika pamoja na kuendelea kufungua mifumo
ya TEHAMA katika vituo vya Maziwa makuu (Victoria, Tanganyika na Nyasa).
56. Mheshimiwa Spika, Serikali
inaendelea kutekeleza mpango wa kuboresha Shirika la Ndege Tanzania ambapo
katika kipindi cha mwaka 2021/22 Serikali imepokea ndege tatu (3). Kati ya
hizo, ndege mbili (2) ni aina ya Airbus
A220 300 na ndege moja ni aina ya Dash 8
Q400. Vilevile, Serikali imefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mpya tano
(5) ambazo ni ndege mbili (2) aina ya Boeing 737-9, ndege moja (1) aina ya De
Havilland Dash 8-Q400, ndege moja (1) aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, na ndege
moja (1) ya mizigo aina ya Boeing 767-300F.
57.
Mheshimiwa
Spika, uboreshaji wa viwanja vya
ndege unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kutekeleza hilo,
Serikali imesaini mkataba kwa ajili ya
ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Msalato awamu ya kwanza itakayohusisha ujenzi wa njia ya kuruka na kutua
ndege pamoja na jengo la abiria. Aidha, Serikali imekamilisha upanuzi wa njia
ya kutua na kuruka ndege na kufungwa kwa mfumo wa kuongoza ndege katika Kiwanja
cha Ndege cha Dodoma; pamoja na usanifu na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa
jengo la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza. Viwanja vinavyoendelea
kufanyiwa ukarabati na ujenzi ni viwanja vya ndege vya Songea (asilimia 96),
Mtwara (asilimia 89), Iringa (asilimia 44.65), Songwe (asilimia 95) na Musoma
(asilimia 10). Vilevile, Serikali inaendelea kufanya maandalizi ya ujenzi na
upanuzi wa viwanja vya ndege vya Shinyanga, Kigoma,
Tabora na Sumbawanga vitakavyogharimu Euro milioni 50 sawa na shilingi
bilioni 136.85.
Elimu, Sayansi na Teknolojia
58.
Mheshimiwa Spika, Serikali imewezesha ujenzi wa madarasa 15,000 katika shule za
sekondari na vituo shikizi na mabweni 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
maalum. Ujenzi wa
miundombinu hii umewezesha wanafunzi wote 907,803 waliofaulu mtihani wa darasa
la saba mwaka 2021 kupata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza Januari 2022 bila
kusubiri chaguo la pili. Kadhalika, Serikali imekamilisha maboma 560 ya vyumba
vya madarasa katika shule za sekondari kutokana na tozo za miamala ya simu
ambapo shilingi bilioni 7.0 zilitolewa; Aidha, Serikali imetoa mikopo yenye
thamani ya shilingi bilioni 569 kwa wanafunzi 177,777 wa elimu ya juu.
59. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23 Serikali itaenda kutekeleza
mradi wa “Higher Education for Economic
Transformation” (HEET) wenye thamani ya dola za Marekani milioni 425. Mradi
huu utahusisha ujenzi wa miundombinu katika vyuo vikuu mama na katika mikoa
kadhaa ambayo haina vyuo vikuu ikiwemo Lindi, Kagera, Rukwa, Katavi, Manyara na
kukamilisha ujenzi wa Institute of Marine
Science Zanzibar na kujenga chuo kipya cha TEHAMA Dodoma.
60.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kugharamia programu ya elimumsingi bila
ada ambapo hadi Aprili 2022, jumla ya shilingi bilioni 244.5 zilitolewa. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais
wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameguswa sana na watoto
kukatisha masomo kwa ajili ya sababu mbalimbali. Miongoni mwa sababu
zinazosababisha kukatisha masomo ni umaskini wa kipato kwenye familia zetu,
mimba za utotoni, mwamko duni wa elimu kwa baadhi ya jamii na utoro na wale
wasioendelea kufuatana kwa mujibu wa sheria (Ufaulu). Ili
kukabiliana na utoro (drop out) wa
wanafunzi wanaotoka familia maskini, bado tuna watoto wanaoshindwa kumudu
mahitaji ya lazima licha ya kuwepo kwa programu ya elimu bila malipo na hivyo wanasaidiwa na wabunge, madiwani na
wengine kuchangiwa na wasamaria wema. Napendekeza
kuanzisha dirisha maalum (Special Fund)
kupitia TASAF itakayosaidia watoto wanaotokea familia maskini. Kwa msingi
huo napendekeza kuanza na bilion 8 kwa ajili ya watoto masikini watakaopatikana
kwenye database ya TASAF na taarifa za wabunge na madiwani.
61.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na mimba za utotoni, Serikali itaendelea
kujenga mabweni kwenye maeneo hatari kwa watoto wa kike. Aidha, ili kutoa fursa
kwa watoto wasioendelea na vidato na vyuo, Serikali itaendelea kuimarisha elimu
ya ufundi hususan katika vyuo vya kati kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiajiri
ama kuajiriwa. Mpaka sasa Wilaya 77 zina vyuo vya Ufundi VETA kati ya Wilaya
138 nchini kote. Tuna mikoa 25 ina Vyuo vya Ufundi kati ya mikoa 26. Bado mkoa
wa Songwe hauna kabisa Chuo cha VETA na
wabunge wa mkoa wa Songwe wamekuwa wakishinda Ofisini wakifuatilia ahadi
waliopewa na Mheshimiwa Rais. Bado kuna wilaya 36 ambazo hazina vyuo wala vyuo vya Mkoa.
Napendekeza kutoa bilioni 100 kwa ajili ya ujezi wa vyuo vya ufundi kwa Mkoa wa
Songwe na wilaya 36 ambazo hazina vyuo ili kufanya wilaya zote 138 kuwa na chuo
cha Ufundi (VETA). Waheshimiwa wabunge, Huyo ndio SAMIA.
62.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takriban 90,825 na
kidato cha sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi 10,339,350,000. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza Wizara, napendekeza kufuta ADA kwa wanafunzi wa
kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za
msingi mpaka kidato cha sita. Serikali itajipanga kuangalia namna ya
kusaidia vyuo vya kati kadiri hali
ya uchumi itakavyotengemaa. Nani kama SAMIA? Nani kama Mama? Nani kama CCM? CCM
ni Na. 1.
Sekta ya Afya
63.
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2021/22, Serikali imewezesha ujenzi,
upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya afya ikiwemo: majengo 66 ya wagonjwa
mahututi - ICUs; majengo 100 ya dharura - EMDs; nyumba 150 kwa ajili ya
watumishi wa Afya; Hospitali za Rufaa za Mikoa 7 na hospitali maalum 1
(Mirembe); na vituo vya Afya 304 ili kuboresha huduma ya mama na mtoto. Aidha,
Serikali imetoa ruzuku ya shilingi
bilioni 23.32 kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kukamilisha ujenzi wa
maboma 564 ya zahanati. Serikali pia imeendelea na ujenzi wa hospitali 99 na
kuanza ujenzi wa hospitali mpya 28. Vilevile, Serikali imewezesha ujenzi wa
vituo vya afya 234 kwa kutumia tozo ya miamala ya simu yenye thamani ya
shilingi bilioni 86.0.
64. Mheshimiwa
Spika, Serikali inaendelea kuimarisha
huduma za afya kwa kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa ambapo hadi sasa
katika hospitali zetu mbalimbali kuna jumla ya mashine 11 za CT scan,
mashine 7 za MRI na mashine 105 za digital X Ray zinazofanya kazi. Kati ya hizo, mashine 42 za digital X Ray
zipo katika hospitali za ngazi ya taifa, kanda na maalumu na rufaa za mikoa na
mashine 63 zipo katika hospitali zilizo chini ya OR-TAMISEMI. Serikali itaendelea kutoa kipaumbele katika
eneo hili ambapo ununuzi zaidi wa vifaa vya uchunguzi wa magonjwa umekamilika
na vifaa hivyo vitasimikwa katika hospitali na taasisi zetu mbalimbali. Vifaa ambavyo vimeshaagizwa ni pamoja na, MRI 4; CT “Scan 31; Digital
X Rays” 130; mini angio suite moja na “Echo Cardiography” 7.
Aidha, Serikali inaendelea na usimikaji wa vinu ya kuzalisha na kujaza hewa
tiba ya oksijeni ambapo hadi sasa vinu 13 vimesimikwa katika hospitali zetu
mbalimbali na hivyo kusogeza huduma za kitabibu kwa wananchi.
65. Mheshimiwa
Spika, Serikali
ya CCM inayoongozwa na Mheshimiwa Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM itaendelea
kuboresha sekta ya afya kwa kujenga, kukarabati na kupanua miundombinu ya
kutolea huduma za afya ikiwemo: Ujenzi wa Hospitali Maalum ya Mama na Mtoto
Jijini Dodoma; kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi;
kukamilisha ujenzi wa Hospitali (5) za Rufaa za Mikoa katika Mikoa mipya ya
Katavi, Geita, Njombe, Songwe na Simiyu; na kukamilisha upanuzi wa hospitali
nane (8) za Rufaa za Mikoa. Aidha, Serikali itaendelea kuboresha huduma za
matibabu ya ubingwa bobezi katika Hospitali ya Taifa na Kanda kwa kuimarisha
miundombinu na ununuzi wa vifaa na vifaa tiba katika Taasisi ya JKCI, Hospitali
za Rufaa za Kanda za Chato, Mtwara, KCMC, Bugando na Mbeya.
Sekta ya Maji
66.
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa
Rais wetu amewezesha kukamilika kwa miradi 303 ya maji vijijini na miradi 40
mijini ikiwemo miradi mikubwa ya Misungwi, Orkesumet, Chalinze-Mboga na
Longido; kuongezeka
kwa kiwango cha upatikanaji wa huduma za maji nchini kutoka asilimia 72.3
vijijini na 86 mijini mwaka 2020/21 hadi asilimia 74.5 vijijini na 86.5 mijini; kuimarika kwa usimamizi wa rasilimali ya maji kwa kuendelea
kutambua, kuweka mipaka na kuhifadhi vyanzo 178 vya maji pamoja na kuandaliwa
kwa mipango ya utunzaji wa maeneo ya vidakio vya maji katika mabonde yote
nchini.
67.
Mheshimiwa
Spika, Serikali pia
imekamilisha taratibu za ununuzi wa seti 25 za mitambo ya kuchimba visima
ambayo itasambazwa kwa kila mkoa isipokuwa Dar es Salaam; seti 5 za mitambo ya
ujenzi wa mabwawa ambazo zitapelekwa kwenye kila kanda; na seti 4 za vifaa vya
utafiti wa maji chini ya ardhi. Mitambo hii inatarajiwa kupokelewa mwishoni mwa
mwezi Juni, 2022. Aidha, mnamo tarehe 6 Juni 2022, Serikali ilisaini mikataba
ya kusambaza maji kwa miji 28, ambazo ni fedha za mkopo wenye thamani ya dola
za Marekani milioni 500 kutoka Exim bank - India. Kati ya fedha hizi, dola
milioni 35 zitatekeleza miradi ya maji Zanzibar.
Sekta ya Mali Asili na Utalii
68.
Mheshimiwa Spika, Aprili mwaka huu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alizindua filamu ya “The
Royal Tour” ambayo
imelenga kuonesha uwezo na fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya utalii na
uwekezaji. Hivyo, kupitia Bunge hili, napenda kuendelea kuwakaribisha diaspora
wa Tanzania na wawekezaji kutoka kona zote za dunia kuja kutalii na kuwekeza
katika fursa za uwekezaji zilizopo nchini kwani Tanzania tuna “JAMBO LETU”
kwenye kuinawirisha sekta binafsi katika uwekezaji. Tumejipanga na kujizatiti
kuifanya Tanzania kuwa “KITOVU na MFANO” wa sehemu ya uwekezaji salama, haraka,
rahisi, wenye tija na manufaa kwa pande zote. Kufuatia ziara hiyo kwenye kanda
za utalii Tanzania, tayari booking zimejaa mpaka Desemba 2022 kwenye
maeneo mengi. Naomba kutoa wito kwa wawekezaji wote kuwa, Tanzania
kumenoga, milango iko wazi, njooni muwekeze kwa maslahi mapana ya pande zote.
Sekta ya Madini
69. Mheshimiwa Spika, chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, mchango wa
sekta ya madini umeongezeka kutoka asilimia 6.7 mwaka 2020 hadi asilimia 7.2
mwaka 2021 ambapo ukuaji huu uliifanya sekta hii kushika nafasi ya tano
miongoni mwa sekta nyingine za kiuchumi nchini. Aidha, kasi ya kukua kwa
shughuli za madini hapa nchini imekuwa ikiendelea kuongezeka ambapo katika
mwaka 2021, sekta ya madini ilikua kwa asilimia 9.6 ikilinganishwa na ukuaji wa
asilimia 6.7 mwaka 2020, na hivyo kuwa ya tatu miongoni mwa sekta nyingine kwa
kiwango cha ukuaji katika kipindi hicho. Mwenendo huu wa ukuaji wa sekta
umetokana na ongezeko la uwekezaji uliofanyika kupitia uchimbaji mkubwa, wa
kati na mdogo nchini. Lengo la Serikali ni kuona sekta ya madini inachangia
asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa katika Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025.
70. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa
wachimbaji wadogo kushiriki uchumi wa madini, Serikali imezihamasisha taasisi
za fedha na benki nchini kutoa mikopo kwa wachimbaji hao ili kuwawezesha kukua
na kufanya uchimbaji wenye tija. Baadhi ya benki ikiwemo NMB, NBC, CRDB na KCB
zimeridhia na kuanza kutoa mikopo ambapo jumla ya shilingi bilioni 36
zimekopeshwa kwa wachimbaji hao. Hizi ni miongoni mwa juhudi ambazo Serikali
imezifanya ili kuhakikisha wachimbaji wadogo wanakua na kufikia hadhi ya kiwango cha kati na hatimaye
wakubwa, wanashiriki uchumi wa madini na kuchangia katika Pato la Taifa. Aidha,
kufuatia Serikali kuendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo, mchango wao katika
maduhuli ya Serikali umeongezeka hadi kufikia takriban asilimia 40 ya maduhuli
yote. Kutokana na mchango wao, Serikali itaendelea kuwawezesha ili waendelee
kuchangia zaidi katika uchumi wa Taifa.
71. Mheshimiwa Spika, Serikali
kupitia Taasisi ya Jiolojia Tanzania - GST imeweza kufanikisha ugani wa
jiolojia kwa asilimia 96 ya nchi nzima, ugani wa jiofizikia kwa skeli ndogo
(Low Resolution) asilimia 100 na skeli kubwa (High Resolution) asilimia 16 na
ugani wa jiokemia asilimia 25 ya nchi nzima. Kupitia tafiti hizo Serikali
imefanikiwa kugundua maeneo mapya yenye rasilimali madini na kuyatangaza kwa
lengo la kuvutia uwekezaji mkubwa. Baadhi ya rasilimali zilizogunduliwa katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita ni pamoja na dhahabu (Malinyi - Morogoro na
Liwale - Lindi), gesi ya helium (Masware - Babati na Ziwa Natroni - Arusha),
chokaa na feldispa (Kiteto - manyara), chokaa (Mkalama - Singida).
