Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omari Mgumba akutana na Maafisa wa Mamlaka wa Mapato TRA na kuishukuru Mamlaka hio kwa kuwatembelea walipakodi hao wa Mkoa wa songwe kwa ajili ya kutoa elimu mlango kwa mlango kufanya hivo itapelekea uelewa mpana kwa wafanyabiashara wa Songwe kujua wajibu wa mamlaka na wajibu wakulipakodi.

Pia Mkuu wa mkoa aliendelea kwa kusema wafanyabiashara hao kutoa ushirikiano wa dhati kwa ajili ya kupata elimu ya kodi, kwakuhakikisha wasanimamia maneno na maelekezo ya Serikali ya Mh. Raisi wa Tanzania Samia Suluhu Hassan bila kutumia nguvu, bila kutumia mabavu na bila kutumia hila, Mamlaka ya Mapato imekua ikikusanya kodi kwa weledi kukutana na wafanyabiashara kuwapa elimu ili kujua umuhimu wa kodi na madhara ya ukwepaji kodiVilevile alitoa rai kwa wafanyabiashra wanapouza bidhaa watoe risiti na mnunuzi kudai risiti kwa kutokufanya hivo nikuikosesha mamlaka na serikali mapato yake halali na kudhoofisha juhudi za serikali.

Kwa upande wa Meneja wa Songwe wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Dickson Kimaro aliongezea kwa kusema ujio wa Maafisa hao kutoka Makao makuu utasaidia ongezeko la ukusanyaji wa mapato nakuondoa changamoto walizokua nazo walipakodi katika mkoa huo wa Songwe.

Pia Afisa uhusiano Mkuu Bw. MacDonald Mwakasindile kutoka Makao Makuu TRA amesema kuwa kuwa zoezi hili linafahamika kwa jina la mlango kwa mlango linalenga kuwahudumia wafanyabiashara ili kuangalia jinsi wanavyolipa kodi.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omari Mgumba akizungumza na maafisa wa TRA waliotembelea ofisini kwake kwa ajili ya kutoa elimu kwenye mkoa huo
Meneja TRA songwe Bw Dickson Kamaro
Afisa Uhusiano Mkuu Bw. macDonald Mwakasindile
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bw. Omar Mgumba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...