Na Amiri Kilagalila,Njombe.


Wananchi wilayani Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kuwaficha watu wenye ulemavu wakati wa zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika agosti 23 mwaka huu.

Wito huo umetolewa na Bonfas Hilary mratibu wa sensa ya watu na makazi halmashauri ya mji wa Njombe katika vijiji vya kata ya luponde wakati wa ziara ya kikazi ya mkuu wa wilaya ambapo anasema kitendo cha kuwaficha walemavu wasihesabiwe kinawakosesha haki ya kupata huduma za kijamii.

“Kama una mlemavu ndani wa aina yoyote mtoe ahesabiwe,afahamike ili hesabu yake nayo iingizwe kwenye mipango ya taifa”alisema Bonifas

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu sana katika mipango ya taifa kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Mtaalamu amesema vizuri pia kutakuwa na madodoso mbali mbali naomba sana wote tujitokeze tarehe 23 mwezi wa nane na tutoe ushirikiano ili tuweze kuhesabiwa ili nchi yetu iweze kupanga mipango thabiti ya maendeleo”alisema Kissa Kasongwa

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Madobore akiwemo Hery Mtega na Merina Sambanaye wamekiri kuelimishwa vyema juu ya sensa na kuahidi kujitokeza kuhesabiwa kwa maslahi mapana ya taifa na maisha yao huku wakiwaasa wale wenye tabia ya kuwaficha .


Sensa ya watu na makazi hufanyika kila baada ya miaka kumi ambapo kwa mara ya mwisho ilifanyika mwaka 2012 na mwaka huu sensa itafanyika kuanzia tarehe 23 mwezi wa nane mwaka huu.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa akitoa elimu ya sense alipofika katika vijiji vya Luponde wakati wa ziara yake ya kikazi ya kijiji kwa kijiji katika halmashauri ya mji wa Njombe.
Baadhi ya wananchi wa Madobore wakimsikiliza mkuu wa wilaya alipofika katika kijiji chao.

 
Bonfas Hilary mratibu wa sensa ya watu na makazi halmashauri ya mji wa Njombe akifafanua umuhimu wa sense ya watu na makazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...