72.
Mheshimiwa Spika, migodi
mikubwa iliyopo kama GGML, Bulyanhulu North Mara na mgodi mpya wa Kabanga
Nikeli na Nyanzaga imetokana na taarifa za awali za jiolojia zilizofanywa na GST
miaka ya nyuma. Kutokana na mafanikio hayo, Serikali itaendelea kuiwezesha GST
ili iweze kufanya utafiti zaidi wa jiofizikia kwa skeli kubwa (High
Resolution) kwa lengo la kufikia asilimia 65 kutoka asilimia 16 iliyopo
sasa. Manufaa yanayotarajiwa ni pamoja na; Uwezekano wa kuanzishwa kwa migodi
mipya ambayo itachangia Pato la Taifa kupitia sekta ya madini; ukuaji wa sekta
mtambuka ambazo hutegemea sana sekta ya madini kama vile kilimo, ujenzi na
maji; uanzishwaji wa viwanda vinavyotegemea upatikanaji wa malighafi za madini
kama vile viwanda vya saruji, mbolea na marumaru; na kuongezeka kwa ufahamu
zaidi wa jiolojia ya nchi na hivyo kuchochea shughuli za utafiti na uchimbaji
wa madini ambao utachangia katika maendeleo ya Taifa.
73.
Mheshimiwa
Spika, kila mtanzania mwenye umri wa
zaidi ya miaka 18 na mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi. Ili kutimiza amza
hiyo, Serikali inakusudia kutoa namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) kwa
kila mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi. Kwa kuwa utaratibu wa
usajili wa namba ya utambulisho wa Taifa (NIDA) unamtaka kila mwananchi mwenye
umri wa miaka 18 au zaidi kujisajili NIDA, napendekeza kuwa wale wote wenye
NIDA kwa sasa (wanaofikia milioni 19 nchi nzima) wapatiwe namba ya TIN na
itumike kwenye miamala yote inayofanyika katika ununuzi na mauzo yanayofanyika
ndani ya nchi. Kila mwenye namba ya mlipakodi atapata makadirio yake kwa njia
ya simu na kulipa kodi husika kwa njia ya mtandao.
74. Mheshimiwa Spika,
vijana wetu wa bodaboda wanapata shida kufuata leseni yalipo makao makuu ya
mkoa, yaani mtu atoke Mererani kwenda Babati makao mkuu ya mkoa wa Manyara,
atoke Kakonko kufuata leseni Kigoma, atoke Wilaya ya mwisho kule mpakani na
Lindi, Mtwara na Ruvuma kufuata leseni Morogoro ili hali taarifa zake zote ziko
kwenye kitambulisho cha NIDA. Napendekeza taarifa zilizopo kwenye kitambulisho
zitumike kutengeneza leseni, akishakufuzu ajiandikishe atoe namba yake ya NIDA,
TRA na Jeshi la Polisi wafanye kazi ya kuoanisha taarifa na wamtumie mhusika
leseni yake kwa simu. Aidha, napendekeza wananchi wote wenye namba ya
utambulisho wa mlipakodi (TIN) wapeleke ritani za kodi Mamlaka ya Mapato
Tanzania kwa mwaka mara moja. Utaratibu huu utachachua utamaduni wa kulipa kodi
miongoni mwa Watanzania na hivyo kuiongezea Serikali mapato yatokanayo na sekta
ambazo hazichangii kwenye makusanyo ya Serikali kwa sasa licha ya kuwa na
mchango mkubwa kwenye Pato la Taifa kama vile sekta za mifugo, kilimo, uvuvi na
nyinginezo.
Bunge
75.
Mheshimiwa Spika,
Serikali inatambua uzito wa majukumu ya Bunge na hivyo itaendelea kuhakikisha
kwamba Bunge linawezeshwa kifedha na kujengewa uwezo ili kuongeza ufanisi
katika utekelezaji wa majukumu yake ya msingi ya kutunga sheria, kushauri na
kusimamia Serikali. Kwa kulitambua hilo, katika mwaka wa fedha 2022/23, Bunge
limeongezewa kiasi cha shilingi bilioni 5 kwa ajili ya matumizi mengineyo ili
kuwezesha utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo kuwajengea uwezo wabunge ili waweze
kuisimamia vizuri Serikali. Serikali pia imeongeza bajeti ya mfuko wa Jimbo ili
kuwawezesha wabunge kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kuchochea maendeleo
katika majimbo yao. Serikali itahakikisha kuwa fedha kwa ajili ya shughuli
za Bunge zinatolewa kwa wakati. Aidha, Serikali itaendelea kutoa ushirikiano
kwa Bunge lako Tukufu kwa kulipatia taarifa zote muhimu zinazohitajika na kwa
wakati ikiwepo taarifa za kila robo mwaka za kitengo cha Tathmini na
Ufuatiliaji ili ziwasaidie wabunge wanapofanya ziara za kukagua miradi kama
nilivyopendekeza awali.
Utawala Bora
76.
Mheshimiwa Spika, kwa
upande wa mahakama, Serikali itaendelea kuimarisha usimamizi wa mifumo ya haki
na utoaji haki kwa kuendelea kuwezesha mhimili wa Mahakama kuongeza kasi ya
kusikiliza mashauri na hivyo kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani.
Aidha, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya utoaji haki kupitia ujenzi
na ukarabati wa miundombinu ya mahakama ikiwa ni pamoja na kuimarisha matumizi
ya TEHAMA hususan mfumo wa mkutano mtandao na mfumo wa kielektroniki wa
usimamizi na uendeshaji wa mashauri. Utekelezaji wa masuala haya unalenga
kuboresha ufanisi wa mahakama na kufanya usimamizi wa mahakama kuwa wa kisasa
zaidi na hivyo kuwawezesha wananchi kupata haki sawa na kwa wakati.
77. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2022/23, Serikali
itaendelea kugharamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali zinazolenga katika utoaji haki kwa wananchi na
kupambana na rushwa. Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa vituo
jumuishi vya utoaji haki na kutafsiri sheria ambapo kiasi cha shilingi bilioni
5.7 zimeongezwa kwenye bajeti ya awali.
Aidha, Serikali imeongeza kiasi cha shilingi bilioni 20 kwenye bajeti ya
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kwa ajili kugharamia mashahidi wa
makosa ya jinai na ujenzi wa vituo jumuishi vya utoaji haki.
Ulinzi na Usalama
78. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2021/22, Serikali
kupitia majeshi yetu imeendelea kudumisha amani na usalama nchini na hivyo
kuwezesha watanzania kutembea kifua mbele na kutekeleza shughuli mbalimbali za
kijamii na kiuchumi bila wasiwasi. Aidha, Serikali imeendelea kuimarisha
ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi na nchi mbalimbali na tunaamini kuwa vyombo
vyetu vya ulinzi na usalama vitaendelea kutimiza wajibu wake wa kulinda mipaka
na amani ya nchi yetu kwa moyo wa kizalendo na hivyo kuzidi kuimarisha
mazingira ya amani na utulivu ya kuvutia biashara na uwekezaji. Katika mwaka
2022/23, Serikali itaendelea kuviimarisha na kuvijengea uwezo vyombo vya ulinzi
na usalama ili kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa weledi na uzalendo.
79.
Mheshimiwa Spika, sambamba
na zoezi la anuani za makazi linaloendelea, Serikali itaimarisha shughuli za
usalama ngazi ya kaya ili kujidhatiti na aina mpya ya uhalifu ambao tumeusikia
kwa baadhi ya majirani zetu. Utaratibu huo ni pamoja na kuhakikisha viongozi wa
mitaa na shehia wanahusika kwenye upangishaji wa nyumba za kuishi ili kila
nyumba ya kupanga itumie mkataba wa Serikali ya vijiji/mitaa uliopigwa muhuri
wa ofisi ya vijiji/mitaa husika. Kadhalika, mauziano ya mali zisizohamishika
lazima zihusishe uongozi wa Serikali husika hata kama wahusika wana mawakili
binafsi ila viongozi wa serikali za vijiji/mitaa wawe na taarifa za mambo
yanayoendelea katika maeneo yao.
Uhusiano wetu na Washirika wa Maendeleo
80.
Mheshimiwa Spika, jitihada za kuimarisha ushirikiano na Washirika wa Maendeleo
pamoja na mataifa mbalimbali duniani zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, zimewezesha kusainiwa kwa
mikataba ya misaada na mikopo mbalimbali. Baadhi ya mikataba ya miradi
iliyosainiwa ni pamoja na: Uboreshaji wa
Umiliki wa Ardhi; kuboresha Elimu ya Msingi; na mradi wa Maboresho ya Mahakama
ili kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi. Aidha, baadhi ya mikataba
ya miradi inayotarajiwa kusainiwa ni pamoja na: Mradi wa Kufungamanisha
Uchukuzi ambao una lengo la kuboresha na kuunganisha njia kuu za barabara na
viwanja vya ndege vya mikoa (TanTIP); na Mpango Kabambe wa Kuboresha na Kuimarisha
Takwimu - TSMP II.
81. Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha majadiliano ya upatikanaji wa
mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia wenye thamani ya dola za Marekani milioni
500, sawa na shilingi bilioni 1,167. Aidha, Serikali imefikia makubaliano ya
kupata mkopo nafuu wenye thamani ya shilingi bilioni 2,567, sawa na dola za
Marekani bilioni 1.1 kupitia dirisha la Extended Credit Facility (ECF)
chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa - IMF. Mkopo huo wa IMF utatolewa kwa
awamu saba katika kipindi cha miezi 40 kuanzia Julai 2022 hadi Julai 2025. Fedha hizo
zitaelekezwa katika kuimarisha sekta za uzalishaji, huduma za jamii pamoja na
kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji na kuinua sekta
zilizoathiriwa na vita ya Ukraine na Urusi.
Maslahi ya Watumishi wa Umma na Wastaafu
82. Mheshimiwa Spika,
tuzo ya watumishi wachapakazi na wazalendo ni ipi? Matunda ya utumishi wa kujitoa
na uadilifu wa watumishi hao ni yapi? Lakini Je, ni nani wa kuyatambua na
kuyapa thamani halisi mambo hayo? Sauti zenye maswali haya zilitawala masikio
ya Mheshimiwa Mama yetu mwenye usikivu, unyenyekevu na anayejali, na hatimaye
maswali haya yamejibiwa na kalamu yenye mamlaka ya Mheshimiwa Rais wetu kwa
kuridhia nyongeza ya kima cha chini cha mshahara
kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma. Kwa kuendelea kuonesha kujali na
kuthamini utumishi wa umma, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya
Mungano wa Tanzania na Mwenyekiti
wa CCM amefanya maboresho kwenye viwango vya posho. Aaminie katika wema na kujali, hutenda na kuuishi wema. Hivyo,
Mheshimiwa Rais wetu ni mfano sahihi wa maneno haya katika jambo hili.
Watumishi wa Umma wanauliza Nani kama Mama Samia? na wanasema Asante sana Mama!
83. Mheshimiwa Spika,
Serikali itaendelea na jitihada za kulipa madai ya Watumishi wa Umma pamoja na
kupandisha madaraja watumishi wanaostahili. Tutaendelea kuboresha mazingira ya
kazi na maslahi yao kadri uchumi wa nchi utakavyoruhusu bila kuathiri makundi
mengine ya wananchi, huduma mbalimbali pamoja na utekelezaji wa miradi ya
maendeleo. Katika kuhakikisha maslahi ya wastaafu wetu waliotumikia Taifa hili
kwa uzalendo, uadilifu na bidii kubwa wananufaika na michango waliyochangia
katika mifuko ya hifadhi ya jamii, Serikali sikivu ya Mama yetu imeridhia
kuongeza malipo ya mkupuo kwa wastaafu kufikia asilimia 33 badala ya asilimia
25 iliyopendekezwa mwaka 2018.
84. Mheshimiwa Spika,
Serikali itaendelea na mikakati mbalimbali ya kulipa madeni ya mifuko ya
hifadhi ya jamii. Katika mwaka 2021/22, Serikali ilitoa hatifungani maalumu
yenye thamani ya shilingi trilioni 2.18 kwa ajili ya kulipa deni la Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma - PSSSF linalohusu michango ya watumishi
waliokuwa kwenye utumishi kabla ya mwaka 1999. Mwaka 2022/23, Serikali
itaendelea na uhakiki wa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii na kulipa deni
stahiki. Lengo ni kuhakikisha watumishi wanalipwa kwa wakati mafao yao mara
baada ya kustaafu pamoja na pensheni zao za kila mwezi.
Mazingira
ya Biashara ndogo na Sekta Binafsi
85.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha azma ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya kuwapanga, kuwasimamia,
kuwalinda na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo inafikiwa, Serikali itaendelea
na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wajasiriamali hao wadogo wanaboreshewa
mazingira ya kufanyia biashara. Aidha, Serikali itaendelea kuwatambua na kuwaunganisha na Taasisi za fedha ili waweze
kupata mikopo nafuu. Vilevile, Serikali itaendelea kutenga maeneo na ujenzi wa
miundombinu kwa ajili ya wajasiriamali wadogo. Katika kuhakikisha utatuzi wa
changamoto za machinga unakuwa shirikishi, Mheshimiwa Rais ameahidi kutoa
shilingi milioni 10 kila mkoa kwa ajili ya kuimarisha uongozi wa machinga
pamoja na ujenzi wa ofisi za machinga. Aidha, napendekeza kufanya mgao mpya wa
mapato ya ndani ya halmashauri kama ifuatavyo: Asilimia 10 ya mapato ya vyanzo
vya Halmashauri, napendekeza asilimia 5 iwe kwa ajili ya miundombinu na
masoko ya machinga; asilimia 2 kwa vijana; asilimia 2 wanawake; na asilimia 1
kwa wenye ulemavu. Aidha, Serikali imetenga shilingi bilioni 45 kwa ajili ya
kuendelea na ujenzi wa miundombinu na mtaji kwa machinga ambapo kila mkoa,
machinga walioko kwenye maeneo yaliopangwa wawe na revolving fund
ya shilingi bilioni 1 kwa utaratibu utakaowekwa .
86. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza jitihada za kurasimisha sekta isiyo
rasmi ili inufaike na kuwa sekta rasmi, Serikali imepanga kuweka mazingira
rafiki ya kisheria na kikanuni katika usajili na uendeshaji wa biashara,
kuharakisha usajili wa biashara kwa kuhakikisha usajili unakamilika ndani ya
siku moja iwapo muombaji amekidhi masharti yanayohitajika, kuongeza upatikanaji
wa mikopo kwa biashara zinazorasimishwa, kuongeza upatikanaji wa huduma kama
miundominu ya biashara, mafunzo teknolojia na masoko. Vilevile, Serikali
imepanga kuongeza vituo atamizi vya kukuza
biashara na maeneo maalumu ya viwanda.
