NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema maeneo ya Mapori Tengefu yatakayopandishwa hadhi kuwa Mapori ya Akiba ni maeneo yenye hadhi nzuri kwa ajili ya uhifadhi na hayana vijiji vya wananchi.

Ameyasema hayo leo Juni 20, 2022 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka kwamba Serikali itayapandisha hadhi maeneo ya wananchi.

“Hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii iligusia upandishwaji wa maeneo ambayo hayatahusisha vijiji vya wananchi, hivyo maeneo yanayokwenda kupandishwa hadhi kutoka mapori tengefu kuwa mapori ya akiba ni maeneo muhimu tu kwa ajili ya uhifadhi na hayana wananchi ndani yake” Amesisitiza Mhe. Masanja.

Ameongeza kuwa maeneo hayo ya mapori tengefu kutokana na umuhimu wake kwa asilimia kubwa yanatumika kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na utalii.

Amesema Serikali inapoona pori tengefu lina hadhi nzuri na sifa ya kuhifadhiwa zaidi kwa maslahi ya taifa hulipandisha hadhi kutoka pori tengefu kuwa pori la akiba vivyo hivyo pori la akiba linapoongezeka sifa linapanda kuwa hifadhi ya Taifa.

Mhe. Masanja amewaomba wabunge wanaopakana maeneo hayo wawe na uelewa wa pamoja huku akisisitiza kuwa ardhi ni mali ya umma na si ya mtu mmoja akiwaomba waache kutumia kauli zinazoweza kuwagawa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...