Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

MKUU wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge ametoa Rai kwa Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Lindi na Mtwara kuhakikisha Jitihada za Serikali awamu ya sita za Kuvutia Wawekezaji zinafikiwa,ikiwa Ni Pamoja na kuchangamka Kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vipya .

" Rais Samia Suluhu anavutia Wawekezaji na  ameshasema nini kifanyike jinsi gani hayo yanatekelezeka  Maafisa Biashara  mnapaswa kufanya, Vinara wa Utekelezaji ni ninyi Maafisa Biashara tuone Uwepo wenu (Visibility). Lazima muelewe matarajio ya Nchi ili muyatimize.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea Uwezo Maafisa Biashara wa Mikoa ya Pwani, Dar es salaam, Mtwara na Lindi.

Amewaeleza kuwa Serikali imeamua kuanzisha Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Ofisi ya Rais TAMISEMI ili kuongeza ufanisi wa Sekta hiyo.

Amewataka kuhakikisha wanatoa huduma Bora kwa Wawekezaji na Wafanyabiashara.

"Lazima tutoe huduma bora, lazima tujue wateja wetu ni Wafanyabiashara, huduma bora inabadilika mara kwa mara kwa Wafanyabiashara" Ameeleza Kunenge.

Amewaeleza kuwa Tanzania tupo eneo la Kimkakati  Strategic position na kila Afisa Biashara anatakiwa kujua Fursa za Uwekezaji zilizopo kwenye Eneo lake.

Amewataka kusoma  na kutumia Takwimu za Taasisi mbalimbali katika Kushauri na Kufanya Maamuzi "Wawekezaji wanapokuja manawapa Takwimu gani? Amehoji Kunenge- 

"Wajibu wenu kuhakikisha Spidi ya Teknolojia  mnakwenda nayo mkishindwa mtakuwa hamfai Maafisa Biashara mnatakiwa msome kila kitu" amesitiza Kunenge

Ameeleza kuwa utafiti  unaonesha Maafisa Biashara  wanatumika zaidi kama wakusanya Mapato  badala ya kuwa wasaidizi na washauri wa  Wafanyabiashara na Wawekezaji. 

Amewataka baada ya mafunzo hayo kubadilisha fikra na mitazamo yao na kuwa watoa huduma  na msaada kwa Wafanyabiashara.

Nae Afisa Mtendaji  Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa Amewataka Maafisa Biashara hao kutokuwa maafisa Biashara wa Ofisini badala yake kuwasadia na Kushauri Wafanyabiashara.

Hata hivyo ,amekemea tabia ya  baadhi ya Maafisa Biashara kufoji Leseni za Biashara Daraja B na kuwaeleza kuwa sasa wameandaa mfumo ambapo leseni zote zitatolewa kwa njia ya mtandao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...