Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tarehe 20.06.2022 Imegawa pikipiki 22 kwa maafisa Ugani ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Hafla fupi ya Ugawaji pikipiki, imefanyika katika Viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, na Mgeni Rasmi alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas akiwa akiwa ameambatana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Nyasa.

Akikabidhi Pikipiki hizo, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa kutatua Changamoto za usafiri kwa maafisa kilimo, kwa kuwa walikuwa wanachangamoto kubwa ya usafiri lakini kwa sasa amewataka, maafisa hao kufanya kazi kwa bidii na kuacha visingizio kwa kuwa wameshapewa usafiri hivyo wahakikishe wanatatua changamoto za wakulima na kuongeza tija hasa katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Aidha amewataka kuzitunza pikipiki hizo na kuhakikisha wanazitumia kwa maslahi ya wakulima wa Wilaya ya Nyasa na hatimaye kutengeneza utofauti kipindi hawana usafiri na sasa, baada ya kupata usafiri hasa katika kuongeza Uzalishaji wa Mazao.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Nyasa Crodivic Duwe amewataka maafisa ugani kuongeza ari ya kufanya kazi kwa kuwa serikali imewapa motisha ya usafiri hivyo kwa kuwa Wilaya yetu ni ya kilimo waongeze uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Awali akitoa Taarifa Fupi, Mkuu wa Idara Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Pasifiki Mhapa ameishukuru Serikali, kwa kutatua Changamoto ya Usafiri kwa maafisa Kilimo Nchini, kwa kuwa walikuwa wakishindwa kuwafikia wakulima wengi ipasavyo, lakini kwa sasa wanaenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo kwa kuwa kwa sasa watakuwa na uwezo wa kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Maafisa kilimo waliopewa pikipiki wamesema watazitunza pikipiki na kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuwa awali walikuwa na changamoto ya usafiri kwa sasa watafanya kazi kwa bidii na kuwafikia wakulima wengi zaidi. 



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...