Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Masasi

WANANCHI wa Kitongoji cha Chiwata wilayani Masasi Mkoani Mtwara wamesema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ,wameomba changamoto zinazokabili ikiwemo ya ubovu wa barabara, kukosa umeme na uhaba wa maji zikapatiwa ufumbuzi.

Wametoa maombi hayo leo Juni 3,2022 wakiwa kwenye mkutano wa Shina wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi kufika kwenye kitongoji hicho na kutoa nafasi ya kusikiliza kero za wananchi.

Hivyo Wananchi waliopata nafasi ya kuzungumza wametumia nafasi hiyo kueleza kwamba wanafurahishwa na kazi ya utekelezaji miradi ya maendeleo inayofanywa na Rais Samia na wanamshukuru kwa namna anavyoendelea kuwatumikia Wana Masasi huku wakiamini changamoto zilizopo zitapatiwa ufumbuzi.

Wananchi hao wamesema kuwa katika Kijiji chao barabara imekuwa mbovu na imefungwa wakati barabara hiyo imebeba uchumi wana Chiwata, hivyo wameomba ifunguliwe.Pia wametoa kilio chao kuhusu changamoto ya uhaba wa maji na hivyo kuomba kuharakisha kwa mradi wa maji ambao ujenzi wake unaendelea kukamilika.

Wakati changamoto nyingine ambayo wameileza ni kukosa umeme kwenye kitongoji chao.Hata hivyo pamoja na kutoa changamoto hizo wamemhakikishia Shaka kuwa wao wataendelea kuwa watiifu na waaaminifu kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwani wamekuwa na matumaini nayo makubwa hasa kutokana na Rais Samia kuonekana amedhamiria kutatua changamoto za wananchi.

Akizungumzia baada ya kusikiliza changamoto hizo Shaka amesema amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ya CCM itaendelea kuzitafutia ufumbuzi wa haraka."Nataka niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan yupo pamoja na ninyi.

"Nataka niwahakikishie sisi ndio tuliokuja tukaahidi kwenu katika kipindi cha 2020-2025 tutahakikisha tunatatua shida zenu, changamoto zote za kimsingi kupitia Ilani ya CCM tutazitatua.Diwani, Mbunge na Rais wote wamebeba dhima hiyo, na sisi kama Chama ndio tumekuja sasa kuwasikiliza ninyi wananchi ili kuona hizi changamoto wapi zinakwama.

"Tumeambiwa uchumi wa hapa (Chiwata) unategemea barabara hii, lakini imefungwa sababu za msingi hakuna tumetoa maelekezo barabara ifunguliwe na kama kuna shida yoyote TARURA wapo watafanya ukarabati ili ipitike, kubwa tunachohimiza kwenu ni ushirikiano na serikali katika suala zima la usalama.

"Tukubaliane wananchi lazima muwe sehemu ya kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili amani iliyopo iendelee kuwepo, maadui wasioitakia mema nchi yetu, wasioitakia mema Mtwara wazidi kubainika na hatua kiusalama zichukuliwe, nyie wote mnajua Mkoa huu unachangamoto za kiusalama.

Pamoja na maelezo hayo ya Shaka bado aliamua kutoa nafasi kwa viongozi aliokuwa ameambatana nao akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya Masasi pamoja na wakuu wa Idara wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Masasi.

Wakati wakitoa ufafanuzi wa baadhi ya changamoto wameahidi kuzitafutia ufumbuzi kwani Serikali ya Awamu ya Sita ipo kazini na inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero zilizopo.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwasalimia wanafunzi wakiwemo wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika Shule ya Sekondari Chidya, aliposimama kusalimia wanafunzi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akiwasalimia wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanaosoma katika Shule ya Sekondari Chidya, aliposimama kusalimia wanafunzi akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, akimsikikiza mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu wa kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Chidya, Said Mwanyaba akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. (Picha zote na Fahad Siraji wa CCM).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...