87.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua
mchango wa sekta binafsi katika uwekezaji, Serikali imeendelea kuboresha
mazingira ya uwekezaji na biashara nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa
Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini ili sekta binafsi iweze kushiriki
kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi. Mwaka 2021/22, Serikali kwa
kushirikiana na sekta binafsi ilishiriki majadiliano ya kutatua changamoto
zinazoikabili sekta hiyo katika kufanya biashara katika masoko ya nchi
mbalimbali ikiwemo Kenya ambapo vikwazo visivyo vya kikodi 42 kati ya 64
vimepatiwa ufumbuzi. Hali hiyo
iliwezesha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Kenya. Aidha,
kupitia Sheria ya Fedha 2022/23, Serikali inapendekeza kufanya maboresho ya
jumla ya maeneo 19 ya sheria mbalimbali ili kuboresha zaidi mazingira ya
biashara na uwekezaji kama nitakavyoeleza baadae.
88.
Mheshimiwa Spika, Serikali
imeendelea kuratibu ushiriki wa watanzania katika miradi ya kimkakati na
uwekezaji unaofanyika hapa nchini (Local
Content) ambapo jumla ya ajira 72,395 za moja kwa moja na zisizo za moja
kwa moja zilizalishwa katika mwaka 2021. Vilevile, miradi ya kimkakati ilitoa
kandarasi ndogo ndogo kwa kuingia mikataba na kampuni 2,019 za watanzania kwa
huduma za chakula, ulinzi, biashara, bidhaa za ujenzi kama vile saruji, nondo,
kokoto, mchanga, kampuni za usafiri, kampuni za bima na kampuni za mafuta.
Kadhalika, Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa na mikataba ya
uwekezaji inasomana na sheria za kodi kwa ajili ya kutatua changamoto ya
kutotekelezeka kwa baadhi ya miradi ya uwekezaji kutokana na kukinzana na
sheria za kodi.
Ubia wa Sekta
ya Umma na Sekta Binafsi (PPP)
89.
Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa miradi ya PPP, jumla ya miradi mitano (5) ipo
katika hatua ya ununuzi wa mbia. Aidha, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu
kuwa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Kwanza umepata mbia wa uendeshaji
ambapo hatua inayofuata ni majadiliano na mbia husika. Hatua hii itaongeza
ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma na mradi huu utakuwa mradi wa
kielelezo uliopitia hatua zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya PPP, Sura
103. Upatikanaji wa wabia katika miradi ya PPP utaleta ahueni katika bajeti ya
Serikali na hivyo kuwezesha kuongeza rasilimali fedha katika maeneo mengine na
hivyo kuwaletea maendeleo watanzania. Serikali itaendelea kufanya tathmini ili
kuboresha na kuipa nafasi sekta binafsi kushiriki katika kutekeleza miradi ya
Serikali kwa mfumo wa Ubia na hivyo Serikali kujikita zaidi katika kuweka
mazingira wezeshi na kuboresha huduma za kijamii.
90.
Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na
mazingira wezeshi ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, Serikali itaendelea
kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara kwa kuimarisha miundombinu
wezeshi ya usafirishaji na nishati; kuhakikisha uhimilivu wa viashiria vya
uchumi jumla; na kuwianisha tozo na ada mbalimbali zinazotozwa na Wizara na
Mamlaka za Udhibiti kwa lengo la kupunguza na kurahisisha ulipaji wake na
kuzifuta baadhi ya tozo na ada za kero. Aidha, mwaka 2022/23, Serikali itaendelea kufanya marekebisho ya viwango vya
kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya sheria mbalimbali. Marekebisho hayo
yanalenga kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi, hususan katika sekta ya viwanda,
uwekezaji na biashara pamoja na kuongeza ajira, mauzo nje, mapato na akiba ya
fedha za kigeni. Vilevile, katika kuepusha malimbikizo ya marejesho ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani - VAT na kupunguza mzigo wa madai ya fedha kutokana na
ucheleweshaji wa marejesho kwa sekta binafsi, Serikali itaanza mchakato wa
kuhakiki marejesho ya VAT kwa njia ya kielektroniki kuanzia mwaka 2022/23.
Sensa ya Watu
na Makazi
91. Mheshimiwa Spika, kipaumbele kingine katika bajeti ya mwaka 2022/23 ni
ugharamiaji wa Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti 2022. Ili kuwezesha zoezi hili muhimu, Serikali imetenga
jumla ya shilingi bilioni 400.9. Aidha, napenda kutumia nafasi hii kupitia
Bunge lako Tukufu kuhimiza wananchi wote kutoa ushirikiano siku hiyo hasa
ukizingatia zoezi hili ni jukumu la kila mtu. Ushiriki wetu utaiwezesha
Serikali, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na sekta binafsi kupata takwimu sahihi
zitazokuwa msingi wa kuandaa, kutekeleza na kutathmini sera na mipango
mbalimbali ya maendeleo katika nchi yetu.
Lugha ya Kiswahili
92.
Mheshimiwa Spika, lugha ya kiswahili ndio lugha ya
Taifa, ndio lugha ya ofisini, ndio lugha ya pili kwa watoto wa vijijini na
lugha ya kwanza kwa watoto waliowengi wa sasa, ndio lugha ya msingi, ni lugha
ya Bunge, na nikiwa Waziri wa Katiba na Sheria nilileta mapendekezo kuifanya
kuwa lugha ya Mahakama na lugha ya hukumu. Aidha, Kiswahili ni lugha ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo tumeipeleka wenyewe, ikiwa ni pamoja na
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) na Umoja wa Afrika (AU). Vilevile, UNESCO wameitambua na watakuwa
wanaiadhimisha tarehe 7 Julai kila mwaka. Hii ndiyo lugha yetu, kwa nini usaili
wa mtoto wa kitanzania anapotafuta kazi unafanyika kwa lugha ya Kingereza?
Yaani afisa kilimo, afisa mifugo, mtumishi wa Serikali anakazi ya kuhudumia
watanzania tunapima akili zake kwa kupima kingereza chake kwa ajili ya nini?
Napendekeza saili zote zifanyike kwa Kiswahili, na kumbi zote za mikutano na
ofisi za Serikali ziwe na vifaa vya kutafsiria lugha za kigeni na watafsiri ili
tuweze kuienzi lugha yetu ya Taifa.
Sekta ya Michezo
93.
Mheshimiwa Spika, Serikali
itarejesha bahati nasibu ya taifa kwa utaratibu wa kutumia Sekta Binafsi.
Sambamba na hiyo Serikali kupitia Bodi
ya Michezo ya kubahatisha, TRA na Sekta Binafsi wataanza kuendesha bahati
nasibu kwa kupitia risiti za EFD ili kuchochea wananchi kudai risiti
wanaponunua bidhaa. Aidha, Serikali itatumia sehemu ya Mchango wa Wajibu wa
Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibity) kwa kiwango kisichozidi
asilimia 2 kwa ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha ili
kuendeleza michezo nchini ambapo makampuni yataruhusiwa kukitambua kiasi hicho
kwenye mapato yanayostahili kutozwa kodi. Nitumie nafasi hii kuwahakikishia
watanzania kuwa tutaweka nyasi bandia kwenye viwanja vitano kwa kuanzia Mwanza,
Arusha, Tanga, Dodoma na Mbeya ili kukuza mchezo hapa nchini. Katika mwaka wa
fedha wa 2022/2023 msamaha wa kodi kwenye nyasi bandia na vifaa ambata vyake
utakwenda mpaka ngazi ya Halmashauri. Nitumie fursa hii kuzipongeza timu zetu
za Serengeti Girls na Tembo Warriors zilizokata tiketi za kuiwakilisha nchi
kwenye mashindano ya Dunia. Niitakie kila la heri timu yetu ya Taifa Stars ambayo
bado iko kwenye kampeni za kutafuta tiketi ya mashindano ya kimataifa.
Mkakati wa Uchumi wa Buluu
94.
Mheshimiwa Spika, uchumi wa buluu kwa hapa Tanzania siyo jambo jipya kwani
shughuli mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika maeneo yenye fursa hizi za
kiuchumi. Katika maeneo hayo, fursa za uwekezaji zinazopatikana ni za uvuvi wa
samaki, ufugaji wa samaki, madini ya chumvi, utafutaji wa gesi na mafuta,
kilimo cha mwani, utalii wa fukwe, usafiri na usafirishaji, utunzaji wa
mazingira, na kilimo cha umwagiliaji. Hata hivyo, licha ya kuwepo kwa fursa
nyingi katika eneo hili, bado mchango wake katika uchumi ni mdogo
ikilinganishwa na uwezo uliopo. Hii ni kutokana na kukosekana kwa mfumo
madhubuti wa kuongoza na kuelekeza
uvunaji na matumizi endelevu ya rasilimali hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa
na vijavyo. Mheshimiwa Spika, sekta zilizoko katika eneo hili hazijawa na uratibu mzuri na
kila moja inajifanyia shughuli zake bila utaratibu maalum na ushirikishaji wa
kutosha wa wadau katika tasnia hii. Kama fursa hizo zingetumika kikamilifu,
zingeweza kuwa kichocheo cha kukua kwa uchumi, chanzo cha chakula na ajira,
msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kukuza viwanda, kupunguza umaskini
na kuongeza mapato ya Serikali.
95.
Mheshimiwa Spika,
kufuatia umuhimu wa sekta hii,
Serikali inakamilisha maandalizi ya Mkakati wa Uchumi wa Buluu ili kutambua
mchango wa sekta hiyo katika uchumi na ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, Ibara ya 27. Mkakati huo unaandaliwa kwa njia
shirikishi inayohusisha wadau wa sekta ya umma, sekta binafsi, washirika wa
maendeleo na jamii kwa ujumla. Mheshimiwa Spika,
shughuli nyingi zinazofanywa katika sekta za uchumi wa buluu
ni biashara. Hivyo, sekta binafsi inatarajiwa kuwa na jukumu muhimu katika
kufadhili mkakati huo. Serikali itajikita zaidi katika kujenga mazingira
wezeshi ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi. Fedha za Serikali zitaelekezwa
maeneo ambayo sekta binafsi ina hamu ndogo ikiwa ni pamoja na miundombinu
wezeshi, kuweka mifumo ya kisera, kisheria na kitaasisi ya usimamizi na
matumizi endelevu ya rasilimali hizo kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Mikakati ya
Kupunguza Makali ya Maisha kwa Mwananchi
96.
Mheshimiwa Spika, Serikali itachukua hatua za
makusudi ili kupunguza makali ya maisha kwa mwananchi
yaliyotokana na athari za vita. Hatua
zitakazochukuliwa kukabiliana na hali hiyo ni kama ifuatavyo: kuhusu
ongezeko la bei za mafuta ya petroli: Serikali imepunguza tozo
mbalimbali zilizokuwa kwenye ukokotoaji wa bei ya nishati ya mafuta. Aidha,
Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza bei za
nishati ya mafuta hapa nchini. Vilevile, Serikali inachukua hatua nyingine
katika suala hili ikiwemo: kuendelea kutoa ruzuku kwa ajili ya kupunguza bei ya
nishati ya mafuta; kuruhusu watu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu;
kuanzisha mfuko wa kuhimili ukali wa bei za mafuta (Fuel Price Stabilization
Fund) baada ya bei za mafuta kutulia katika soko la dunia; kuanzisha
hifadhi ya mafuta ya kimkakati (National Strategic Petroleum Reserve);
na kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghala moja (Single Receiving Terminal
- SRT).
97.
Mheshimiwa Spika, kuhusu ongezeko la bei za mafuta ya kula: Serikali itaweka mikakati ya kikodi ili kutoa unafuu wa
uagizaji wa mafuta ghafi ya kula kwa wachakataji wa ndani kwa lengo la kuongeza
uzalishaji, kupunguza bei ya bidhaa hiyo na kuongeza ajira. Aidha, Wakala wa
Taifa wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mbegu za Kilimo imesafisha na kusambaza kwa
wakulima tani 2,000 za mbegu za alizeti zenye thamani ya shilingi bilioni 5.84
kwa utaratibu wa ruzuku kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula
ambapo wastani wa tani 400,000 za alizeti na tani 100,000 za mafuta
zinatarajiwa kuzalishwa. Vilevile, Wakala umezalisha mbegu-miche ya michikichi
121,292 ili kuongeza uzalishaji wa mafuta ya michikichi. Hatua hizi kwa pamoja
zitasaidia kuongeza upatikanaji wa mafuta na hatimaye kupunguza kasi ya kupanda
kwa bei. Napendekeza kutoza kodi ya
ongezeko la thamani kwa kiwango cha sifuri kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa
nchini.
98.
Mheshimiwa Spika, kuhusu ruzuku ya mbolea: Wote tunatambua umuhimu wa
kilimo katika uchumi wetu na maendeleo ya wananchi. Sekta hii inakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, tija ndogo pamoja na
athari zinazoikumba dunia hivi sasa kutokana na vita kati ya nchi za Urusi na
Ukraine. Katika kuongeza tija na uzalishaji wa sekta hii na kumpunguzia mzigo
mkulima, Serikali imejipanga kutoa unafuu wa upatikanaji wa pembejeo ikiwemo
mbolea, zana za kilimo, viuatilifu, mbegu bora na kuimarisha kilimo cha
umwagiliaji. Katika kuongeza uzalishaji na
upatikanaji wa mbolea nchini, Serikali itatoa ruzuku ya mbolea na kuvipa kipaumbele viwanda vya ndani vya
mbolea katika matumizi ya chokaa ili kupunguza gharama za uzalishaji. Napendekeza
kutoza kodi ya ongezeko la thamani kwa kiwango
cha sifuri kwenye mbolea inayozalishwa nchini. Kiwango hiki kitahusu tu
wazalishaji wa mbolea. Kadhalika, napendekeza kupunguza tozo ya mrahaba
kwenye madini ya kuzalisha nishati na mbolea viwandani.
99. Mheshimiwa Spika, Serikali
inachukua hatua hizi zote ili kupunguza makali ya maisha kwa watanzania.
Serikali imekubali kupunguza mapato yake ili mwananchi au mtanzania apate
unafuu. Ruzuku kwenye nishati ni kwa ajili ya wananchi siyo kwa ajili ya
makampuni. Wafanyabiashara tusitumie majanga kujinufaisha kwa gharama ya
kuwaumiza wananchi kwa kutengeneza faida kubwa kuliko kipindi cha majanga.
Kipindi cha matatizo ya kiuchumi kila mmoja anatakiwa kubadili makadirio yake
ya kiuchumi. Tunatoa ruzuku ili kupunguza gharama za uzalishaji na hivyo, kuleta
unafuu kwa mwananchi. Naelekeza mamlaka
zote zinazosimamia sekta za huduma wasimamie haki za wananchi ili azma ya
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kumpa nafuu mtanzania iweze kuwanufaisha
watanzania.
V.
