Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro amekabidhi pikipiki kwa Maofisa ugani katika Wilaya hiyo huku akiwataka kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa hasa kutoa elimu kwa wakulima.
Aidha ametoa onyo kwa maofisa ugani ambao watabainika kutumia vibaya pikipiki hizo kufanya biashara kama (boda boda) kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogoro amesema lengo la kutolewa kwa Pikipiki hizo ni kurahisisha utendaji kazi kwa maofisa ugani kuwafikia wakulima ndani ya Wilaya hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Anastazia Ruhamvya amewataka maofisa ugani hao kutoa elimi ya kutosha kwa wakulima wadogo na wa kubwa lengo ni kuboresha kilimo katika wilaya ya Same na kukusanya mapato zaidi.
"Malengo makuu ni kufikia ndoto za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan za kuongeza uchumi wa wananchi kupitia sekta ya kilimo kuijenga nchi yetu.Niwaombe maofisa ugani na wote wanaohusika kwenye kilimo kufanya kazi kwa uwaminifu na uwadilifu,"amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogoro akikabidhi funguo ya pikipiki kwa mmoja ya maofisa ugani wa Wilaya hiyo kama ishara ya ugawaji pikipiki hizo kwa maofisa ugani katika Wilaya hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Anastazia Ruhamvya ( aliyesimama) akizungumza wakati wa tukio la ugawaji wa pikipiki kwa maofisa ugani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...