Na Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki ametoa wito kwa watanzania kutembelea vifutio vya utalii vilivyopo hapa nchni kwani masharti yaliyokuwepo awali yamepungua..

Mhe Ndaki ameyasema hayo Leo jijini Arusha kwa niaba ya waziri wa Mali asili na utalii Pindi Chana wakati akizindua maonyesho ya karibu Kili fear 2022 yalioanza Leo katika viwanja vya Kisongo magereza jijini Arusha.

Amesema kuwa watanzania na watalii wanapaswa kutembelea vifutio vya kiutalii kwa kiwa maeneo hayo yanafikika ikiwa ni pamoja na masharti kupungua.

"Nitoe wito kwa watanzania na watalii kutembelea vivutio vyetu vilivyopo hapa nchi kwani maeneo yanafikika lakini pia masharti yamepungua kwani Covid imeshaisha na ndio ilikuwa inafanya kuwepo masharti."aliongeza

Mwenyekiti wa kamisheni ya utalii Zanzibar Mohamed Mansour amesema kwa upande wa Zanzibar wanaumuunga mkono Raisi na wameweza kujumuika na Tanzania bara kutangaza utalii.

"Sisi Zanzibar tumeamua kuungana na Tanzania katika maonyesho haya ili kuunga mkono jitiada za kutangaza Royal Tour,"aliongeza Mansour.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa Arusha Ni salama na itaendelea kuwa salama na kama mkoa agenda yao ni kkuifanya iwe kitovu Cha matukio makubwa.

Mongela amesema kuwa maonyesho hayo yanatangaza nchi na jumuiya ya Afrika mashariki Arusha inafikiri jinsi ya kutengeneza mshikamano ambao utauza vivutio kitaifa ili nchi iweze kunufaika zaidi.

Mkurugenzi wa Kili fear Company ltd Dominic Shoo ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo amesema kuwa wmaefanya uzinduzi rasmi kuonyesha dunia kuwa Kuna utalii na kwamba Kuna mengi ya kujifunza.

Waziri wa mifugo na uvuvi Mashimba Ndaki akitembelea mabanda katika maonyesho ya karibu Kilifear   yaliyoanza leo katika viwanja vya kisongo magereza jijini Arusha
Mkuu wa mkoa Arusha John Mongella akizungumza na waandishi kuhusu maonyesho hayo
Mkurugenzi wa Kilifear Company ltd Dominic Shoo waandaaji wa maonyesho hayo
Mwenyekiti wa kamisheni ya utalii Zanzibar Mohammed  Mansour


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...