Na Khadija Kalili, Pwani
HAYAWIHAYAWI sasa yamekuwa ambapo kesho majira ya saa kumi alasiri katika Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani timu ya maafande wa Ruvu Shooting itashuka dimbani kukipiga na wageni wake Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.

Wenyeji hao wa Ruvu Shooting walizungumza kuhusu kuhusu mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambapo unatarajiwa kuwa wa kufa ama kupona.

Kocha Msaidizi kutoka timu ya Ruvu Shooting, Frank Msese amesema kuwa licha ya timu hiyo kupoteza michezo yake mitatu na kwamba hiyo haitoi picha nzuri lakini anapenda kuwahakikishia wapenzi na mashabiki kuwa katika mchezo wa kesho hawatapoteza nafasi yao huku akisema kuwa kesho watacheza kitofauti.

Aidha Kapteni wa timu ya Ruvu Shooting Renatus Kisase amesema kuwa wanaamini kuwa mechi yao ya kesho (Jumatano) itakuwa mechi ngumu huku amesisitiza kuwa itakuwa sawa na kucheza fainali na kutoa ahadi ya kuibuka na ushindi.

"Kuhusu mchezo wa kesho ni muhimu na utaamua nani apande na nani ashuke daraja tunaithamini sana mechi ya kesho na tunatambua ubora na udhaifu wa Tanzania Prisons" alisema Kapteni huyo Ruvu Shooting.

Kwa upande wa timu ya Tanzania Prisons Kocha Shabani Mtupah amesema kuwa maandalizi yanatofautiana na benchi la ufundi ni lingine hivyo vijana wake watacheza kabumbu kwa maarifa zaidi ya ilivyozoeleka.

"Kesho tutashinda kwani hii ni mechi yetu ya fainali na tunajua kesho lazima mshindi apatikane tunaimani kesho vijana watafanya vizuri kwani wachezaji wote wako vizuri" alisema Kocha huyo.

Wakati Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) ambaye pia ni Msimamizi wa Kituo Mohammed Masenga amesema kuwa maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na muamuzi ni dakika 90 huku akitoa hamasa kwa wakaazi wa Mkoa wa Pwani na viunga vyake wajitokeze kwa wingi Ili kuipa hamasa timu inayobeba Mkoa.
Kocha Msaidizi kutoka timu ya Ruvu Shooting, Frank Msese akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Pwani leo Juni 28,2022.
Kutoka Kushoto ni Msimamizi wa Kituo Mohammed Masenga, katikati ni Mwalimu Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shabani Mtupah na Kapteni wa timu hiyo Benjamin Asukile

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...