MABORESHO YA MFUMO WA KODI, ADA, TOZO NA HATUA NYINGINE ZA MAPATO
100. Mheshimiwa Spika, kuanzia kipindi cha mwaka 2019/20, Dunia imepita
kwenye changamoto kubwa ya kiuchumi kufuatia kuenea kwa janga la UVIKO-19 na
baadaye kuzuka kwa vita ya Urusi na Ukraine Februari 2022. Hii imeathiri si tu
upatikanaji wa bidhaa muhimu katika soko la Tanzania lakini pia imesababisha
mfumuko wa bei, kupanda kwa gharama za maisha na kuathiri ukuaji wa uchumi
nchini. Athari
za kiuchumi zilizoanza kujitokeza ni pamoja na kupungua kwa uzalishaji
viwandani na mashambani kulikosababishwa na changamoto ya upatikanaji wa
malighafi muhimu za viwandani na kilimo kama vile ngano, mbolea na mafuta
ghafi. Hatua za mapato kwa mwaka 2022/23 zinalenga “Kuongeza
kasi ya Kufufua Uchumi na Kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya Kuboresha
Maisha ya Watanzania”.
101. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maelezo hayo,
napenda kuwasilisha mapendekezo ya kufanya marekebisho ya mfumo wa kodi,
ikiwemo baadhi ya viwango vya kodi, tozo na ada zinazotozwa chini ya Sheria
mbalimbali na kurekebisha taratibu za ukusanyaji na usimamiaji wa mapato ya
Serikali. Marekebisho haya yamezingatia dhamira ya Serikali ya kuendelea kuwa
na mfumo wa kodi ambao ni tulivu na wa kutabirika. Vilevile, marekebisho
yanatarajiwa kujibu maswali na kukidhi kiu ya jamii ya Watanzania yakilenga
kuchachua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali ndani ya nchi kwa kuweka mkazo
katika sekta za kimkakati kama vile kilimo, ufugaji na uvuvi, miundombinu ya
umeme, uchukuzi na usafirishaji na sekta za kijamii za elimu na afya ili
kuboresha uzalishaji, kukuza uchumi jumla, kukuza ajira na hatimaye kupunguza
ukali wa maisha ya wananchi. Aidha, hatua hizi zinalenga kuimarisha usimamizi,
ukusanyaji wa mapato ya ndani ya nchi na kudhibiti upotevu wa mapato ya
Serikali. Marekebisho
yanayopendekezwa yanahusu sheria zifuatazo:
(a)
Sheria ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148;
(b)
Sheria ya
Kodi ya Mapato, SURA 332;
(c)
Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;
(d)
Sheria ya
Usimamizi wa Kodi, SURA 438;
(e)
Sheria ya
Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290;
(f)
Sheria ya
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, SURA 263;
(g)
Sheria ya
Madini, SURA 123;
(h)
Sheria ya
Korosho, NAMBA 18;
(i)
Sheria ya
Usafirishaji Bidhaa Nje ya Nchi, SURA 196,
(j)
Sheria ya
Posta na Mawasiliano ya Kielektroniki, SURA 306;
(k)
Sheria ya
Bima, SURA 394;
(l)
Sheria ya
Magari ya Kigeni, SURA 84;
(m)
Sheria ya
Benki Kuu ya Tanzania, SURA 197;
(n)
Sheria ya
Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004;
(o)
Utekelezaji
wa Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara (Blueprint) kwa
kurekebisha Ada na Tozo mbalimbali; na
(p)
Marekebisho
madogo madogo katika baadhi ya Sheria za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali.
(a)
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148
102. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani, Sura 148 kama ifuatavyo:
(i)
Kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwenye miti ambayo haijachakatwa (standing tree). Lengo la hatua hii ni
kuchochea ukuaji wa sekta ya misitu, kuongeza ajira na kuwa na usimamizi
endelevu wa rasilimali za misitu. Hatua hii itapunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 8,814. Hata hivyo, mapato yatakayoongezeka kutokana na
ukuaji wa sekta ya misitu na mnyororo wake wa thamani ni shilingi milioni
16,125 na hivyo kuleta ongezeko katika sekta hii kwa kiwango cha shilingi
milioni 7,311;
(ii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Thamani kwenye malighafi zinazotumika kuzalisha mitungi ya gesi
zinazotambulika kwa HS Code
7229.90.00, 3810.90.00, 3401.19.00, 7904.00.00, 4016.93.00, 8481.10.00 na
8309.90.90. Lengo la hatua hii ni kuwapa unafuu wazalishaji wa mitungi ya gesi
na kulinda viwanda vya ndani. Aidha, msamaha husika utatolewa baada ya
mzalishaji kusaini Mkataba wa Utekelezaji (Performance Agreement) na Serikali;
(iii) Kufanya marekebisho kwenye
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kutambua mikopo mbadala inayofuata
misingi na taratibu zilizo nje ya sekta ya fedha kwa asili yake ishughulikiwe
sawa sawa (treated) na mikopo inayotolewa na benki katika utaratibu wa kawaida.
Lengo la hatua hii ni kuchachua ukuaji wa bidhaa nyingine zenye lengo la
kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi na kuweka usawa katika ulipaji kodi;
(iv) Kutoza Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwa Kiwango cha asilimia 0 kwenye bidhaa za mafuta ya kula yanayozalishwa
nchini kwa mwaka mmoja ili kuleta unafuu wa bei ya mafuta ya kula iliyopanda
kutokana na mdororo wa uchumi;
(v) Kutoza Kodi ya Ongezeko la Thamani
kwa kiwango cha sifuri kwenye mbolea inayozalishwa nchini kwa mwaka mmoja. Kiwango
hiki kitahusu tu wazalishaji wa mbolea tu. Lengo la hatua hii ni
kuleta unafuu kwa wakulima hasa katika kipindi hiki cha mdororo wa uchumi
duniani;
(vi) Kufanya marekebisho kwenye
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya Fedha, mamlaka ya kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
wawekezaji mahiri maalumu baada ya kuidhinishwa na NISC kwa mujibu wa kifungu cha
20(8) cha Sheria ya Uwekezaji SURA, 38 pamoja na kupata ridhaa ya Baraza la
Mawaziri. Lengo la hatua hii ni kufanikisha maendeleo ya sekta ya uwekezaji
nchini na kuondoa mgongano wa kisheria kuhusu utoaji wa vivutio vya ziada vya
kikodi kati ya Sheria ya Uwekezaji na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani;
(vii) Kufanya marekebisho kwenye
Kifungu cha 11 (10) cha Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani ili kuhusisha
bidhaa za mtaji zinazotambulika kwa heading 87.16 na HS Code 8701.20.90
kwenye bidhaa za mtaji (capital goods) zinazostahili kupata ahirisho la Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT deferment). Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za
uwekezaji na kuchochea maendeleo ya viwanda nchini;
(viii) Kutoa msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye vifaa vya kupima kiwango cha maji na unyevunyevu
kwenye udongo (chameleon sensor reader) zinazotambulika kwa HS Code 9026.10.00, kifaa cha kupima
kiasi kilichochukuliwa na udongo hasa katika eneo la mizizi ya mmea (wetting
front detectors) kinachotambulika kwa HS
Code 9031.80.00, kifaa cha kupima kiwango cha chumvi katika maji
(electronic conductivity meter) kinachotambulika kwa HS Code 9027.80.00, na kifaa cha kupima kiwango cha naitrojeni
katika hali ya naitreti (nitrate test strips) kinachotambulika kwa HS Code 9027.90.00. Lengo la hatua hii
ni kukuza utafiti na kuendeleza sekta ya kilimo kwa ukuaji endelevu pamoja na
kuongeza tija. Msamaha utatolewa baada ya kupata uthibitisho wa Waziri mwenye
dhamana ya masuala ya kilimo ili kuhakikisha msamaha husika unatumika kwa
manufaa ya wakulima na si vinginevyo. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 2,995;
(ix) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye vyandarua vinavyotumika katika uzalishaji wa mbogamboga na maua
(Agro-net) vinavyotambulika kwa HS Code 56.08. Lengo la hatua hii ni kukuza
sekta ya kilimo na kuongeza tija kwenye uzalishaji;
(x) Kutoa msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye vifaa vya kupima kiwango cha unyevunyevu (moisture
meter) vinavyotambulika kwa HS Code
9003.18.00, kifaa cha kupima kiwango cha mvua iliyonyesha (rain gauge for
weather stations) kinachotambulika kwa HS
Code 9023.00.90, kifaa cha kupima hali ya alkaline na tindikali (PH meters)
kinachotambulika kwa HS Code 3822.00.90;
kifaa cha kuzalisha miche/mbegu kwa chupa (tissue culture equipment)
kinachotambulika kwa HS Code
8419.89.60; na kifaa cha kupima uwezo wa kuvutika (tension meters)
kinachotambulika kwa HS Code
9031.80.00. Lengo la hatua hii ni kuboresha utabiri wa hali ya hewa,
kufahamisha mipango sahihi na kupunguza hatari zinazohusiana na kutokuwa na
uhakika wa hali ya hewa na hali ya udongo. Msamaha utatolewa baada ya kupata
uthibitisho wa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kilimo ili kuhakikisha
msamaha husika unatumika kwa manufaa ya wakulima na si vinginevyo. Hatua hii
inatarajia kupunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
1,634.52;
(xi) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye magari yenye jokofu (refrigerated trucks) yanayotambulika kwa HS Code 8704.21.90, 8704.22.90,
8704.23.90, 8704.31.90, 8704.32.90, 8704.90.90 na vyumba vya ubaridi (cold
rooms) vinavyotambulika kwa HS Code 9406.10.10 na 9406.9010. Hatua hii inalenga kuzuia mazao kuharibika
baada ya mavuno na kuchochea kilimo cha kisasa. Msamaha utatolewa baada ya
kupata uthibitisho wa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya kilimo na au Waziri
mwenye dhamana ya masuala ya mifugo na uvuvi ili kuhakikisha msamaha husika unatumika kama
ilivyokusudiwa na si vinginevyo. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 3,744.47;
(xii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye malighafi za kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa HS Code 2528.00.00, 2710.99.00 na 3505.20.00 na mashine za kutengeneza mbolea zinazotambulika kwa Sura
(Chapter) 84 na 85 ya Kitabu cha Ushuru wa pamoja wa Forodha wa Afrika
Mashariki. Hatua hii inalenga kutoa
unafuu kwa wazalishaji wa mbolea na kuvutia uwekezaji nchini. Msamaha utatolewa
baada ya kupata uthibitisho wa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya viwanda ili
kuhakikisha msamaha husika unatumika kwa manufaa ya wazalishaji wa mbolea na si
vinginevyo. Hatua hii inatarajia kupunguza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 139;
(xiii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vanila ya kijani
isiyochakatwa inayotambulika kwa HS Code
0905.10.00 ili kuleta usawa na mazao mengine yasiyochakatwa ambayo
husamehewa Kodi ya Ongezeko la Thamani. Hatua hii inalenga vanilla
isiyochakatwa kutoka nje ya nchi kuingizwa na kuchakatwa hapa nchini na hivyo
kuongeza ajira na fedha za kigeni. Vanila inayolimwa hapa nchini haitoshelezi
mahitaji ya kiwanda cha kuchakata zao hili. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 38;
(xiv) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye kamba za katani
zinazozalishwa nchini. Lengo la hatua hii ni kukuza zao la katani na kuongeza
ajira;
(xv) Kutoa msamaha wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwenye mtindi (yoghurt) na maziwa yanayozalishwa kwa joto
la juu na kudumu kwa muda mrefu (UHT Milk). Hatua hii inalenga kuwawezesha
wazalishaji wa ndani kushindana kikanda na kimataifa, kuongeza ajira na
kuboresha maisha ya watu. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 480;
(xvi) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye vifungashio vya maziwa (dairy packaging materials)
vinavyotambulika kwa HS Code 3923.30.00,
4819.10.00, 4819.20.00 na 4819.20.90. Hatua hii inalenga kutoa
unafuu kwenye sekta ya maziwa nchini na kuwawezesha wazalishaji wa ndani
kushindana kwenye masoko ya kikanda na kimataifa. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 1,197;
(xvii)Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye hereni za mifugo za kieletroniki (ear tag) zinazotambulika kwa HS Code 3926.90.90, meza za kuwekea
hereni za mifugo (Automatic Turning Table/ Ear tag supporting table)
zinazotambulika kwa HS Code 8207.30.00,
Ear tag Applicators zinazotambulika
kwa HS Code 8456.90.00 na Lessor
beam Machines zinazotambulika kwa
HS Code 9402.90.90. Lengo la hatua hii ni kuleta ufanisi katika
utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo nchini. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 794;
(xviii) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwenye vifaa vya machinjio (stunning box) vinavyotambulika kwa HS Code 8438.50.00 na Skinning & dehiding pulling machines
zinazotambulika kwa HS Code
8453.10.00. Hatua hii inalenga kuhamasisha ukuaji wa sekta ya mifugo, kuongeza
ubora wa nyama na ngozi na kuhakikisha kuwa viwanda vya ndani vinapata
malighafi za kutosha. Msamaha utatolewa baada ya kupata uthibitisho ya Waziri
mwenye dhamana ya masuala ya mifugo na uvuvi ili kuhakikisha msamaha husika
unatumika kama ilivyokusudiwa na si vinginevyo. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 331.95;
(xix)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mbegu za malisho zinazotambulika kwa HS Code 1209.25.00 (pasture grass
seeds); HS Code 1209.21.00 (pasture legume seeds), HS Code
1209.29.00 (Pasture multiple tree seeds and pasture cuttings and rhizomes and
stolons). Hatua hii inalenga kuhakikisha upatikanaji wa mbegu za malisho za
kutosha na kukuza sekta ya mifugo;
(xx) Kufanya marekebisho kwenye
Kipengele cha 18 cha Sehemu ya Kwanza ya Jedwali la Msamaha ili kuhusisha vifaa
na mashine zinazotumiwa na vyombo vya ulinzi na usalama (military and armed
forces). Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za ununuzi wa mashine na vifaa
husika na kuimarisha mfumo wa ulinzi na usalama nchini. Msamaha utatolewa baada
ya kupata uthibitisho wa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya ulinzi na usalama
ili kuhakikisha msamaha husika unatumika kwa manufaa ya vyombo vya ulinzi na
usalama na si vinginevyo;
(xxi)
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
vifaa na mitambo ya hali ya hewa vinavyoingizwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa
Nchini (TMA). Hatua hii inalenga kuimarisha mifumo ya utendaji kazi kwa kutumia vifaa vya kisasa kutabiri hali ya hewa kwa ajili
ya mipango sahihi na usalama wa Taifa;
(xxii)
Kusamehe kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye
nyavu za kuvulia (fishing net) zinazotambulika kwa HS Code 3926.09.10; ndoano (fishing hooks) zinazotambulika kwa HS
Code 9507.20.00; na kamba za kufungia ndoano (fishing lines)
zinazotambulika kwa HS Code 9507.90.00 na 9507.30.00. Lengo la hatua hii
ni kukuza wavuvi wadogo na kuchochea ukuaji wa Sekta ya Uvuvi;
(xxiii) Kufanya marekebisho ya
Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 ili kuiwezesha Serikali
kukusanya Kodi ya Ongezeko la Thamani katika biashara mtandao (digital services) bila
kuathiri uwajibikaji chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332. Aidha
marekebisho haya yanalenga kurahisisha utaratibu wa usajili wa walipakodi
wanaotoa huduma za kidijitali bila ya kuwa na makazi hapa nchini (simplified
registration). Hatua hii inalenga kwenda sambamba na mwamko wa shughuli za
kibiashara duniani zinazofanyika kwa njia ya mtandao. Hatua hii inatarajiwa kuiongezea Serikali mapato ya shilingi milioni 34,240;
(xxiv) Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye simu
janja za Mkononi (Smartphones) HS code 8517.12.00, vishikwambi (Tablets)
HS Code 8471.30.00 au 8517.12.00 na Modemu HS Code 8517.62.00 au
8517.69.00 kwa kuwa msamaha husika haujawezesha kupatikana kwa
bidhaa hizo muhimu kwa bei nafuu kwa walengwa na badala yake unawanufaisha
wafanyabiashara. Hatua hii
inalenga kuiongezea Serikali mapato
kiasi cha Shilingi milioni 33,705; na
(xxv) Kufuta msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye huduma za kukodi ndege (air charter services) kwani huduma hizi
hutolewa kibiashara kama huduma za kukodi vyombo vingine vya usafiri ambazo
kisheria hulipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shillingi milioni 36,545.
