Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Profesa Siza Tumbo  (kushoto)  wakati alipokagua  pikipiki zilizopo katika Ofisi za Wizara ya hiyo Juni 8, 2022 jijini Dodoma, ambazo zilitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Maafisa Ugani kote nchini. Waziri Mkuu ameiagiza Wizara  hiyo kuhakikisha ifikapo Juni 12, 2022 (jumapili) ziwe zimeshakabidhiwa kwa Maafisa Ugani. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.)

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tano kuanzia leo Juni 8, 2022 hadi Juni 12, 2022 Wizara ya Kilimo iwe imeondoa pikipiki zote wizarani hapo na kuzikabidhi kwa wakurugenzi.

“Hii haikubaliki, Wakurugenzi wote waandikiwe barua waje wazichukue, kama kuna ufungaji wa plate number utafanyika huko huko. Jumapili saa 10 jioni ziwe zimefika kwa wahusika.”

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Juni 8, 2022) alipokagua Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo eneo la VETA, Dodoma na kukuta pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya maafisa ugani zikiendelea kuwepo.

Aprili 4, 2022 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Maafisa Ugani wote nchini. Vifaa ni pamoja na pikipiki.

Amesema tayari Mheshimiwa Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba wamepokea maelezo hayo na watayafanyia kazi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...