Na Pamela Mollel,Arusha
Mkuu
wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda amewafunda wastaafu watarajiwa mkoani
hapa,kufanya matumizi sahihi ya fedha za mafao yao pindi wanapolipwa na
kuacha kujiingiza kwenye starehe na kununua magari mabovu badala yake
wajikite katika kuanzisha miradi vijijini au kuwekeza hisa kwenye
mabenki
Pia
aliwashauri kurudi kijijini kuanzisha miradi ya kisasa ya kilimo
,ufugaji na viwanda vidogo hatua itakayosaidia kunufaika na mafao yao
kuliko kukimbilia kununua magari mabovu ya biashara au kujenga nyumba ya
kupangisha jambo litakalopelekea kutapeliwa na kujikuta wakifilisika.
Kauli
hiyo ameito wakati akifungua semina ya siku mbili ya wastaafu na
wanachama wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF , wapatao 300,semina
iliyolenga kuwajenga kisaikolojia, ambapo pia aliwashauri kuhakikisha
wanawekeza kwa kununua hisa kwenye mabenki na kujiweka salama na fedha
zao.
Alisema
kumekuwepo na tabia inayojitokeza kwa wastaafu pindi wanapolipwa mafao
yao ambapo baadhi yao hujiingiza kwenye starehe na kuona vibinti vidogo
ambao huwaibia fedha zao na muda mfupi huishiwa na kubaki wakihangaika
hapa mjini.
Aliwataka
wastaafu hao kutoogopa maisha mapya bali wazingatie kazi na matumizi
sahihi ya fedha watakazolipwa kwa kwenda kuanzisha miradi vijijini au
kuwekeza kwenye hisa kwenye benki
" Epukeni starehe za kuoa mabinti wadogo watakaowaponza na kufilisika au kwenda kununua magari mabovu ya biashara"alisema
Alisisitiza
kuwa dhana ya kukimbilia kununua Magari ya biashara hususani Coaster ni
ushauri mbovu kwa sababu wengi wao wanashauriwa bila kuwa na utaalamu
wa biashara hiyo ,epukeni uwekezaji usio sahihi.
Awali
meneja usimamizi wa mafao kutoka NSSF Taifa,James Galusoigo alisema
semina hiyo inalenga kuwaanda wastaafu watarajiwa wanaokaribia kustaafu
wenye umri kati ya miaka 55 hadi 60 ili kuhakiki kumbukumbu zao mapema
baada ya ujio wa mfumo wa NIDA ili kuepuka kucheleweshewa mafao yao.
Alisema
kuwa NSSF imefanya mabadiliko makubwa katika mfumo wake wa malipo
ambapo mstaafu aliyekamilisha vema kumbukumbu zake atapokea mafao yake
ndani ya mwezi mmoja baada ya kustaafu.
Kwa
upande wake Josephat Komba meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha,alisema semina
hiyo ni fursa nzuri kwa wastaafu katika kuwajengea uwezo juu ya
matumizi sahihi ya mafao yao .
Alisema
washiriki wa semina hiyo ni wanachama wa mfuko wa NSSF kutoka kampuni
na taasisi mbalimbali mkoa wa Arusha ambao wanatarajiwa kustaafu hivi
karibuni
Alitoa
wito kwa waajiri kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao
kwa wakati ili kuepuka ucheleweshaji wa malipo ya mafao pindi
wanapostaafu.
Baadhi
ya washiriki wa semina hiyo Issa Mohamed au Onyango Kanindo msanii
mchekeshaji,Steven Mwilolezi na Justine Lyela walisema semina hiyo
imekuja wakati mwafaka kwani itasaidia sana kuwaanda wastaafu
kisaikolojia ambao wengi wao wamekuwa wakitapeliwa mafao yao na kujikuta
wakiadhilika na kuwa ombaomba.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Said Mtanda akizungumza na wastaafu watarajiwa
kuhusu fedha za mafao pindi wanapolipwa kufanya matumizi sahihi ya fedha
hizo
Mchekeshaji maarufu hapa nchini Onyango Kanindo akizungumza na waandishi wa habari
Meneja wa NSSF Mkoa wa Arusha Josephat Komba akizungumza katika semina hiyo
Mstaafu mtarajiwa Steven Mwilolezi akizungumza na waandishi wa habari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...