NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MAAFISA
Kazi nchini wameaswa kuwa waadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao, Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Jamal Katundu amesema mjini Morogoro Juni
18, 2022 wakati akifungua kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
(WCF) na Maafisa Kazi nchini chenye lengo la kuwajengea uelewa wa maboresho ya sheria
ya fidia kwa wafanyakazi.
“Nichukue
nafasi hii kuwakumbusha kwamba uadilifu ni jambo la msingi sana katika kazi
zinazofanywa katika Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake ninyi
mkiwemo,hakikisheni taarifa za ukaguzi zinakuwa za kweli na sahihi msiingie kwenye vishawishi”
alisema
Alisema
Maafisa Kazi nchini ni mabalozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, na wanapaswa kuwa na
uadilifu wa hali ya juu, WCF ipo Ofisi ya Waziri Mkuu hivyo wanapaswa
kutekeleza majukumu yao ili kuweka heshima ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Aidha
Kamishna Mkuu Idara ya Kazi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Suzan Mgangwa amesema
idara yake na WCF zimeazimia kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kulinda
mfanyakazi nchini wanapopata majanga wakati wakitekeleza majukumu yao.
Akizungumza
mwanzoni mwa kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini WCF, Bi. Rifai
Mkumba alibainisha kuwa katika muktadha wa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma
za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Bodi imeendelea kusisitiza umuhimu wa Mfuko
kuendelea kutoa elimu kwa wadau ikiwa ni pamoja na taasisi mbalimbali hususan
za serikali wakiwemo Maafisa Kazi ili kukuza uelewa kuhusu masuala ya fidia
ikiwemo huduma mpya kama zilivyoboreshwa na serikali.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma
alisema lengo la kikao kazi hicho ni kujengeana uwezo ili kuwa na uelewa wa
pamoja.
“Mabadiliko
ya kisera, mabadiliko ya kisheria na kanuni na mabadiliko ya kiutendaji
yaliyotokea kwenye mifumo ambayo inatumika kwenye utekelezaji wa shughuli za
Mfuko kwa hiyo kikao hicho kitasaidia kuona maendeleo ya mabadiliko hayo.”
Alisema Dkt. Mduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...