Na. Catherine Mbena/TARANGIRE

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), ilikagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi ya uboreshaji wa miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Tarangire ambapo ukarabati wa barabara, viwanja vya ndege pamoja na ununuzi wa mitambo umefanyika kupitia Mradi wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa miradi hiyo tarehe 29.06.2022 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA,Jenerali (Mstaafu). George Waitara aliipongeza Menejimenti ya Hifadhi za Taifa kwa kazi nzuri ya usimamizi wa miradi hiyo

“Naona tupo vizuri na tuendelee kufanya kazi kwa kujituma zaidi ili kama kuna fungu jingine nina hakika ni rahisi kupewa.Simamieni kwa umakini mkubwa hii miradi ili iwe na ubora uliokusudiwa kulingana na thamani ya pesa ilivyotumika alisema Waitara

Naye, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Kamishna Nsato Marijani alipongeza kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati huku ikizingatia thamani ya pesa

“Kukamilika kwa wakati kwa miradi hii ni kazi kubwa sana imefanyika, kiwango cha kazi kinalingana na thamani ya pesa, hii ni dhahiri kwamba kuna usimamizi mzuri wa miradi”

Awali, akiwakaribisha wajumbe wa bodi katika Hifadhi ya Taifa Tarangire Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, William Mwakilema alibainisha umuhimu wa miundombinu hiyo katika ustawi wa utalii nchini ambapo kwa muda mfupi Hifadhi imeshuhudia ongezeko kubwa la wageni.

Bodi ya wadhamini wa TANAPA inaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya uboreshaji miundombinu katika Hifadhi za Taifa Mkomazi na Kilimanjaro.







 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...