Hatua zote za Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 87,523.
(b) Sheria
ya Kodi ya Mapato, SURA 332
103.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Kodi ya Mapato, Sura 332 kama ifuatavyo:
(i)
Kufanya marekebisho kwenye Jedwali la Kwanza la
Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuweka kiwango cha asilimia 3.5 kwa walipakodi
wenye mauzo yanayozidi shilingi milioni 11,000,000 lakini yasiyozidi shilingi
milioni 100,000,000/= kwa mwaka (Presumptive Regime) kwa lengo la
kuweka uwazi na kurahisisha makadirio na ulipaji wa kodi. Hatua hii itaongeza
ulipaji kodi wa hiari na hivyo kuongeza mapato ya Serikali ambayo yanatarajiwa kuongezeka
kwa shilingi milioni 60,413.37. Sambamba na pendekezo hili,
inapendekezwa kufanya maboresho kwenye mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania ili
kuwezesha malipo kufanyika kwa njia ya simu;
(ii) Kufanya marekebisho kwenye
Sheria ya Kodi ya Mapato ili kubainisha kuwa mikopo mbadala
iliyoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania inayotolewa na benki kwa wateja wake
ambayo inahusisha ununuzi na
uuzaji wa mali anazozihitaji mteja kwa faida inayowekwa juu ya gharama ya mali ni sawa na mikopo mingine ya kawaida. Hatua hii haimwondolei muuzaji wajibu wa kulipa kodi ya
ongezeko la mtaji kwa mujibu wa Sheria katika muamala wa mauzo ya mali kwa
mteja wa benki aliyenunua mali hiyo kupitia utaratibu wa mkopo mbadala. Lengo la hatua hii ni
kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanaweza kupata mikopo katika taasisi za fedha
ikijumuisha wale ambao hawakubaliani na utaratibu wa riba;
(iii) Kufanya marekebisho kwenye
Kifungu cha 10 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya Fedha mamlaka ya kusamehe kodi ya mapato kwa wawekezaji mahiri
maalumu baada ya kuidhinishwa na NISC kwa mujibu wa kifungu cha 20(8) cha
Sheria ya Uwekezaji Sura ya 38, pamoja na kupata ridhaa ya Baraza la Mawaziri.
Lengo la hatua hii ni kufanikisha maendeleo ya sekta ya uwekezaji nchini na
kuondoa mgongano wa kisheria kuhusu utoaji wa vivutio vya ziada vya kikodi kati
ya Sheria ya Uwekezaji na Sheria ya Kodi ya Mapato;
(iv) Kufanya marekebisho kwenye
Sheria ya Kodi ya Mapato ili kuondoa msamaha wa kukata Kodi ya Zuio kwenye
malipo ya upangishaji nyumba, vyumba na majengo ya biashara. Lengo la hatua hii
ni kuwezesha wapangaji kukusanya kodi ya zuio kwenye pango na kuiwasilisha
Serikalini. Aidha, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ataingia makubaliano ya
uwakala na OR - TAMISEMI juu ya usimamizi na ukusanyaji wa kodi hii;
(v) Kusamehe Kodi ya Ongezeko
la Mtaji kwenye uhamishaji wa haki na taarifa za madini kwenda kwenye Kampuni
za Ubia zinazoundwa baina ya Serikali na wawekezaji na uhamishaji wa hisa (Free
Carried Interest) kutoka Kampuni ya Ubia kwenda kwa Serikali. Hatua hii
inalenga kusaidia Serikali kutekeleza majukumu yake ya kimkataba na kuhakikisha
kuwa uhamishaji na ubadilishaji wa haki na taarifa za madini unafanyika kwa
wakati;
(vi) Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwenye hisa ambazo Serikali
imepata kupitia Msajili wa Hazina. Lengo la hatua hii ni kutatua changamoto
zilizopo na kuhakikisha kuwa zoezi la ubadilishaji umiliki wa hisa hizo
linafanyika kwa wakati;
(vii)
Kusamehe kodi ya zuio kwenye Kuponi za Hati
Fungani za Makampuni na Manispaa (Coupon for corporate and municipal bond).
Pendekezo hili linalenga kuongeza vyanzo mbadala vya kugharamia miradi ya maendeleo
(alternative financing);
(viii)
Kupunguza kiwango cha kodi ya zuio kwenye
tasnia ya filamu kwa malipo yanayofanyika kwenda kwa watoa huduma wa nje ya
nchi kutoka asilimia 15 hadi asilimia 10. Lengo la hatua hii ni kukuza tasnia
ya filamu na kuchochea uhamishaji wa ujuzi kwenye tasnia hiyo kwa lengo la
kuongeza ajira na kuboresha maisha;
(ix) Kutoza Kodi ya Mapato ya
asilimia 2 kwenye malipo yanayofanywa kwa watoa huduma za kidijitali wa kigeni.
Lengo la hatua hii ni kuongeza wigo wa kodi na kuzingatia kanuni za usawa za
kodi. Hatua hii inatarajia kuongeza
mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 4,889.35;
(x) Kutoza Kodi ya Zuio kwa
kiwango cha asilimia 2 kwenye malipo ya wachimbaji wadogo wa madini (Small Scale Miners). Hatua hii inalenga kuweka
utaratibu maalum wa utozaji kodi kwa wachimbaji hao na kutatua changamoto zilizopo kwenye ukusanyaji
kodi katika sekta hiyo. Hatua hii inatarajia kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
37,290.40;
(xi) Kutoza kiwango cha mfuto (flat rate) cha shilingi
3,500,000 ikiwa ni kodi ya mapato inayopaswa kulipwa kwa kila magari ya mizigo
na mabasi ya abiria kwa mwaka. Lengo la hatua hii ni kuongeza uwazi katika
makadirio ya kodi baina ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na walipakodi, kuweka
mfumo wa kodi unaotabirika na kuongeza mapato ya Serikali. Hatua hii
inatarajiwa kuiongezea Serikali mapato yanayokadiriwa kuwa shilingi
milioni 141,052;
(xii)
Kuanzisha
utaratibu wa kutoza kodi ya awali ya mapato (advance income tax) ya shilingi 20
kwa lita kwa wafanyabiashara rejareja wa mafuta ya petroli nchini
itakayokusanywa na waingizaji wa mafuta hayo kwa jumla na kulipwa Serikalini.
Lengo la hatua hii ni kurahisisha ulipaji kodi ya mapato kwenye vituo vya
mafuta na kupunguza gharama za matumizi hususan karatasi za kutolea risiti za
kielektroniki; Hatua hii inatarajiwa kuiongezea Serikali mapato
yanayokadiriwa kuwa shilingi milioni 59,820.
Hatua hizi za Kodi ya Mapato kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 102,593.
(c)
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
104. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa kifungu cha 124(2), marekebisho ya viwango maalum vya ushuru
wa bidhaa (specific duty rates) kwa
bidhaa zote zisizo za petroli yanaweza kufanyika kila mwaka
ili kuviwianisha na mfumuko wa bei na viashiria vingine vya uchumi jumla. Hata
hivyo, kutokana na biashara za bidhaa hizi kuzorota kutokana na athari za
kiuchumi zilizosababishwa na kupanda bei kwa bidhaa za mafuta, napendekeza kutokufanya mabadiliko ya
viwango maalum vya Ushuru wa Bidhaa kwa bidhaa zote zisizo za petroli.
Aidha, hatua hii inazingatia kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei nchini na azma
ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda, na hivyo kuhamasisha uwekezaji kwenye
sekta ya viwanda, kuvilinda na hatimaye kukuza ajira na mchango wa sekta hiyo
kwenye pato la Taifa.
105. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya marekebisho ya
Ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zifuatazo:
(i) Kupunguza ada ya leseni kwa
wazalishaji na waingizaji wa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa kutoka
shilingi 500,000/= hadi shilingi 300,000/=. Hatua hii inalenga kuwapa unafuu
wazalishaji na waingizaji wa bidhaa hizo pamoja na kusaidia kurejesha ukuaji wa
Sekta baada ya athari za UVIKO-19 na athari zinazotokana na msukosuko wa
kiuchumi duniani. Hatua hii inatarajiwa kupunguza mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 77.4. Utaratibu wa
ukusanyaji wa kodi kwenye vitenge unafanywa na Kamishna wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania chini ya Sheria ya Pamoja ya Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya mwaka 2004;
(ii) Kusamehe Ushuru wa Bidhaa
kwenye vifungashio vya maua, matunda, na mbogamboga vinavyotambulika kwa HS Codes 3923.29.00 (puneet, plastic
cryovac bags, modified atmosphere packaging - MAP bags, plastic sleeves,
perforated bags, poly packaging bags), HS
Code 3921.12.90 (cling firm), HS Code
3902.90.00 (plastic liners). Lengo la hatua hii ni kuwapunguzia gharama
wazalishaji wa matunda, mbogamboga na maua, na kuongeza usafirishaji wa bidhaa
hizo nje ya nchi na hivyo kuongeza fedha za kigeni. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi
cha shilingi milioni 653.12;
(iii)
Kutoza ushuru wa bidhaa wa shilingi 700 kwa kilo
ya bidhaa za sukari (sugar confectionery) zinazoingizwa kutoka nje ya nchi na
shilingi 500 kwa kilo ya bidhaa za sukari zinazozalishwa hapa nchini
zinazotambuliwa kwa HS Code
1806.31.00, 1806.32.00, 1806.90.00, (chokoleti), 1905.31 (biskuti) na 1704
(chingamu). Viwango tofauti vinapendekezwa ili kulinda viwanda vya ndani. Hatua
hii inatarajia kuongeza mapato ya
Serikali kwa shilingi milioni 34,453.87;
na
(iv)Kutoza Ushuru wa Bidhaa
kwenye betri za maji (Lead-acid battery) kwa kiwango cha asilimia 5
zinazotambuliwa kwa HS Code 8507.10.00, na 8507.20.00. Hatua
hii inalenga kupunguza madhara ya mazingira yanayosababishwa na matumizi ya
bidhaa hizo. Hatua hii inatarajiwa kuongeza
mapato ya Serikali kwa shilingi milioni
1,864.85;
Hatua hizi za Ushuru wa Bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla
wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 50,292.
(d) Sheria
ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438
106. Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Usimamizi wa Kodi, SURA 438
ili kumrejeshea Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Fedha na Mipango mamlaka ya
kusamehe riba na adhabu baada ya kushauriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania. Lengo la hatua hii ni kuondoa changamoto zilizopo katika kutoa
misamaha hii na kurahisisha upunguzaji au uondoaji wa riba na adhabu ya madeni.
Aidha, Waziri mwenye dhamana ya Fedha na Mipango atatoa utaratibu wa utoaji wa
misamaha hii kwa njia ya kanuni au kwa namna atakavyoona inafaa.
(e)
Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290
107. Mheshimiwa Spika, napendekeza
kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:
(i)
Napendekeza
Kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, SURA 290 ili
kugawanya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri katika utaratibu
ufuatao: asilimia 5 ipelekwe kwenye miundombinu na masoko ya machinga, asilimia
2 kwa ajili ya mikopo kwa vijana, asilimia 2 kwa ajili ya wanawake na asilimia
1 kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Lengo la hatua hii ni kuendeleza juhudi za
Serikali ya Awamu ya Sita zinazolenga kuwawekea miundombinu wajasiriamali
wadogo ili kuhakikisha wanapata maeneo ya kufanyia biashara kutokana na mikopo
wanayopata;
(ii)
Aidha,
Halmashauri zihakikishe kuwa zinafanya tathmini ya vyanzo vya mapato kabla ya
kuingia mikataba ya uwakala wa mapato kutoka kwenye vyanzo husika na
kuhakikisha kwamba kiasi kinachokusanywa kinaendana na uwezo wa chanzo hicho.
Sambamba na hilo naelekeza kuwa fedha zote zinazokusanywa kwa njia ya Point
of Sale (POS) zinazojulikana kama mapato ghafi zihamishiwe benki katika
kipindi kisichozidi siku saba kutokea kukusanywa kwa mapato hayo na Halmashauri
zihakikishe kuwa fedha zinazokusanywa kwenye Halmashauri za Serikali za Mitaa
zinahasibiwa kikamilifu;
(iii)
Kusamehe Ushuru wa Mazao kwenye
mbegu (seeds). Hatua hii inalenga kuwapa unafuu wakulima na kuongeza tija
kwenye uzalishaji mazao mbalimbali;
(iv)Kupunguza Ushuru wa Mazao
ya misitu (forest produce cess) kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3. Lengo la
hatua hii ni kupunguza gharama kwa
wafanyabiashara wa mazao ya misitu na kukuza sekta ya misitu;
(v) Kufanya marekebisho kwenye
Kifungu cha 16(7) cha Sheria ya Fedha za Mamlaka za Serikali za Mitaa Sura 290
ili kubainisha kwamba Makampuni/Taasisi/Biashara/Watu binafsi wanaotakiwa
kulipa Ushuru wa Huduma (service levy) kwenye Halmashauri moja wanatakiwa
kulipa Ushuru wa Mazao (produce cess) kwenye Halmashauri nyingine ambako wananunua
mazao ya kilimo au mazao mengine. Lengo la mapendekezo hayo ni kuhakikisha
kwamba kila Halmashauri inanufaika na shughuli za kiuchumi zinazotekelezwa
kwenye eneo lake la utawala ili kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa jamii; na
(vi)Kufanya marekebisho kwenye Kifungu cha 16 ili kumpa Waziri mwenye dhamana ya
Serikali za Mitaa mamlaka ya kuandaa Kanuni za ugawaji mapato yatokanayo na Ushuru wa Huduma kwenye Makampuni/Taasisi/Bishara/Watu binafsi
wanaotekeleza shughuli zao kwenye Halmashauri zaidi ya moja. Kifungu hiki
kitamwezesha Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa kutoa Mwongozo wa
ugawaji wa mapato hayo kwa Halmashauri husika kulingana na hali halisi.
