Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Shirikisho la Soka duniani (FIFA) limeifungia Klabu ya Geita Gold FC inayoshiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara kusajili Wachezaji hadi itakapomlipa Aliyekuwa Kocha wake Mkuu, Etienne Ndayiragije anayedaiwa kudai malipo yake ya fidia ya kuvunjiwa mkataba na malipo mengine wakati akiifundisha timu hiyo.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) imeeleza kuwa kwa mujibu wa taratibu za FIFA endapo Geita Gold FC itakuwa haijamlipa Etienne suala hilo litawasilishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya FIFA kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.
TFF imeendelea kuzikumbusha Klabu za Soka nchini kuheshimu mikataba ambayo inaingia na Wachezaji na Makocha kutokana na vigezo vya kupata Leseni ikiwa ni utekelezaji wa Kanuni ya Leseni za Klabu (Clubs Licensing Regulations).
Kocha Etienne Ndayiragije aliwahi kuifundisha Klabu ya Geita Gold FC ya Geita ambayo inashiriki Ligi Kuu Soka Tanzania Bara msimu huu wa 2021-2022 kabla ya kufutwa kazi kutokana na matokeo yasiyoridhisha ambapo nafasi yake alichukua Kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...