Makani Mkuu wa Chuo cha DMI akiwa na timu kutoka DMI tayari Kwa maonyesho ya NACTVET katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma.Mhe. Jumanne Kishimba, Mbunge wa Kahama Mjini atembelea banda la DMI.Bi. Winfrida Ngallu, mwanafunzi wa Marine Engineering, mwaka wa tatu akitoa elimu kuhusiana na taaluma ya ubaharia.Capt. Azan Azan kutoka chuo cha DMI akitoa elimu ya kujiokoa wakati wa dharula melini.Umati wa wananchi umefurika katika banda la DMI wakipatiwa elimu ya bahari.Watumishi kutoka chuo cha DMI wakijioanga kutoa huduma Kwa wananchi katika viwanja vya Jamhuri - Dodoma.

Prof. Zacharia Nganilo, Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji (NIT) atembelea banda la DMI.

*****

MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam Dkt. Lucas Mwisila ametoa wito kwa umma wa Tanzania kujiunga na Chuo hicho kutokana na fursa zilizopo katika tasnia ya bahari.

Dkt. Mwisila amesema Kwa sasa dirisha la udahili lipo wazi kwa ngazi ya Cheti na Diploma, hivyo anawakaribisha watanzania na wasio watanzania kujiunga na chuo cha bahari Dar es Salaam.

Chuo cha bahari dar es Salaam kinatoa kozi za ubaharia zikiwemo Uendeshaji wa meli (Unahodha), Uhandisi wa meli, Usimamizi wa masuala usafirishaji na lojistiki, Uhandisi wa mafuta na gesi na nyingine nyingi ambazo zinatolewa Kwa ngazi ya Cheti, diploma, digrii na Uzamili.

Aidha chuo kinatoa kozi fupi pamoja na kozi za umahiri kuhusiana na tasnia ya bahari.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kozi zitolewazo na chuo cha DMI unaweza kutembele tovuti ya chuo www.dmi.ac.tz au unaweza kupiga simu 0688 941 921/ 0716 898 037

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...