(f)
Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Sura 263
108. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi kwa kupunguza kiwango cha mchango kwa sekta binafsi kutoka asilimia
0.6 inayotozwa sasa hadi asilimia 0.5 ya mapato ghafi ya wafanyakazi. Lengo la
hatua hii ni kuleta usawa katika uchangiaji kati ya wafanyakazi wa sekta
binafsi na wa umma.
(g)
Sheria ya Madini, SURA 123
109. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya
Madini, Sura 123 kama ifuatavyo:
(i) Kupunguza kiwango cha mrabaha kutoka kwenye makaa ya mawe
yanayotumika kama malighafi
ya kuzalisha nishati viwandani kutoka
asilimia 3 hadi asilimia moja. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za
uzalishaji viwandani, kuchochea uwekezaji zaidi na kukuza ajira;
(ii) Kupunguza kiwango cha kutoza
mrabaha (royalty) kutoka asilimia 6 hadi asilimia 4 kwa dhahabu inayouzwa
kwenye vituo vya kusafishia madini (refinery centres). Lengo la hatua hii ni
kuhakikisha kuwa vituo vilivyoanzishwa nchini vinapata malighafi ya kutosha kwa
ajili ya kusafisha na hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali;
(h) Sheria
ya Korosho, Namba 18
110. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya
Korosho ili mapato yatokanayo na tozo ya kusafirisha korosho ghafi nje ya nchi
yagawanywe kama ifuatavyo: asilimia 50 ipelekwe Wizara ya Kilimo kwa ajili ya
ruzuku ya pembejeo na Mfuko wa Kilimo (ADF); na asilimia 50 ipelekwe mfuko mkuu
wa Serikali. Lengo la hatua hii ni kuchochea maendeleo ya Sekta ya kilimo na
kusaidia upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya ruzuku na tafiti.
(i)
Sheria ya Usafirishaji Bidhaa Nje ya Nchi, SURA
196
111. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya
Usafirishaji Bidhaa Nje kwa kuanza kutoza tozo ya asilimia 30 au dola za kimarekani
150 kwenye shaba chakavu (copper waste) zinazotambulika kwa HS Code 7204 na
vyuma chakavu (scrap metals) zinazotambulika kwa HS Code 7404. Lengo la hatua
hii ni kulinda viwanda vya ndani na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi kwenye
viwanda husika. Hatua hii inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa shilingi milioni 2,446.
(j)
Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, SURA 437
112. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa kwa kupunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi
shilingi 7,000 hadi kiwango kisichozidi shilingi 4,000 katika kila muamala wa
kutuma au kutoa pesa. Punguzo hili ni sawa na asilimia 43 ya kiwango cha sasa.
Sambamba na hilo, napendekeza kuongeza wigo wa tozo hiyo ili kuhusisha miamala
yote ya kielektroniki. Lengo la hatua hii ni kupunguza makali ya maisha kwa
mtanzania hasa katika kipindi hiki cha changamoto kubwa ya kiuchumi na kuweka
usawa katika utozaji wa tozo hiyo.
(k) Sheria
ya Bima, SURA 394
113. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Bima kwa kuongeza wigo wa bima ya lazima
(mandatory insurance) kwa kujumuisha masoko ya umma, majengo ya biashara,
bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje, vyombo vya baharini na vivuko. Hatua hii
inalenga kuimarisha ushirikishwaji wa kifedha (financial inclusion) na kuongeza
matumizi ya bima.
(l)
Sheria ya Magari ya Kigeni, SURA 84
114. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Magari ya Kigeni, SURA 84 ili kupunguza tozo ya
magari yanayozidi ekseli 3 kutoka dola za kimarekani 16/100 km hadi dola za
kimarekani 10/100 km. Lengo la hatua hii ni kuwianisha utozaji wa viwango vya
tozo hizo katika ukanda wa EAC, SADC na COMESA.
(m)
Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, SURA 197
115. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya
marekebisho kwenye Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania kwa kuweka kiwango cha ukomo
wa Serikali kukopa kuwa kiasi kisichozidi asilimia 18 ya mapato ya ndani
yaliyoidhinishwa katika mwaka husika badala ya kiwango cha sasa cha moja ya
nane ya mapato ya ndani yaliyokusanywa katika mwaka uliotangulia. Lengo la
hatua hii ni kuwianisha kiwango husika na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika
Mashariki pamoja na kuiwezesha Serikali kutekeleza Bajeti yake.
(n) Sheria
ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004
116. Mheshimiwa Spika, kikao cha Mawaziri wa Fedha
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika tarehe 13 Mei, 2022 Mombasa
Kenya, kilipendekeza kufanya marekebisho ya Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa
Forodha (EAC-Common External Tariff) kwa mwaka wa Fedha 2022/23. Mapendekezo
hayo yanalenga kuongeza kasi ya kufufua uchumi na kuimarisha Sekta za
uzalishaji kwa ajili ya kuboresha maisha.
117. Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya Mawaziri wa
Fedha ya kufanya marekebisho kwenye Viwango vya Pamoja vya Ushuru wa Forodha
yanahusisha hatua mpya na zinazoendelea ambazo zimekuwa zikitekelezwa katika
Mwaka wa Fedha 2021/22. Hatua hizo ni kama zifuatazo:
(i)
Mapendekezo ya hatua mpya za Viwango vya
Ushuru wa Forodha ni kama ifuatavyo: -
(a)
Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 au dola za Marekani 1.5
kwa
kila mita moja ya mraba (square meter) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za
marumaru zinazotambulika kwa HS Codes 6907.21.00; 6907.22.00; na 6907.23.00.
Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani vinavyozalisha marumaru, pamoja na kudhibiti udanganyifu wa
thamani halisi ya bidhaa hizo kutoka nje;
(b)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za Marekani 125
kwa kila tani moja (Metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa
kwenye mabati yanayotambulika kwa
HS Codes 7212.20.00; na 7226.99.00 kwa mwaka mmoja badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee.
Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa
thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and
under valuation), na kulinda ajira pamoja na mapato ya Serikali;
(c)
Kurejesha
utozaji wa Ushuru wa Forodha wa kiwango cha asilimia 0 kutoka kiwango kilichokuwa kinatumika cha asilimia 25 kwenye mafuta ghafi ya kula (Crude Palm Oil) yanayotambulika kwa HS
code 1511.10.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa
mafuta ghafi hapa nchini ili wananchi waweze kupata mafuta ya kula kwa bei
nafuu;
(d)
Kutoza
Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kutoka kiwango
cha awali cha asilimia 0 kwenye mafuta ghafi ya soya, karanga, nazi na haradali
zinazotambulika kwa HS codes 1507.10.00; 1508.10.00; 1513.11.00;
1514.91.00; na 1515.11.00. Lengo la hatua hii ni kuoanisha viwango vya
mafuta haya ghafi vifanane na viwango vya mafuta ghafi ya alizeti, pamba na
mafuta ghafi mengineyo ambayo viwango vyake ni asilimia 10. Aidha, hatua hii
pia inalenga kulinda na kuhamasisha uzalishaji wa mbegu za mafuta ya kula
nchini, kuongeza ajira pamoja na kulinda fedha za kigeni zinazotumika kuagiza
mafuta hayo nje ya nchi;
(e)
Kutoza
Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za Marekani 500 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton)
kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya asilimia 35 kwa mwaka
mmoja kwenye mafuta ya kula yaliyochakatwa kwa kiwango cha kati na cha mwisho (semi-refined and refined)
yanayotambulika kwa HS codes 1507.90.00; 1508.90.00; 1509; 1510.10.00; 1510.90.00; 1511.90.10; 1511.90.30; 1511.90.90;
1512.19.00; 1512.29.00; 1513.19.00; 1513.29.00; 1514.19.00; 1514.99.00;
1515.19.00; 1515.29.00; 1515.50.00; na 1515.90.00. Lengo la hatua hii ni kulinda
viwanda na kuhamasisha uchakataji wa mbegu na mafuta ghafi yaliyoingizwa nchini
ili kuongeza thamani ya bidhaa (value addition) na kukuza ajira;
(f)
Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye taulo za watoto (Baby Diapers)
zinazotumbulika kwa HS code 9619.00.90. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda
vinavyozalisha bidhaa hii nchini, kuongeza ajira pamoja na mapato ya Serikali;
(g)
Kuongeza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye
nyuzi za pamba (cotton yarn) zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06 na 52.07 isipokuwa nyuzi za pamba zinazotambulika kwa HS Code 5205.23.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha
bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao la pamba (value addition) nchini;
(h)
Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa
Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye milango na madirisha ya alluminium
na chuma yanayoagizwa kutoka nje yanayotambulika kwa HS Codes 7610.10.00 na 7308.30.00. Lengo la hatua hii ni kulinda wajasiriamali wa ndani
wanaotengeneza bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na mapato ya Serikali;
(i) Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
malighafi za kutengeneza viongeza ladha kwenye vyakula na vinywaji (food
flavors) zinazotambulika kwa HS
Code 1901.90.10; 3302.10.00; na 3505.10.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa
bidhaa hizo nchini;
(j)
Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 25 au asilimia 10 hadi asilimia 0
kwa mwaka mmoja kwenye karatasi
zinazotambulika kwa HS Codes 4804.19.90; 4804.39.00; 4804.42.00;
4804.51.00; 4804.52.00; 4805.11.00; 4805.19.00; 4805.24.00; 4805.25.00;
4805.93.00; 4810.13.00; 4810.19.00; 4810.31.00; na 4810.32.00 zinazotumika
kama malighafi ya kutengeneza vifungashio aina ya maboksi (corrugated boxes).
Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa vifungashio hivyo hapa
nchini ili wananchi waweze kuvipata kwa urahisi na kwa bei nafuu;
(k) Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
malighafi za kutengeneza vioo vizito (toughened glass) zinazotambulika kwa HS Codes 7005.10.00; 7005.21.00;
7005.29.00; na 7005.30.00. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa vioo hivyo nchini;
(l) Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka
asilimia 25 au asilimia 10 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza nyaya za umeme (electrical
cables) zinazotambulika kwa HS Codes 7312.10.00; 7217.20.00; 7408.19.00;
7409.11.00; 7605.21.00; 2710.19.56; 3815.90.00; 5402.19.00; 5903.90.00; 7217.20.00;
7907.00.00; 7312.10.00; na 2712.10.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa nyaya hizo pamoja na kuvutia uwekezaji nchini;
(m)Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja
kwenye malighafi za kutengeneza sabuni (toilet soap) zinazotambulika kwa HS
Code 3401.20.10. Lengo la hatua hii ni
kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni nchini, kuongeza ajira na mapato ya
Serikali;
(n)
Kutoza
Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 25 badala ya kiwango cha asilimia
100 au dola za Marekani 460 kwa kila tani moja ya ujazo kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka mmoja kwenye sukari ya matumizi ya kawaida (consumption
sugar) inayoagizwa kutoka nje ya nchi kwa vibali maalum kwa lengo la kuziba
pengo (gap) la uzalishaji hapa
nchini;
(o)
Kutoa
unafuu wa Ushuru wa Forodha kwa utaratibu wa Duty Remission kutoka
asilimia 25 hadi asilimia 0 kwenye hema za chuma (Prefabricated building)
zinazotambulika kwa HS Code 9406.20.90 zitakazoagizwa na wafugaji, kwa mwaka
mmoja. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwenye sekta ya mifugo, kuvutia
uwekezaji, kuongeza ajira, pamoja na mapato ya Serikali kutokana na uwekezaji;
(p) Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35
kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704. Hatua hii
inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali;
(q) Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka
asilimia 25 hadi asilimia 10
kwenye mafuta mengineyo ya petroli yanayotambulika kwa HS Code 2710.19.10.
Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu na kulinda watumiaji wa bidhaa hii;
(r) Nchi Wanachama
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kutoza Ushuru wa Forodha kwa
kiwango cha asilimia 35 kwenye sigara za kielektroniki zinazotambulika kwa HS Code
8543.40.00. Lengo la hatua hii ni kulinda mnyororo wa thamani wa zao la tumbaku
nchini, kulinda viwanda vya ndani, pamoja na kuongeza ajira;
(s) Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
zimekubaliana kufanya marekebisho kwenye tafsiri (descriptions) ya HS Codes
7310.29.20 na 7612.90.10 ambapo awali zilikuwa zinatafsiri makasha ya
kuhifadhia vinywaji pekee ambayo ushuru wa forodha ni asilimia 0 na sasa
kujumuisha makasha ya kuhifadhia chakula ili yaweze kutozwa ushuru wa forodha
kwa kiwango cha asilimia 0 badala ya asilimia 25. Lengo la marekebisho hayo ni
kutoa unafuu kwenye vifungashio vya vyakula ili kulinda walaji.
(ii)
Mapendekezo ya kuendelea na utekelezaji wa Viwango vya Ushuru wa
Forodha vya mwaka 2021/22 ni kama ifuatavyo; -
(a)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25
au asilimia 10 hadi asilimia
0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi zinazotumika katika
uzalishaji wa vifaa maalum vinavyotumika katika kupambana na ugonjwa wa homa
kali ya mapafu (UVIKO-19)
vikiwemo barakoa (Masks), kipukusi (sanitizer), mashine za
kusaidia kupumua (ventilators), na
mavazi maalum ya kujikinga
yanayotumiwa na madaktari na wahudumu wa afya
(PPE). Msamaha huu utatolewa kwa utaratibu wa “duty remission”.
Hatua hii inalenga kutoa unafuu kwa
wazalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini ili
kuongeza kasi katika kupambana na ugonjwa huo;
(b)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye mashine za kielektroniki zinazotumika
kukusanya mapato ya Serikali (Cash registers, Electronic Fiscal Device (EFD)
Machines and Point of Sale (POS) machines) zinazotambulika kwa HS Code 8470.50.00 na 8470.90.00. Lengo
la hatua hii ni kuhamasisha matumizi ya vifaa hivi katika kuhasibu mapato ya
Serikali;
(c)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vinavyotumiwa na
wazalishaji wa maziwa kwa joto la juu yanayodumu kwa muda mrefu (UHT Milk) vinavyotambulika kwa HS code
4819.50.00. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa maziwa hapa
nchini. Utaratibu wa Duty Remission
utatumika kutoa unafuu huo;
(d)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka
kiwango cha asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa
mwaka mmoja kwenye vifuniko vya chupa za mvinyo (corks and stoppers)
vinavyotambulika kwa HS Code 4503.10.00 kwa kuzingatia kuwa havizalishwi hapa
nchini. Hatua hii inalenga kuwapunguzia gharama wazalishaji wa mvinyo ili
kuhamasisha na kuendeleza kilimo cha zao la zabibu nchini pamoja na ajira.
