Na John Walter-Simanjiro
MWENGE wa Uhuru upo mkoani Manyara ambapo umeanza mbio zake katika wilaya ya Simanjiro juni 13 ukitokea mkoani Kilimanjaro.
Aidha
Mwenge wa Uhuru mwaka 2022 umesita kufungua,kuweka mawe ya msingi
miradi mitatu katika wilaya ya Simanjiro ambayo imekutwa na dosari
mbalimbali.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Sahel Geraruma
amewataka viongozi kusimamia vyema miradi inayotekelezwa kwa fedha za
serikali ili walengwa ambao ni wananchi wanufaike na miradi hiyo kama
ilivyokusudiwa.
Moja baada ya kufanya ukaguzi kwenye mradi wa Ujenzi
wa darasa moja katika Shule ya Sekondari Terrat iliyojengwa kwa fedha za
mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19
mwaka 2021/2022 shilingi Milioni 20,0000,000 wamebaini kuwa limejengwa
chini ya kiwango.
Pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa mwaka 2022
Sahel Geraruma amelazimika kuwanyang'anya leseni madereva sita wa
Kikundi cha Vijana wanaofanya biashara ya usafirishaji kwa kutumia
pikipiki (bodaboda Family) kilichopokea mkopo wa Halmashauri shilingi
Milio 14,100,000 kwa kushindwa kujibu maswali yanayohusiana na usalama
barabarani na kuwataka kurudi darasani kujifunza na kuelewa alama na
ishara barabarani.
Pia Mwenge wa Uhuru uligoma kuweka jiwe la Msingi
katika mradi wa kituo cha Afya kata ya Terrat inayojengwa kwa fedha za
tozo kutoka serikali kuu kwa gharama ya shilingi Milioni 500.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022 katika mkoa wa Manyara zitahitimishwa Juni 19 katika wilaya ya Mbulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...