Idadi ya wakazi wanaojiandikisha kuhama kwa hiyari kutoka katika hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kuongezeka, huku awamu ya pili ya kuwahamisha wananchi walio tayari kuhama kwa hiyari ikitarajiwa kuanza Alhamisi wiki hii.
Wananchi wa jamii ya Watatoga nao wamesema wamehamasika na wapo tayari kuondoka katika kata ya Eyasi na kwenda kuishi Msomera mkoani Tanga, ili kupisha uhifadhi.
Diwani wa Viti maalum kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) Veronica Gitida amejitokeza kujiandikisha kuhama katika eneo hilo kwa hiyari na kisha kuwataka wananchi wengine wajitokeze kuunga mkono jitihada za serikali za kulinda maeneo ya uhifadhi.
"Mimi ni kiongozi wa wananchi hapa, lakini nimekubali kuhama kwa hiyari yangu kupisha shughuli za uhifadhi ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro." amesema Veronica
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti Jamii ya Watatoga Tanzania, Augustino Ginada namesema kuhama katika eneo la hifadhi ni jambo ambalo litawainua kimaendeleo, kwani wataweza kumiliki ardhi na nyumba za kisasa.
Awamu ya pili ya kuwahamisha wananchi wanaoishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro inatarajiwa kuanza Alhamisi wiki hii, ambapo kaya 24 zinatarajiwa kuhamia katika kijiji cha Msomera, wilayani Handeni mkoa wa Tanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...