Utaratibu wa Duty Remission utatumika
kutoa unafuu huo;
(e)
Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 0 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye
unga wa kakao unaoingizwa kutoka nje unaotambulika kwa HS Code 1805.00.00.
Lengo ni kuchochea na kuhamasisha kilimo cha zao la kakao nchini pamoja na
kuongeza mapato ya Serikali;
(f)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya kuhifadhia kahawa
vinavyotumiwa na viwanda vya kusaga kahawa nchini. Vifungashio
vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika kwa
HS codes 7310.21.00; 6305.10.00; 3923.50.10; 3923.50.90 na 3920.30.90. Hatua
hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la kahawa na kuvipa unafuu wa gharama
viwanda vinavyosaga kahawa hapa nchini. Utaratibu wa “Duty Remission” utatumika
katika kuagiza vifungashio hivyo;
(g)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
vifungashio vya kuhifadhia korosho. Vifungashio vitakavyohusika ni vile vinavyotambulika katika HS code
3923.21.00. Hatua hii inalenga kuongeza thamani kwenye zao la korosho na kuvipa
unafuu wa gharama viwanda vinavyochakata korosho hapa nchini. Aidha utaratibu
wa “Duty Remission” utatumika katika
kuagiza vifungashio hivyo;
(h)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja
kwenye vifungashio vya kuhifadhia pamba (cotton lint). Vifungashio vitakavyohusika ni vile
vinavyotambulika kama HS codes 3920.30.90; 6305.39.00 na 7217.90.00. Hatua hii
inalenga kuvutia uwekezaji ili kuongeza thamani ya zao la pamba nchini;
(i)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 0 kwa mwaka
mmoja kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25
kwenye malighafi za kutengeneza taulo za watoto (Baby Diapers)
zinazotumbulika kwa HS code 3506.91.00 Hot Melt Adhesive; PE film
HS Code 3920.10.90, Empty bag for Baby Diapers HS Code 6305.33.00,
Plastic cask HS Code 3926.90.90; na kiwango cha awali cha asilimia 10 kwenye Super
Absorbent Polymer HS Code 3906.90.00, Wet strength paper HS Code
4803.00.00, Non-woven HS Code 5603.11.00, Polyethylene laminated
Nonwovens HS Code 5903.90.00, Spandex HS Code 5402.44.00 na Dust
free paper HS Code 4803.00.00. Aidha, msamaha huu utatolewa kwa utaratibu
wa “Duty
Remission”. Hatua hii inalenga kutoa unafuu wa gharama za
uzalishaji na kuongeza ajira;
(j)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
vifaa vinavyotumika katika kukata, kung’arisha na kuongeza thamani ya madini ya
vito vinavyotambulika kwa HS Codes 6804.10.00; 7018.90.00; 7020.00.99; 3606.90.00;
6813.20.00; 8202.20.00; 8202.99.00; 8203.20.00; 8205.10.00; 8423.89.90;
8513.10.90; na 9002.19.00. Hatua hii inalenga kuchochea uongezaji wa thamani
kwenye madini, kukuza ajira
pamoja na kuongeza mapato ya Serikali. Utaratibu wa “Duty Remission”
utatumika katika kuagiza vifaa hivyo;
(k)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
vifungashio vya mbegu vinavyotambulika kwa HS codes 3923.29.00; 6305.10.00;
4819.40.00; 7310.29.90; 6305.33.00; 6305.20.00; 6304.91.90 na 7607.19.90.
Utaratibu utakaotumika kutoa unafuu huo ni wa “Duty Remission”. Lengo la
hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa mbegu hapa nchini;
(l)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za Marekani 125
kwa kila tani moja ya ujazo
(Metric ton) kwenye bidhaa za chuma kutegemea kiwango kitakachokuwa
kikubwa badala ya ushuru wa
asilimia 10 kwa mwaka mmoja. Bidhaa hizo ni Flat -rolled
products of iron or non-alloy steel and other alloy steel. Bidhaa hizi zinatambulika kwa HS Codes 7209.16.00; 7209.17.00;
7209.18.00; 7209.26.00; 7209.27.00; 7209.28.00; 7209.90.00; 7211.23.00;
7211.90.00; 7225.50.0 na 7226.92.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya hapa
nchini, kukuza ajira pamoja na kudhibiti udanganyifu wa thamani halisi ya
bidhaa hizo kutoka nje;
(m)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za Marekani 250
kwa
kila tani moja ya ujazo (metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa
kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25 au dola za Marekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo
(metric ton) kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS
codes 7210.30.00; 7210.49.00; 7210.61.00; 7210.69.00; 7210.70.00 na 7210.90.00.
Lengo la hatua hii ni kuwalinda wazalishaji wa bidhaa hizo hapa nchini kutokana
na ushindani wa nje;
(n)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10 au dola za Marekani 250
kwa
kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kwa mwaka mmoja kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika katika HS Code
7212.60.00 badala ya ushuru wa asilimia 10 pekee. Lengo la hatua hii ni kulinda
viwanda vya ndani kutokana na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo
zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under valuation), pamoja na kulinda ajira na mapato ya
Serikali;
(o)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 au dola za Marekani 250
kwa
kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa
kikubwa badala ya ushuru wa asilimia 25 au dola za Marekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton)
kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za mabati zinazotambulika kwa HS Code 7212.30.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vya ndani kutokana na
udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing
and under valuation), pamoja
na
kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(p)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25
au dola za Marekani
250 badala ya kiwango cha asilimia 25 au dola za Marekani 200 kwa kila tani moja ya ujazo (metric
ton) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwenye bidhaa za chuma (Reinforment
bars and hallow profile) kwa mwaka mmoja. Hatua hii inahusu bidhaa
zinazotambulika kwa
HS Codes 7213.10.00; 7213.20.00; 7213.99.00; 7306.30.00; 7306.50.00;
7306.61.00; 7306.69.00; na 7306.90.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda
vinavyozalisha nondo hapa nchini kutokana
na udanganyifu wa thamani halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing
and under declaration), pamoja
na
kulinda ajira na mapato ya Serikali;
(q)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25
au dola za Marekani
250 badala ya kiwango cha asilimia 10 kwenye bidhaa za chuma (Flat-rolled
products of other alloy steel, of a width of 600 mm or more)
zinazotambulika kwa
HS Codes 7225.91.00; 7225.92.00; na 7225.99.00 kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua
hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha nondo hapa nchini kutokana na udanganyifu wa thamani
halisi ya bidhaa hizo zinapoingizwa kutoka nje (under-invoicing and under
declaration), pamoja na
kulinda ajira na mapato ya Serikali,
(r)
Kuongeza
Ushuru
wa Forodha kutoka
asilimia 0
hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za fito
za plastiki zijulikanazo kama PVC
Profiles zinazotambulika kwa HS Codes 3916.10.00; 3916.20.00; na 3916.90.00 ambazo hutumika kutengenezea
fremu za milango, madirisha n.k. Lengo la hatua hii ni kuongeza mapato ya
Serikali;
(s)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25 badala ya asilimia 10 kwa mwaka
mmoja kwenye karatasi zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini ambazo
zinatambulika kwa HS code 4804.29.00. Lengo la hatua hii ni kulinda viwanda
vinavyozalisha karatasi hizo hapa nchini;
(t)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 10 badala ya asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye ngano inayotambulika
kwa HS Codes
1001.99.10 na 1001.99.90 kwa utaratibu wa “Duty
Remission” ambapo wanaonufaika na unafuu huu ni wenye viwanda vya kusaga
ngano. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa viwanda vinavyozalisha unga
wa ngano ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa za ngano kwa bei nafuu;
(u)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 0 kutoka kiwango cha awali cha asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwa
utaratibu wa Duty Remission kwenye
bidhaa ijulikanayo kama “Printed
Alluminium Barrier Laminates” (ABL) HS Code 3920.10.90 ambayo hutumika kama
malighafi ya kutengeneza vifungashio vya dawa ya meno kwenye viwanda vya ndani.
Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu wa gharama kwa viwanda vinavyozalisha dawa
ya meno nchini;
(v)
Kutoza Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha
asilimia 0 kutoka kiwango cha awali cha asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa
utaratibu wa “Duty Remission” kwenye
malighafi ya kutengeneza sabuni ijulikanayo kama RBD Palm Stearin HS
Code 1511.90.40 kwa viwanda vinavyotengeneza sabuni nchini. Lengo la hatua hii
ni kutoa unafuu kwa viwanda vya kuzalisha sabuni nchini;
(w)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25
au dola za Marekani
1.35 kwa kila kilo
moja ya viberiti (safety match boxes) vinavyotambuliwa kwenye HS code
3605.00.00 kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa badala ya asilimia 25 pekee kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni
kulinda viwanda vinavyozalisha viberiti nchini dhidi ya bidhaa zenye ruzuku
kutoka nje na hivyo kuwa na ushindani sawa katika soko;
(x)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 25
au dola za Marekani
350 kwa kila tani moja ya ujazo (Metric ton) kutegemea kiwango
kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka mmoja kwenye bidhaa za chuma za misumari
zinazotambulika kwa HS code 7317.00.00 (nails, tacks, drawing pins,
corrugated nails, and staples other than those of heading 83.05) badala ya
asilimia 25 pekee. Hatua hii inalenga kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa
hizo nchini.
(y)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 60
badala ya asilimia 35 kwa mwaka mmoja kwenye maji ya kunywa (mineral water)
yanayotambulika kwa
HS code 2201.10.00. Hatua hii inalenga kulinda viwanda vinayvozalisha maji ya
kunywa nchini;
(z)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 10
badala ya asilimia 0 kwenye Gypsum Powder inayotambulika kwa HS code
2520.20.00 kwa mwaka mmoja. Lengo la hatua hii ni kulinda wazalishaji wa Gypsum Powder nchini;
(aa)
Kutoza Ushuru wa Forodha wa asilimia 35
kwa mwaka mmoja kwenye mitumba inayoingia kutoka nje badala ya asilimia 35 au dola za Marekani 0.40 kwa kilo moja
kutegemea kiwango kipi kikubwa kwa lengo la kutoa unafuu kwa watumiaji nchini;
(bb)
Kutoa unafuu wa Ushuru wa Forodha kwenye
malighafi, vipuri na mashine vinavyotumika katika kutengeneza viatu vya ngozi
na nguo. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha ukuaji wa sekta ya nguo na viatu vya
ngozi nchini;
(cc)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwenye
mabasi ya abiria yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99
yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka. Hatua hii inalenga kupunguza
gharama za uingizaji wa mabasi hayo ili kurahisisha huduma ya usafiri kwa
wananchi;
(dd)
Kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye
matairi mapya ya pikipiki (new pneumatic tyres of rubber) yanayotambulika kwa
HS Code 4011.40.00. Lengo la hatua hii ni kuhamasisha uzalishaji wa matairi hayo nchini kwa kuwa kuna malighafi za kutosha;
(ee)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
nyaya (wire of other alloy steel) zinazotambulika kwa HS Codes 7229.20.00 na
7229.90.00. Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama kwa
wazalishaji wanaotumia bidhaa hiyo kama malighafi;
(ff)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka
mmoja kwenye milk cans
zinazotambulika kwa HS Codes 7310.10.00 na 7310.29.90. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu wa vifungashio vya kuhifadhia maziwa ili kuwalinda
walaji nchini;
(gg)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye LABSA (Organic
surface-active agents - Anionic) inayotambulika kwa HS Code 3402.11.00 kwa
utaratibu wa Duty Remission. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wazalishaji wa sabuni za unga na maji nchini;
(hh)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kuchakata ngozi zinazotambulika kwa HS Codes 3208.20.00
na 3210.00.10 kwa utaratibu wa duty
remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu kwa
wachakataji wa ngozi nchini;
(ii)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza
mbolea zinazotambulika kwa HS Codes
2710.99.00, 2528.00.00 na 3505.20.00 kwa utaratibu wa Duty Remission. Lengo la hatua hii ni kutoa unafuu
kwa wazalishaji wa mbolea nchini;
(jj)
Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi
asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye vifungashio vya tumbaku iliyochakatwa vinavyotambulika kwa HS Code 5310.10.00
kwa utaratibu wa Duty Remission. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa tumbaku nchini;
(kk)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye
vifungashio vya chai iliyochakatwa vinavyotambulika
kwa HS Codes 4819.20.90, 5407.44.00 na 3923.29.00 kwa utaratibu wa
Duty Remission. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa wachakataji wa chai (tea blenders) nchini;
(ll)
Kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa mwaka mmoja kwa waunganishaji wa pikipiki za
matairi matatu bila kujumuisha fremu ili ziweze kutengenezwa na kuunganishwa
hapa nchini (CKD for three-wheel motorcycles excluding chassis and its
components) zinazotambulika kwa HS Code 8704.21.90 kwa utaratibu wa Duty Remission. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa waunganishaji wa pikipiki hizo nchini ili
kurahisisha usafirishaji wa mizigo;
(mm) Kupunguza
Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 au
asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka mmoja kwenye malighafi za kutengeneza
mabomba ya plastiki (glass reinforced plastic pipes) zinazotambulika kwa HS
Codes 3920.61.10, 7019.39.00, 7019.31.00, 6006.90.00,
7019.12.00, 3920.10.10, 4016.93.00, na 3907.91.00 kwa utaratibu wa duty remission. Lengo
la hatua hii ni kutoa unafuu kwa watengenezaji wa mabomba hayo nchini ili
kupunguza gharama za uzalishaji na kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji; na
(nn) Kutoza
Ushuru wa Forodha kwa kiwango cha asilimia 10 kutoka kiwango cha asilimia 100 au dola za Marekani 460 kwa kila tani moja ya ujazo
(metric tone) kutegemea kiwango kitakachokuwa kikubwa kwa mwaka
mmoja kwenye sukari ya matumizi ya viwandani
(sugar for industrial use)
inayoagizwa kutoka nje ya nchi.
Lengo la hatua hii ni kuwezesha na kutoa unafuu kwenye viwanda vinavyotumia
bidhaa hii kama malighafi.
(iii) Mawaziri wa Fedha
wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walikubaliana kiwango cha juu
cha ushuru wa forodha cha zaidi ya asilimia 25 kuwa ni asilimia 35. Hivyo,
Muundo mpya wa ushuru wa forodha wa EAC utakuwa katika mpangilio wa viwango
vinne (Four Tariff Bands) yaani asilimia 0, asilimia 10, asilimia 25 na
asilimia 35 na utekelezaji wake utaanza tarehe 1 Julai 2022. Bidhaa zitakazo
tozwa ushuru wa asilimia 35 ni pamoja na nyama, samaki, bidhaa za mbogamboga na
matunda, mafuta ya kula, Chai, magunia ya kitani, kahawa, siagi ya karanga, soseji (sausages), nyanya zilizosindikwa (tomato
sauces), saruji, chumvi, sabuni, rangi za majengo, vinywaji,
vipodozi na urembo, bidhaa za samani, bidhaa za ngozi, bidhaa za chuma,
marumaru, pamoja na bidhaa za sukari kama vile chingamu (chewing
gum), biskuti,
peremende, na
chokoleti (chocolates).
