Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MSANII chipukizi wa muziki wa singeli nchini, Mwajuma Othman 'Mwajuma Chaupepo' kutoka lebo ya Peaktime atambulisha rasmi ujio wa EP yake "Kula ushibe" anayotarajia kuzindua Juni 17 katika Ukumbi wa small planet uliopo Tabata jijinDar es Salaam.
EP hiyo yenye jumla ya ngoma saba ambazo ni 'Ndoa', 'Ndala', 'Hatufanani', 'Fresh', 'Singeli Tamu', 'Tatizo Noti', 'Vibe' na 'Baby' ambapo amewashirikisha wasanii mbalimbali wanaofanya vizuri akiwemo Khalid chokoraa,Kinata mc,Manifongo na wengine wengi.
Mwajuma Chaupepo amesema amejipanga kuleta ushindani katika muziki huo, pia kufanya nyimbo kali ambazo zitamtangaza kimataifa.
" Nimejipanga kufanya ngoma kali, nimekuja katika kiwanda muziki wa singeli kuupeleka kimataifa na kutambulisha utamaduni wetu kwa sababu muziki huu ndiyo asili yetu".
Msanii huyo amewaomba watanzania na wadau wa muziki kumpokea na kusapoti kazi zake ili kufika mbali na kuleta ushindani katika soko la muziki nchini.
Mratibu wa matukio ya lebo, Peaktime, Bakari Khatibu amesema wameamua kusapoti singeli kutokana muziki huo kuwa na idadi kubwa ya mashabiki.
Aidha,Khatib ameeleza kuwa mara nyingi wamekuwa wakishughulika na mchezo wa ngumi na kupata idadi kubwa ya Mashabiki ambao pia wanapendelea kupata burudani za kimuziki hivyo kupitia Lebo hiyo wameamua kusapoti na muziki huo kutokana na kushabiana.
Msanii wa Muziki wa singeli Mwajuma Othman a.k.a Mwajuma cha upepo Akizungumza na waandishi wahabari mara Baada ya kutambulishwa rasmi kuwa chini ya Lebo ya Peaktime Media pamoja na kutambulisha EP yake ya "Kula ushibe" anayotarajia kuiachia Juni 17 katika ukumbi wa small planet Tabata ambapo EP hiyo ameshirikisha wakali mbalimbali akiwemo kinata Mc, Khalid chokoraa na Manfongo.
Msanii wa singeli Selemani Edgar maarufu kama Kinata Mc akiongea na machache na kuomba wadau wa muziki wa singeli kumpokea Mwajuma cha upepo kwani ana kipaji na upekee katika uimbaji wake .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...