Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi akizungumza na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mpanda, Jeff Shantiwa, baada ya kuwasili Mkoani Katavi kwa ziara ya kikazi.



Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika, Manga Gassaya, akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kulia) kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa gati katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea ujenzi wake Mkoani humo. Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Usafiri Majini- Sekta ya Uchukuzi, Mussa Shashula.



Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Interconsult ltd, Elisante Urassa akifafanua kwa Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi (kulia), kuhusu hatua iliyofikiwa ya eneo la kuwekea mizigo katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi, wakati Naibu Katibu Mkuu huyo alipotembelea ujenzi wake.



Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya Jengo la Abiria katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi. Mradi wa bandari hiyo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 30 kwa sasa umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.



Naibu Katibu Mkuu-Uchukuzi, Dkt. Ally Possi, akitoa Maelekezo kwa Meneja Bandari za Ziwa Tanganyika, Manga Gassaya (mwenye kaunda suti nyeusi). wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa Bandari ya Karema Mkoani Katavi.



Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya Jengo la mizigo katika Bandari ya Karema Mkoani Katavi. Mradi wa bandari hiyo huo unatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu na umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 30.



Muonekano wa gati jipya katika bandari ya Karema Mkoani Katavi, kukamilika kwa gati hiyo kutaruhusu meli zenye urefu wa mita 150 na upana wa mita 15. Mradi wa upanuzi wa bandari hiyo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika mwezi julai mwaka huu.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...