Hatua hizi kwa
ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato
ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 66,791.
(o) Utekelezaji
wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Kufanya Biashara (Blueprint) kwa
kurekebisha Ada na Tozo mbalimbali.
118. Mheshimiwa Spika, napendekeza
kufuta au kupunguza ada na tozo mbalimbali zinazotozwa na Wizara, Idara na
Taasisi zinazojitegemea ili kuondoa kero na urasimu kwa wafanyabiashara na kuboresha mazingira ya
biashara na uwekezaji hasa katika kipindi hiki cha changamoto kubwa ya
kiuchumi kufuatia kuenea kwa janga la UVIKO-19 na baadaye kuzuka kwa vita ya
Urusi na Ukraine. Hatua hizi
ni sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa Mpango wa kuboresha Mfumo wa udhibiti
wa Biashara (Blueprint for Regulatory Reforms to Improve the Business
Environment). Marekebisho hayo yatajumuisha:
(i)
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
(a) Sekta
ya Mifugo
Napendekeza kufanya marekebisho ya tozo mbalimbali
kwenye sekta ya mifugo kama ilivyoanishwa katika Kiambatisho Namba 5;
na
(b) Sekta
ya Uvuvi
Napendekeza kufanya marekebisho ya tozo mbalimbali
kwenye sekta ya uvuvi kama ilivyoainishwa kwenye Kiambatisho
Namba 6.
(ii) Wizara
ya Kilimo
(a)
Kufuta
tozo ya shilingi 200 (impoundment fee) inayotozwa kwa kila mita ya mraba ya eneo
la uso wa maji yaliyohifadhiwa kwenye mabwawa ya umwagiliaji. Hatua hii
inalenga kupunguza gharama kwa wakulima wanaofanya kilimo cha umwagiliaji; na
(b) Kuongeza ada ya kibali cha kusafirisha mbolea nje ya nchi
kutoka dola za kimarekani 0.2 kwa tani hadi dola za kimarekani 0.5 kwa tani. Lengo
la hatua hii ni kuchochea uzalishaji wa mbolea nchini na kuongeza ajira. Hatua
hii pia inaendana na dhima ya Serikali ya kuchochea maendeleo ya viwanda hapa
nchini.
(iii) Wizara
ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Kuanzisha utaratibu wa kutoza ada ya shilingi 1,000 hadi 3,000 kwenye
ada ya matumizi ya king’amuzi kulingana na kiwango cha matumizi.
(iv)
Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Napendekeza kuanzisha tozo ya asilimia 1.5 kwenye
vifaa vinavyotumika kuzalisha, kusambaza, kudurufu na kutunza kazi za Sanaa,
uandishi na ubunifu mwingine kama vile muziki, filamu, vitabu, picha na aina
nyingine za kazi za ubunifu. Vifaa hivi
ni Radio/ TV set enabling recording;
Analogue audio recorders; Analogue video recorders; CD/DVD Copier; Digital
Jukebox na MP 3 Player.
Hatua hii
inatarajiwa kuongeza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni
9,600.
(v)
Shirika la Viwango Tanzania
Kupunguza
tozo ya kuthibitisha ubora wa shehena (Batch Certification Fee) za sukari zinazoingizwa
nchini kutoka shilingi 6 kwa kilo hadi shilingi 2.5 kwa kilo. Lengo la hatua
hii kupunguza gharama kwa waingizaji wa sukari nchini ili kutoa unafuu kwa
wananchi.
(vi)
Wakala
wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA)
Kufuta
tozo ya kipimio cha mzio (peak expiratory flow test fee) inayotozwa shillingi 10,000 na tozo ya
kipimo cha kilele (allergy test fee) inayotozwa shilingi 25,000. Pendekezo hili linatarajia kuchochea mazingira wezeshi ya
biashara nchini hususan katika maeneo ya viwandani.
(vii)Tume
ya nguvu za mionzi Tanzania
(a) Kupunguza ada ya Utambuzi wa Mionzi kutoka asilimia 0.2
ya Malipwani kwenda asilimi 0.1 ya Malipwani kwenye mizigo yote ya vyakula
inayosafirishwa nje ya nchi ikiwa pamoja na mbolea, tumbaku na bidhaa za
tumbaku na chakula cha msaada kinachoingizwa nchini. Lengo la hatua hii ni
kupunguza tozo kero na gharama za biashara na hivyo kuchochea mauzo ya bidhaa
nje ya nchi sambamba na kupunguza utoroshaji wa mazao hayo kwenda nchi jirani
kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi ; na
(b) Kufanya Maboresho ya ada na tozo mbalimbali zinazotozwa
na Tume ya Nguvu za Mionzi kama zilivyoainishwa kwenye kiambatisho Namba 7 ;
(viii) Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji
Napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Jeshi ya Zimamoto na
Uokoaji Sura 427 kwa kupunguza ada na tozo mbalimbali kama zilivyoainishwa
kwenye kiambatisho Namba 8. Lengo la hatua
hii ni kupunguza tozo kero na gharama za biashara.
(ix)
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Jedwali la viwango vya tozo na
ada la Kanuni za Michezo ya Kubahatisha chini ya Sheria ya Michezo ya
Kubahatisha Sura Na. 41 kama ilivyoainishwa kwenye kiambatisho Na 9.
(x)
Idara ya Uhamiaji
Mwaka wa fedha 2021/22 Serikali ilipitisha uamuzi wa kuondoa ada ya
kibali cha kuingia nchini (VISA/PASS FEE) kwa wanafunzi
wa elimu ya juu kutoka nchi ya Msumbiji kwa ajili ya Mpango wa
kubadilishana wanafunzi wa Elimu ya Juu baina ya Tanzania na Msumbiji (TAMOSE).
Pamoja na uamuzi huo, napendekeza kuondoa tozo ya vibali vya ukaazi kwa
wanafunzi wa elimu ya juu kutoka nchi ya Msumbiji. Lengo la hatua hii ni
kutekeleza matakwa ya makubaliano kati ya nchi hiyo na Tanzania kuondoleana
tozo hizo ambapo Msumbiji imeshaanza kutekeleza makubaliano hayo.
119. Mheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya maboresho ya Sheria
mbalimbali ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kupunguza
mwingiliano wa Sheria. Mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo:
(i)
Kufuta kifungu
cha 6(10) (b) (ii) na (iii) cha Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Na.
12 ili kuwa na viwango vya kitaifa (National Standards) kwa kuzingatia kifungu
cha 4(3) cha Sheria ya Viwango Na. 2. Lengo la hatua hii ni kufanya jukumu la
viwango vya kitaifa kubaki kwa Shirika la Viwango Tanzania pekee. Iwapo Mamlaka
ya Mawasiliano itakuwa na mahitaji ya viwango, itashirikiana na Shirika la
Viwango Tanzania;
(ii)
Kufuta kifungu
cha 7 (1) (b) (ii) na (iii) cha Sheria ya Udhibiti wa Nishati na Maji, SURA 414
ili kubakisha jukumu la viwango vya kitaifa kubaki kwa Shirika la Viwango
Tanzania pekee. Endapo kuna mahitaji ya viwango EWURA watawasiliana na Shirika
la Viwango Tanzania;
(iii)
Kufuta Kifungu
cha 5(1) (c) (i) na (ii) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu Na. 3 ili kazi ya viwango
ifanywe na Shirika la Viwango Tanzania. Mahitaji ya viwango ya LATRA
yatawasilishwa Shirika la Viwango Tanzania;
(iv)
Kufuta Kifungu
cha 5(2) (c) cha Sheria ya Pamba Na. 2 ya mwaka 2001 ili kubakiza jukumu la
viwango kwa Shirika la Viwango Tanzania. Mahitaji ya viwango vya Bodi ya Pamba
Tanzania yatawasilishwa Shirika la Viwango Tanzania;
(v)
Kufuta Kifungu
cha 12(1) (b) na (c) cha Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania Na. 14 ya mwaka 2017
ili jukumu la viwango vya kitaifa libaki kwenye Sheria ya Viwango Na. 2 ya
mwaka 2009. Mahitaji ya viwango ya TASAC yatawasilishwa Shirika la Viwango
Tanzania;
(vi)
Kufuta Kifungu
cha 5 (1) (l) cha Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 ili
jukumu la viwango vya kitaifa libaki kwenye Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka
2009. Mahitaji ya viwango ya TMDA yatawasilishwa Shirika la Viwango Tanzania;
(vii)
Kufuta Kifungu
cha 41 (1) cha Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 ili kazi
ya udhibiti wa machinjio ifanywe na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pekee;
(viii)
Kufuta Kifungu
cha 3(2) (g) cha Sheria ya Magonjwa na Wanyama Na. 17 ya mwaka 2003 ili chanjo
zisajiliwe na TMDA pekee;
(ix)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 10 cha Sheria ya Tasnia ya Maziwa ili Bodi ya
Maziwa iweze kufanya ukaguzi kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania;
(x)
Kufanya
marekebisho kwenye maginal note ya Kifungu cha 46 cha Sheria ya Hakimiliki na
Hakishirikishi ili kuondoa mgongano wa kimaslahi katika kutekeleza majukumu ya
Chama Cha Hakimiliki Tanzania. Aidha, napendekeza kuondoa neno “society” na kuweka neno “Copyright
Office” kwenye Kifungu cha 46, 47, 48 na jedwali lake;
(xi)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 51 cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishirikishi
ili kuongeza sehemu mpya ya saba (PART VII) inayoweka hitaji la Collective
Management Organisations kutoa taarifa ya hesabu zao zilizokaguliwa kwa
Copyright Office kila mwaka na hivyo kuwa na uwajibikaji na kuimarisha
usimamizi wa masuala yanayohusu Hakimiliki na Hakishirikishi;
(xii)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Tasnia ya Pamba SURA 201 ili
jukumu la kusimamia viwango vya pamba lifanywe na Shirika la Viwango Tanzania pekee;
(xiii)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 23 cha Sheria ya Utalii SURA, 65 ili kumpa
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii mamlaka ya kutoa vibali baada ya kuridhiwa na
Bodi;
(xiv)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 28 cha Sheria ya Mbolea SURA, 378 ili jukumu la
kuandaa kanuni za viwango litekelezwe na Shirika la Viwango Tanzania pekee;
(xv)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 17 cha Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi,
SURA 297 ili kuweka sharti la OSHA kutoa leseni ndani ya siku 7 baada ya
mwombaji kukidhi vigezo;
(xvi)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 35 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Urban
Authority) SURA, 287 ili kuweka sharti la Mamlaka za Miji kuanzisha vituo vya
pamoja kwa ajili ya uratibu, uhamasishaji na uboreshaji wa mazingira ya
ufanyaji biashara;
(xvii)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 113 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (District
Authorities) SURA 288 ili kuweka kuweka sharti la Mamlaka za Vijiji kuanzisha
vituo vya pamoja kwa ajili ya uratibu, uhamasishaji na uboreshaji wa mazingira
ya ufanyaji biashara;
(xviii)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 6, 7, na 8 cha Sheria ya Mamlaka ya Serikali za
Mitaa SURA, 290 ili kupunguza kiwango cha tozo ya kitanda siku (hotel levy)
kutoka asilimia 10 hadi asilimia 5; na
(xix)
Kufanya
marekebisho kwenye Kifungu cha 3 cha Sheria ya Ngozi na Bidhaa za Ngozi SURA,
120 ili kuondoa mkanganyiko uliopo kati ya ngozi za wanyama wa majumbani na za
wanyama pori.
(p) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria
za Kodi na Sheria nyingine mbalimbali.
120. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho mengine madogo
madogo yasiyo ya kisera katika sheria mbalimbali za kodi pamoja na sheria
nyingine ili ziwe sanjari na azma ya kurahisisha utekelezaji wake. Marekebisho
hayo yataainishwa katika Muswada wa Sheria
ya Fedha ya mwaka 2022 na Matangazo ya Serikali (Government Notices).
121. Mheshimiwa Spika, sambamba na hatua zilizobainishwa hapo juu,
napendekeza kutoa tamko la biashara ya bima nchini kufanywa kwa ushindani kwa
kufuata misingi ya soko huria kama ilivyo kwa biashara nyingine na kuyaelekeza
mashirika ya bima yanayomilikiwa na Serikali ambayo ni Shirika la Bima la Taifa
(NIC) na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kufanya
biashara kiushundani kwa kutoa huduma bora tofauti na maelekezo yaliyopo
sasa yanayoipatia NIC pekee fursa ya kupata biashara kutoka kwenye Taasisi za
Umma.
(q) Tarehe
ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi.
122. Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kikodi zinazopendekezwa zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai,
2022, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo.
VI.
SURA YA BAJETI KWA MWAKA 2022/23
123. Mheshimiwa
Spika, Sura ya Bajeti kwa mwaka
2022/23 inaonesha kuwa jumla ya shilingi trilioni 41.48 zinatarajiwa kukusanywa
na kutumika. Jumla ya mapato ya ndani yanatarajiwa kuwa shilingi trilioni
28.02, sawa na asilimia 67.5 ya bajeti yote. Kati ya mapato hayo, mapato
yatakayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania yanakadiriwa kuwa shilingi
trilioni 23.65 na mapato yasiyo ya kodi (Wizara, Idara, Taasisi na Mamlaka za
Serikali za Mitaa) yanakadiriwa kuwa shilingi trilioni 4.37.
124. Mheshimiwa
Spika, misaada na mikopo nafuu
kutoka kwa Washirika wa Maendeleo inatarajiwa kuwa shilingi trilioni 4.65, sawa
na asilimia 11.2 ya bajeti yote. Aidha, Serikali inatarajia kukopa
shilingi trilioni 5.78 kutoka soko la ndani ambapo shilingi trilioni 3.30 ni
kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoiva na kiasi cha
shilingi trilioni 2.48 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.
Vilevile, Serikali inatarajia kukopa shilingi trilioni 3.03 kutoka soko la nje
kwa masharti ya kibiashara kwa lengo la kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi
ya maendeleo.
125. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2022/23,
Serikali inapanga kutumia jumla ya shilingi trilioni 41.48 kwa matumizi ya
kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 26.48 zimetengwa
kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni asilimia 63.8 ya bajeti yote,
ikijumuisha shilingi trilioni 11.31 kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali na
gharama nyingine za Mfuko Mkuu na shilingi trilioni 9.83
kwa ajili ya mishahara ikiwemo nyongeza ya mshahara, upandishaji wa madaraja
kwa watumishi na ajira mpya. Aidha, shilingi trilioni 5.34 ni kwa ajili ya
matumizi mengineyo (OC) ikijumuisha shilingi bilioni 200.0 kwa ajili ya kulipa
madeni yaliyohakikiwa ya watumishi na wazabuni.
126. Mheshimiwa Spika,