*Asema dhamira ya Rais Samia kumtua ndoo mama kichwani iko pale pale

Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Tandahimba

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema changamoto ya upatikanaji maji kwa wananchi wa Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara ni kubwa lakini Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inakwenda kumaliza changamoto hiyo.

Shaka ametoa kauli hiyo leo Juni 4,2022 wilayani Tandahimba mkoani Mtwara baada ya kupokea kilio cha wananchi kuhusu changamoto ya maji ambayo wamekuwa wakiipata kwa muda mrefu.Kilio hicho kimethibitishwa pia na viongozi wa Wilaya hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ambao wamesema upatikanaji maji ni asilimia 15 ndani ya Wilaya hiyo ambayo ndogo sana.

Akizungumza baada ya kupokea kilio cha changamoto ya maji Wilaya ya Tandahimba,Shaka amesema katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ibara ya 100 waliahidi katika kipindi cha miaka mitano Serikali watakayoiunda moja ya kazi kubwa itaikayofanya ni kumtua ndoo mama kichwani ,lakini wamewahakikishia watanzania kwamba watapunguza changamoto ya maji mpaka asilimia 80 ifikapo mwaka 2020/2025.

"Tandahimba upatikanaji wa maji ni asilimia 15 ni hali inayosikitisha sana, mwito wangu kwa Wizara ya Maji kuangalia sana maeneo ya vijijini changamoto hii ni kubwa ,kilio kwa wananchi ni kikubwa , upatikanaji wa maji safi na salama lazima uendane na kasi ya mahitajio ya wananchi tuliyonayo hivi sasa.Changamoto hii ya kwamba wananchi wanasubiri mvua mpaka mvua ndio wawe na uhakika wa maji kwa kweli haifurahishi.

"Na kwa kweli sisi kama Chama hatuungi mkono jambo hilo, tutakwenda kuzungumza na watu wa Wizara ya Maji waitazame kwa jicho la pekee Wilaya hii ya Tandahimba ,hali hii inasikitisha sana , Mheshimiwa Rais samia Suluhu Hasan kabla ya kuwa ya Rais alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ajenda moja aliyoibeba kwa wakati ule ilikuwa ni kumtua ndoo mama kichwani na alifanya vizuri kwenye ajenda ile .

"Nataka niwahakikishie kwamba Rais Samia bado suala la kumtua mama ndoo kichwani liko kwenye akili yake, halali anawaza na kufikiria namna gani atamaliza changamoto hii ya maji kwa Watanzania. Chama kimekuja hapa nataka niwahakikishie Wana Tandahimba , Chama tunalichukua jambo hili na tukitoka hapa katika yooote kwa kutambua maji ndio uhai, maji ndio uchumi wana Wana Tandahimba , kwasababu huwezi kujenga uchumi bila kuwa na maji safi na salama.

"Chama tunalichukua hili na tunawahakikishia tunakwenda kubanana na watu wa Wizara ya Maji ili mradi huu mkubwa wa Maji Mitema uweze kukamilika haraka iwezekanavyo.Kwanza watueleze sababu za msingi za mkwamo wa mradi ule ,muda ni mrefu tangu mwaka 2018 mpaka leo mradi haujakamilika,"amesema Shaka.

Ameongeza kukwama kwa mradi ule ni kufifisha juhudi na jitihada za wananchi wa Wilaya ya Tandahimba kujikwamua na mkwamo huu wa kuondosha umasikini."Nataka niwahakikishie Rais Samia yuko pamoja na ninyi na ndio maana amekielekeza Chama kuja kuwasikiliza, nini shida yenu na nyie mmetueleza.

"Nataka niwaahidi yote mliyotueleza tunayachukua na wala hii sio siasa , tunafanya kazi ambayo tumetumwa na Watanzania, tumetumwa na wana Tandahimba.Dhamira yetu Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) inayoongozwa na Rais Samia ni njema sana kwa Watanzania ,changamoto nyingine zote namkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba na bahati nzuri tulikuwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara tangia tumeanza ziara yetu.

"Lakini katika la Maji Tandahimba kuna jambo kubwa la dharura limetokea ,tayari Mkuu wa Mkoa amekwdenda kushuhudia akiwa na Mwenyekiti wa CCM utiwaji saini wa mkataba wa maji ambao unakwenda kumaliza changamoto hii.Inakuja neema kwa wana Mtwara kaeni mkao wa kula.

"Na hayo yote ni mapenzi mema ya Rais Samia Suluhu Hassan ndio maana amewaita viongozi wetu wa Mkoa huu Dodoma kwenda kuwabidhi neema ya Wana Mtwara , kwa hiyo muda sio mrefu mambo yatafunguka katika Mkoa huu wa Mtwara . Nikiri yawezekana hapo katikakati mliihisi kwamba mko wapweke,"amesema Shaka.

Amefafanua uwepo wa Rais Samia Suluhu Hassan Mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa iliyopewa kipaumbele na ndio maana mkla Mkoa huo peke yake umepewa Sh.bilioni 13.6 kwa ajili ya miradi ya maji."Sasa tunafuatilia fedha na thamani ya fedha hizo iendane na matokeo ya upatikanaji wa huduma."

"Narejea tena thamani hiyo kubwa iendane na matokeo ya upatikanaji wa huduma , narejea tena tutasimamia fedha fedha zinazotolewa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ili kuhakikisha hakuna ubabaishaji, hakuna mkwamo katika kuwaletea huduma Watanzania lakini kuwaletea huduma Wana Tandahimba.

"Niwashukuru viongozi wa Serikali kwa majibu mazuri waliyoyatoa kwenu, kazi kubwa tuliyokuwa nayo ni kuhakikisha tunazungumza na wananchi tukayaeleza haya tusisubiri mpaka viongozi wakubwa wanakuja, ndio tunatoa majibu.Kuna watu wanang'onoka nong'ona wana hofu, msiwe na hofu tumekuja kusikiliza na tutatafuta majibu, "amesema Shaka.

Akizungumza zaidi Shaka amesema CCM ndio iliyoomba ridhaa kwa wananchi ,hivyo wanakila sababu ya kuwasikiliza huu ndo muda muafaka."Tukisema tunakuja 2024/2025 mtatuhukumu lakini sasa hivi tunakuja ili mtuambie kama mambo yanakwenda vizuri,"amesema.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...