Na Said Mwishehe,Michuzi TV,Mtwara

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema  hakitamtazama mtu machoni  katika jambo linalogusa maslahi ya wananchi ambao wametoa kura nyingi kwa Chama hicho wakiwa na matumaini kuwa changamoto na shida zao zitatuliwa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akiwa mkoani Mtwara.Amesema inasikitisha kuona  katika baadhi ya maeneo Serikali inatoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwemo inayohusu huduma za jamii, lakini baadhi ya waliopewa dhamana wanaichelewesha.

“Sasa niwaombe baadhi ya ndugu zetu mliopewa dhamana kwenye maeneo nyeti kabisa yanayogusa maslahi na maisha ya Watanzania simamieni, tendeni uadilifu. Uzalendo uwe kwanza,” alisema shaka akiwa anazungumza na wananchi wilayani Nanyumbu baada ya kupokea taarifa ya kukwama kwa mradi wa maji wa Nandete, na kufanya  wananchi waendelee kukosa maji safi.

Hata hivyo, Shaka amewahakikishia wananchi wa Nanyumbu na Watanzania kwa ujumla Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi itahakikisha inasimama na wananchi kwenye changamoto zinazowakabili.

“Katika mambo yanayohusu maslahi ya wananchi hatuwezi hata siku moja kuona watu wachache ambao wamebeba ubinafsi ama maslahi yao binafsi wanasababisha kukwama kwa utoaji wa huduma kwa wananchi walio wengi,” alisema.

Shaka alisisitiza Chama hakitavumilia jambo hilo na kwamba kuna baadhi ya miradi imekuwa ikisuasua na danadana nyingi na huku wananchi wqkiendekea kupata shida.

”Rais Samia anatoa fedha nyingi sana kwa ajili ya kutatua changamoto za wananchi, lakini changamoto hizo hazitatuki. Chama hakiwezi kukubali kabisa kuona mambo yakiendelea hivyo," alisema.

Pamoja na mambo mengine Shaka alisema Rais Samia anaguswa na changamoto zinazowakabili wananchi, ndio maana amekuwa akitafuta fedha kutatua changamoto hizo huku akiahidi atakayoyaona katika ziara yake hiyo mkoani Mtwara na maeneo mengine yote atafikisha kwa Rais.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...