Mkuu wa kitengo cha Cha uendeshaji Equity Bank Tanzania ndugu Rojas Mdoe Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya KARIBU MEMBA
Baadhi ya wafanyakazi  wa Equity Bank wakishiriki katika uzinduzi wa kampeni mpya ya Karibu memba.

Na Shikunzi oscar, Michuzi Tv
WAKULIMA nchini wameshauriwa Kujiongezea uelewa wanamna ya kutunza fedha zao kupitia kampeni ya KARIBU MEMBA iliyozinduliwa na benki ya equity

Ni katika jitiada za kuwainua wakulima nchini ambapo Benki ya Equity kwa kushirikiana na taasisi za kutoa pembejeo YARA NA AGRICOM ambezindua kampeni ya karibu memba itakayokuwa msaada kwa wakulima katika maswala ya kifedha.

Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji Benki ya Equity, Rojas Mdoe akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Equity Benki, Isabel Maganga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya KARIBU MEMBA ambayo imezinduliwa kwaajili ya kuanza kusherehekea miaka 10 ya utoaji huduma kwa watanzania, Mdoe amesema ndani ya miaka kumi Benki ya Equity imeweza kutoa ajira kwa watanzania zaidi ya 430 na kubadilisha maisha ya watanzania zaidi ya 500,000 kiuchumi na kijamii.

"Tunahudumia watanzania zaidi ya laki tano mpaka sasa na tunategemea kuongeza zaidi lakini pia tumehudumia kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa wafanyabiashara wadogowadogo wakiwemo wakulima, kutoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwa ni pamoja na utunzaji wa fedha, akaunti za watoto, vikundi, mikopo mbalimbali kama ya wakulima, wastaafu, wafanyabiashara kubwa na ndogondogo, waajiriwa n.k"

Katika hatua nyingine Mdoe amesema katika kuunga mkono serikali kuhakikisha wanaipa nguvu sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi wa nchi, hivi karibuni waliweza kuzindua mradi na taasisi mbalimbali kwaajili ya mikopo ya wakulima.

Aidha Mkuu huyo wa kitengo wa Benki ya Equity alisema mikopo yao ina riba nafuu ambayo inatolewa katika ngazi zote za kilimo, kwa mkulima anaelima mwenyewe, kwa yule anaesambaza pembejeo, anaeingiza pembejeo na anaenunua mazao;

"Mikopo yetu ya kilimo riba yake ipo kuanzia 8% mpaka 15% kulingana na ngazi katika mnyororo wa thamani lakini pia uwezo wa yule anaekopeshwa na uwezo wake wa kifedha wa kuweza kuhudumia lakini pia uzalishwaji wake kwasababu riba ni sehemu ya mchango katika uzalishaji wa mkopeshwaji."

Mkuu huyo wa kitengo alisema, Miongoni mwa changamoto zilizopo katika sekta ya kilimo ni umilikaji wa mali na utambulisho hivyo amewashauri watengeneze vikundi ili kuwa rahisi kwa Benki kuwatambua.

Hata hivyo Benki Equity imejikita katika kutatua changamoto za wananchi na itaendelea kutoa elimu na fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki kwa Memba wa Tanzania na Dunia kwa ujumla

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...