WANANCHI Wilayani Meatu mkoani Simiyu wameendelea kulalamika kuwepo kwa Wanyama aina ya Tembo ambao wanaendelea kuwasumbua Wananchi hao katika makazi yao na kutafuna Mazao yao mbalimbali katika maeneo yao ya Kilimo.
Akizungumza na Wananchi hao Wilayani humo, katika Kata ya Mwandu Itenje, katika Jimbo la Kisesa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo ametoa mwezi mmoja kwa Watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha wanatatua kero hiyo kwa Wananchi hao ambao hapo awali waliwahi kulalamika kuhusu kero hiyo.
Chongolo amesema anaenda kutoa taarifa ya kero hiyo kwa Wizara hiyo ili Wananchi hao wa Meatu kupata unafuu na kuepukana na Wanyama hao ambao wamekuwa kero kubwa kwao.
“Nawahakikishia ndani ya Wiki Nne, lazima Viongozi wa Wizara ya Maliasili waje hapa, wawaambie hatua wanazochukua katika kukabiliana na changamoto ya Tembo kwenu ninyi Wananchi”, amesema Chongolo.
“Tunajua Rais aliagiza kuchukuliwa hatua za haraka kutatuliwa changamoto hii, na hatuwezi kuwa na watu wanaogizwa na Mamlaka kuja kuchukua hatua kwa ajili ya maslahi ya Wananchi, huku wao wanaendelea kukaa bila kutekeleza maagizo wanayopewa”, ameeleza.
Pia amesema CCM ni Chama kinachosimamia Serikali hivyo itaendelea kutatua changamoto za Wananchi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha Wananchi hao wanaendelea kukaa vizuri katika maeneo yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila amesema tayari amefanya mawasiliano na timu ya watu 10 kutoka Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) wamefika katika Wilaya hiyo kukabiliana na Wanyama Tembo.
“Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA) wameanza kusambaza vikozi vya kuzuia Wanyama Tembo wanaosumbua katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo hili la Meatu”, amesema Kafulila.
Pia amesema wanaheshimu Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ni Chama kinachosimamia Serikali, amesema wao kama Viongozi hawati kuharibu vibarua vyao kwa sababu ya kero mbalimbali wanazokutana nazo Wananchi katika maeneo wanayoongoza, hivyo amesema hakuna budi kutatua kero hizo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wakazi wa shina namba 1 Mwandu Itinje wilayani Meatu mkoa wa Simiyu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...